Wali kupika kwa gesi, unaweza kukausha?

Wali kupika kwa gesi, unaweza kukausha?

Pressure cooker inapika kuanzia birian, wali, ugali mpaka makande, supu na mboga za majani! Rice cooker sidhan kama inaweza fanya hivyo

Kama ni bachela ajikusanye anunue pressure cooker walau ya Von.
Ndio maan nkasema kuokoa gharama.
 
Nunua pressure cooker ya Von (around 250k) au kama una kauwezo kidogo nunua ya Nutri cook (around 300k).

Ukiwa na hizo ni swala la kubonyeza button wali unaiva.
Pesa ya kupata pressure cooker ipo kabisa mkuu, sema sikuwa na ufahamu wa hv vitu.. nitajaribu kuvifuatilia madukani ikiwezekana wiki hii nivute mzigo huo(Pressure cooker) kazi ya kupika hii kwa kweli naona tabu sana na inanipotezea time yangu
 
Fanya hivi..., kwanza ukaange na mafuta kisha tia maji ya baridi...., moto uwe kiasi..., pili ukianza kukauka maji weka mfuniko wa bati au chuma chini ya sufuria hapo sasa uache uendelee kuiva pole pole ila uwe unauangalia. Hiyo ndio siri ya kambi [emoji2308][emoji2308]
Hakuna haja ya kuweka mfuniko chini, badala yake vikichemka kabla ya kukauka apunguze moto, na mfuniko uwe tait, punguza tena moto ili uive taratibu kwa robo saa mpaka dak 20, Funua onja, kama kuna kiini subiri dak 10 mbele lazima utakuwa poa
 
Siwezi kula MamaNtilie siku zote, Kuna aina ya vyakula napika mwenyewe na nainjoi kabisa. Kuhusu bei ya Gas naimudu ndo maana Niko nayo.
Ng'ang'ana na ubishi uje uungue nyusi ufanane na msukule.
OPTIONS:
-Oa haraka,
-Mwambie mpenzi wako awe anakuja kukupikia,
-Endelea kujipikilisha ule vibichi.
Natania.Fuata maelezo unayopewa na wajumbe hapo juu.
 
Njoo nikuoe wewe kama unajua kupika kweli ili nami nijilambe vitam kutoka mapishi yako
 
Hapo ishu ni moto ...maji yakikaribia kukauka punguza moto ubaki kidoogo wali utaiva polepole
 
Wali hauhitaji moto mwingi ili uive,ule moto wa chini kabisa,ambao mara nyingi inakua changamoto kuukadiria ndio unahitajika kuivisha...ukiweza hilo,wali hautakusumbua.
 
Unachotakiwa kuelewa kwenye Mapishi ya wali kinachohitajika ni mvuke. Kaanga mchele wako kidogo tia chimvi na maji kiasi yatokeze kidogo juu alafu funika acha utokote kwa dakika kadhaa alafu shusha moto wako acha chakula kiive kwa moto mdogo sana. Imeisha hiyo
 
Pesa ya kupata pressure cooker ipo kabisa mkuu, sema sikuwa na ufahamu wa hv vitu.. nitajaribu kuvifuatilia madukani ikiwezekana wiki hii nivute mzigo huo(Pressure cooker) kazi ya kupika hii kwa kweli naona tabu sana na inanipotezea time yangu
Si uwe unaenda hotel au mgahawa
 
Ng'ang'ana na ubishi uje uungue nyusi ufanane na msukule.
OPTIONS:
-Oa haraka,
-Mwambie mpenzi wako awe anakuja kukupikia,
-Endelea kujipikilisha ule vibichi.
Natania.Fuata maelezo unayopewa na wajumbe hapo juu.
Unatania huku umemdhamilia dah
 
Ukiweza kubalance kupunguza moto basi umeweza wali ukishakauka maji hautaki moto kwaiyo punguza kabisa moto wa jiko lako utaiva vizur.
 
Wakuu nipeni ujuzi hapa,

Kila siku nikipika wali kwa kutumia jiko langu la Gas naona unanisumbua sana, kwanza hauivi pia unaungua sana chini ya sufuria, nimewaza hadi kununua Rice cooker Wenda itanisaidia kuivisha vizuri.

Kwa sasa sijaoa, mchumba wangu ni Mtumishi wa Umma anakujaga weekend tu na anapenda kupika vitu vya kukaangakaanga tu.
Kijana chapa kazi achana na mambo ya kuendekeza kula. Unakuwa kama wale jamaa wa makobazi bana.
 
Back
Top Bottom