Woman, i love you. Wanawake tunatiaga huruma, ujinga wa mwanaume ila tutautafutia excuse ili ionekane tu haikuwa ni kosa lao. Wao ni watoto kila siku, hawana ufahamu wa kulijua jema lipi na baya lipi
Ujue nasoma comments hadi macho yanapoteza uono; like seriously ndiyo tumefika huku?Mabinti wengi wa kazi wanatoka kwenye familia zisizojiweza, wanakuja kwetu wenye unafuu kidogo angalau wajipatie ridhiki watunze familia zao. Imagine huku kwetu wanapotutegemea, ndiyo wanakutana na hawa wabakaji tunaowaita waume zetu: disgusting.
Majority ni watoto ambao hawawezi kujitetea; hawa waume zetu wanatake advantage wa unyonge wao. Wanawatia mimba afu tunaishia kiwafukuza warudi vijijini kwao wakaongeze ugumu wa maisha. Tunashiriki kuharibu maisha ya watoto wa wengine, afu tunajifanya "watoto wangu wapo vizuri tu na tunaishi kwa amani"; amani ipi hiyo wakati mnapanda uharibifu kwa watoto wa wengine? Huyo Mungu haoni machozi na magumu mnayoyapanda kwa watoto wa watu?
Hivi maids si wanatakiwa watreatiwe kama watoto wa nyumbani, tangu lini wamegeuka kuwa wake zenu? Mwanaume asiyeweza kuheshimu mabinti wa nyumbani kwake; huko nje si ndiyo papuchi zinamtambua kwa zipu? Na kama anaweza kulala na maid ambaye ni kama binti yake, siku akikosa maid si ndiyo atahamia kwa binti zake au watoto wake wa kiume? Vijana wa kiume wajifunzie kukojoa kwa maids, na wewe baba mzima ukalale na maid; no wonder unakuta familia nzima imeambukizwa gonjwa kisa tamaa. Mnavyovipanda kwa mabinti wa wenzenu; mtavivuna kwa vizazi vyenu. Ngoja siku muingie kwenye familia zilizoshindikanika, mkatie mimba watoto wa watu afu mjifanye kuwatelekeza; maji mtaita mma.
Mijinga mingine haina hata haya, eti kuna maids wana makalio; kwa hiyo na mabinti zenu wakiwa na makalio mtawalala? Huo ufirauni wenu uwe na limit.