sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Leo mtoto wangu wa darasa la nne kaniletea barua kutoka shuleni kwao kwamba eti yafaa zaidi awe anabaki huko huko shuleni boarding asiwe anarudi nyumbani. Nikiwa kama mzazi wake hii barua ilinipa hasira sana, hhizi shule za sikuhizi wametanguliza sana pesa kuliko watoto wetu, Kuna kipindi walinilazimisha nilipie school bus yao kwa shule ambayo mtoto aanatembea na wenzake wa shule ya karibu kwa dakika 15 niliakatalia kabisa, na kwenye hili la boarding wala siwezi kujiuliza mara mbili, Huyu mwanangu bado ni mtoto mdogo anahitaji uangalizi wangu, huko boarding mpaka aende labda akifika miaka 17 wakati ambao analau ana akili ya maisha na hata ile miaka ya foolish age ya balehe imeanza kufifia.
kupeleka mtoto huko boarding chekechea , msingi na O-level ni kumuweka hatarini mtoto, kwa form 5 kuna angalau. Boarding tulizosoma enzi hizo na hizi za sasa ni tofauti sana, Dunia imepitia mabadiliko mengi sana,,, Elimu pekee isiwe kigezo cha kumtelekeza mtoto huko boarding, mtoto kuwa chini ya uangalizi wa mlezi ni kitu muhimu sana,,
Huko boarding kusema kwamba umtegemee mwalimu na patron / matron kulea mtoto ni kujidanganya, shule nzima nakuta matron anasimamia wasichana zaidi ya 300 na patron anasimamia wavulana zaidi ya 400, hivi atawezaje kuweka umakini wote kwa mtoto wako? hata ukiwapa zawadi watie umakini kwa mtoto wako unadhani wewe ni mlezi pekee anaefanya hivyo ?
Haya ni baadhi ya mambo hatarishi yanayoweza kumkumba mtoto akiwa boarding bila uangalizi wa makini wa mlezi:
MAPENZI YA JINSIA MOJA - Mambo ya ushoga na usagaji kwa shule za boarding yapo tangu zamani ila yalikuwa kwa uchache sana lakini siku hizi utandawazi umeenea sana na kusambazwa kionekane ni kitu cha kawaida kupitia mitandao ya kijamii, filamu, tamthilia, katuni, games, miziki.. watoto bila uangalizi wa wazazi wanaiga haya mambo kirahisi hasa wakiwa boarding ambako uangalizi wa karibu wa walezi haupo, Tabia hizi zinaweza kuanzia mabafuni, wakiwa mabwenini mida ya usiku, hali inakuwa mbaya zaidi pale wale wanaopenda kuonea wenzao wakianza kutumia ubabe wao kuwalawiti kinguvu wenzao hasa wale wenye sura nzuri za mama zao.
Haya mambo yapo kabisa, Mwaka uliopita kuna mtoto wa rafiki yangu wa kazini alifukuzwa shuleni kwa sababu ya kushawishi wenzake wawe wanamlawiti, hii tabia ilianza alipolazimishwa kinguvu kwa mara ya kwanza ila kwa sasa hawezi kuacha, ameshafundisha wengine huu mchezo ambao nao yawezekana wameanza kuwaingilia kinguvu wanafunzi wenzao na si ajabu moja wao akawa mwanao.
UONEZI - kaika shule za boarding ni kitu cha kawaida sana, na endapo mtoto wako akiwa mwathirika wa hii ishu anakuwa ni muoga anashindwa hata kukwambia. Nimeshuhudia uonezi ukipelekea mpaka wawanafunzi kulawiti na wababe usiku wakati walimu wamerudi makwa na matron anauchapa usingizi, likizo mtoto anarudi wiki 2 au mwezi ila akirudi shuleni anaanza kula vipigo miezi minne mfululizo, anapumzika likizo wiki 2 anarudi tena shuleni jehanamu, mlezi hujui chochote hapo.
HAKUNA MSAADA WA ZIADA WA TUISHENI - hizi hizi tuisheni zinakuwa na wanafunzi wanakua wachache au mwalimu anakuja nyumbani kumfundisha mtoto peke yake, tuisheni hizi zinasaidia sana wanafunzi ambao wakiwa darasa la wanafunzi wengi hawaelewi vizuri, walimu hawawapi umakini, wanaogopa au hawapati nafasi ya kuuliza maswali, walimu hawaingii madarasani, walimu wanafundisha kwa spidi kubwa kuzidi uwezo wao, n.k huku tuishen mwalimu anamfundisha mwanafunzi moja moja kwa umakini, Mwanafunzi anakuwa huru kuuliza maswali, Mwalimu anafundisha kulingana na spidi ya uelewa wa mwanafunzi, mwalimu hakosi vipindi, n.k. Tuisheni zinasaidia sana sio za kuzibeza hata kidogo.
Kuliko kupeleka mtoto boarding ni bora nitafute kijana aliemaliza degree ya ualimu anaetafuta ajira niwe nampa elf 5 kila siku jioni awe anakuja nyumbani kumfundisha mwanangu one on one kwa umakini zaidi kuliko huko boarding ambako wanajisomea bila msaada wa ziada.
USHAWISHI WA MAKUNDI MABOVU - Makundi mabovu nayo hasa kwa vijana wadogo wanaobalehe ni hatari kwenye mindset ya mtoto, kijana akiangukia kundi bovu nae ataanza kuziiga tabia zao kwa dhana ya kuonekana mjanja, tabia hizi ni kama ulevi wa pombe, kuvuta bangi, ngono zembe bila condom, wizi, n.k. hakuna jicho la mlezi hapo, hakuna wa kumuokoa tofauti na day ambako ni rahisi mlezi kujua mtoto kuna mahala anateleza kwa kuchunguza mabadiliko yake ama hata kuzipata habari zake mtaani,, vijana wa form 1 hadi 4 wapo kipindi cha balehe, ni vema uwe nao karibu