Ninadhani wahusika wamesikia changamoto za utaratibu mpya,lakini tuwape "benefit of doubt " waanze utekelezaji wakikwama watarekebisha utaratibu.
Si vema kuhukumu kuwa huko halmashauri za wilaya rushwa na upendeleo umetamalaki,kiasi kwamba watendaji wote wilayani wataleta ndugu zao au watapokea rushwa kuleta watu wao.
Kwa uelewa wangu, wilayani Kuna Takukuru na Usalama wa Taifa ambao wako Kyle kuhakikisha kuwa haki inatendeka na taifa linakuwa salama.
Ushauri wangu
1). Maombi yatumwe kwenye hizo tume za Walimu za wilaya kupitia mfumo wa ki Electronics.
2). wakati wa kupanga ajira ,hizi tume zishirikishe tukukuru na TISS.
3).Tamisemi iwe inatoa vigezo na miongozo ya uendeshaji wa zoezi zima.
4).Tume itakayobainika kukosa maadili ya kazi zao iwajibike Mara moja.
Manufaa ya utaratibu mpya
1).Walimu wengi watapangiwa kazi maeneo waliyoombea kazi
2).Tume ya Walimu ya Wilaya husika itakuwa inafahamu mahitaji halisi ya Walimu kwa kila shule wilayani
3). Utaratibu wa kuajiri Walimu kutoka Makao Makuu Tamisemi,mara ya mwisho,ulisababisha Mwalimu mmoja jina lake kujirudia mara 196,(unapokuwa na idadi kubwa ya Waombaji na watalaam wa IT wasio na weledi).
4). wilaya za pembezoni,nazo zitapata Walimu waliokubaliana na mazingira ya eneo hilo (itaondosha walimu wengi kutoripoti vituo vya kazi au kuomba uhamisho ndani ya muda mfupi)