Walimu kuajiriwa na TSC badala ya Wizara kunaenda kutengeneza rushwa, undugu na kujuana kwenye ajira. Rais litazame hili linaenda kukuharibia

Ni sababu ipi iliyofanya OTEAS iondolewe....?? ..hili swali ni la kujiuliza mno!
Hakuna sababu maalum ila naona wameamua kubuni njia mpya ya kuchomeka ndugu zao kwenye ajira na watatumia mlango wa kujitolea ili kufanikisha adhima hiyo. Kama huamini subiri muda ufike utanambia
 
Kwani nani kasema njia ya kietronic haiwezi kutumika na TSC?
Bado haimeki sense kwa sababu tamisemi kama wizara wana facilities toshelevu na uwezo wa kusimamia hili zoezi kwa ufanisi mkubwa kuliko hicho kiidara kilichojaa wala rushwa
 
Huyu mama ummy mwalimu anapoekekea sio pazuri
Wakati anaingia alianza kufanya vizuri kwa kurekebisha makosa yaliyofanywa awamu iliyopita hasa kwa kuanza kuajiri kwa kufuata series ya miaka lakini ghafla anataka kuharibu utaratibu huu aturudishe kule kule tulikotoka
 
Rushwa na kujuana nchi hii hakuwezi kuisha. Kila nikiwaza Utumishi wanavyofanya kwa nafasi kubwa nachoka kabisa, wapuuzi wamekuja na mbinu mpya anzia mwaka jana. Nafasi zote zile nzuri na kubwa zinatangazwa ila kwenye interview hazitangazwi, watu wanaitwa kimya kimya ili waweze kuchomeka watu wao.
Mnafanya interview vizuri kabisa ila nafasi anakuja kupewa mtu ambae hakuwepo kabisa kwenye intvw. Nafasi wanatuachia tupasuane kiukweli ni za chini tu. Sasa huko kwenye walimu tunaenda kuuana tena
 
Mimi nalitazama hill swala kwa pande mbili, upande was chanya ; njia hii ikitumika itasaidia mwajiliwa kuchagua halimashauli anayopenda kufanyia kazi kuliko hivi sasa ambapo wengi hupelekwa halimashauli wasizotaka hivyo kuanza kuomba uhamisho.
Pili njia hii itasaidia kutatua tatizo la uhaba wa walimu vijijini kwa kuwa kila halimashauli itapeleka walimu sehemu yenye uhitaji mkubwa

Kwa upande wa hasi; swala la rushwa litatamalaki sana.kwakuwa hofu kubwa ni rushwa kutamalaki basi selikari ifanye yafatayo; iandae vigezo vitakavyotumiwa na tume kuajili walimu na vigezo hivyo visima miwe na selikari ,kama nikigezocha umri basi iwe hivyo isitokee mhitimu wa hivi karibuni ameajiliwa wakati wazamani wapo
 
Mimi naona wizara ndio iajiri lakini kazi ya kusambaza walimu kwenye vituo vya kazi ndio ifanywe na Tsc! Unless siungi mkono ajira kusimamiwa na wala rushwa Tsc!
 
Tume ya walimu ujinga huu
 
Kati ya tume za hovyo zinazopaswa kufumuliwa ni tume ya walimu...!

Tume imejaa vibibi vina roho mbaya kichizi halafu vinajifanya vina maadili kumbe vipiga madili vikubwa..nyambafu kabisa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…