Walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega wameamua kugeukia Mahakama ili kudai haki yao baada ya Mkurugenzi wao, Ndugu Maiko Kachoma, kukaidi matakwa ya sheria na kupuuza maombi yao. Walimu hao, zaidi ya 150, wamempa notisi ya siku tisini kuhakikisha kuwa amekamilisha mchakato wa kuwatoa katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuwaunganisha na Chama cha Walimu Chakuhawata. Notisi hiyo inamtaka Ndugu Kachoma kushughulikia suala hilo mara moja, la sivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa gharama zake mwenyewe.
Inasikitisha kuona baadhi ya wakurugenzi, walioteuliwa kusimamia watumishi wa umma na kufuata sheria za nchi, wanageuka kuwa viongozi wenye kiburi na dharau. Ndugu Maiko Kachoma amejitwalia mamlaka makubwa kiasi cha kuonekana kama "Mungu mtu," akiwataka walimu wamuabudu ili awatekelezee matakwa yao. Hali hii inazua maswali kuhusu vigezo vinavyotumika kuwateua viongozi wa aina hii.
Walimu wamebeba mzigo mkubwa wa kifedha kwa kuchangisha zaidi ya shilingi 5,000 kila mmoja ili kugharamia huduma za kisheria. Fedha hizi, ambazo zingeweza kusaidia familia zao, sasa zimetumika kwa sababu ya ukaidi wa kiongozi mmoja. Ni haki kwamba Ndugu Kachoma atoe fidia kutoka mfukoni mwake kwa
inashangaza jinsi mtu anayekaidi sheria anaweza kutegemewa kutetea maslahi ya wananchi na kusimamia utungaji wa sheria. Tabia yake ya kiburi na ukaidi si tu inakera, bali pia inahatarisha uhusiano kati ya serikali na watumishi wa umma. Hata ofisini kwake, amekuwa kero kwa watumishi huku akijitambulisha kama "Afisa Kipenyo" au "Afisa Usalama."
Kwa mara nyingine, naomba mamlaka za uteuzi zimwangalie kwa makini Ndugu Maiko Kachoma. Kiburi chake kinazidi kuleta mgawanyiko na kuharibu taswira ya serikali mbele ya watumishi wa umma.