Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Walimu hao mara baada ya kurejea nchini, walipata mwaliko wa Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba kuhudhuria shughuli za Bunge Mei 04, 2026 jijini Dodoma na kupokelewa kwa pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Prof Shemdoe na Waziri wa Elimu, Prof. Mkenda ambao ofisi zao ziliratibu ziara ya mafunzo ya walimu hao nchini India.
Sanjari na hilo, Prof. Shemdoe amewataka walimu hao kuhakikisha yote waliyojifunza nchini India wanaenda kuwafundisha wanafunzi madarasani na kwa vitendo ili wapate ujuzi utakaowawezesha kuwa wabunifu, wajasiriamali na uwezo wa kushindana katika ajira za ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kujiajiri.
Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Serikali iliwapeleka walimu hao wapatao 150 nchini India kwenda kujifunza namna wanavyoendesha shule za amali na kutekeleza mtaala wao wa elimu ili wakirejea nchini waweze kuwa chachu ya kutekeleza vema mtaala mpya wa elimu kwa kutumia vema teknolojia iliyopo katika kuwafundisha vijana wa kitanzania elimu ya ufundi stadi.
“Sisi tulichukua walimu 150 na kuwapeleka India ili waende kujifunza namna masomo ya elimu ya amali yanavyofundishwa ili wakirejea waje kuwa chachu ya kuboresha namna ya kufundisha masomo ya amali, hatua hii ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya mapema ya Mhe. Rais kwa wizara ya Elimu na yale aliyoyatoa wakati akizindua sera yetu ya elimu,” amesema Prof. Mkenda.