WALIMU: Kwa wale wanaotaka kubadilishana vituo vya kazi
Kwanza kabisa niwape pole kwa shughuli zenu za kila siku katika ujenzi wa taifa. Pia niwaombe Moderators wasiunganishd thread yangu wakaifanya kuwa reply ya thread nyingine,hii huniboa sana.

Moja kwa moja niende kwenye lengo la thread hii.Kumekuwa na ugumu mkubwa kwenye suala la watumishi hasa walimu wa sekondari kupata uhamisho kutoka TAMISEMI. Madai ya TAMISEMI ni kwamba Kuhama kwa Mtumishi kunasababisha uhaba sehemu anayotoka.

Kwa walimu wa S/Msingi ni rahisi kupata mwalimu wa kubadilishana naye kutokana na Masomo anayofundisha kutozingatiwa zaidi. Lakini kwa Mwalimu wa Sekondari,kama unafundisha Physics basi kuhama ni lazima umpate mtu wa Physics wa kubadilishana naye kutoka sehemu unayotaka kuhamia. Na hii imezidisha ugumu wa kuhama.

NATAFUTA MTU WA KUBADILISHANA NAYE KITUO CHA KAZI.

Mimi ni Mwalimu nimeajiliwa Mkoani Njombe Wilaya ya Ludewa,nafundisha masomo ya Physics na Chemistry. Nyumbani kwetu ni Kasulu Kigoma,hivyo basi natafuta Mwalimu wa kubadilishana naye kituo cha kazi yeye aje huku Njombe Ludewa mimi niende Kigoma Wilaya yoyote ile ilimradi niwe karibu na Nyumbani. Mtu huyo Sharti awe mwalimu wa Physics.

Napenda niwaombe mnitangazie tangazo hili kwa yeyote ambaye mnamfahamu anauhitaji wa kuhamia niliko. Tapeli yeyote asijidanganye kujifanya ananipigia. Wale watu wa kuja na gia ya kuniunganisha na mtu aliyeko TAMISEMI siwahitaji make nao ni Matapeli Mara Nyingi,nataka wa kubadilisha naye tu full stop.

Mawasiliano:

0622182501.
 
Kwa jinsi watu walivyorogwa na Dar (jiji chafu - mwenye watoto Dar ambae anamaliza mwezi hajaenda kumtafuta Dr Massawe et al aniambie, vurugu mtupu, joto, na kila aina ya changamoto za maisha lakini bado wanaamini kuwa usipokaa Dar utakufa) sijui kama utampata mtu wa aina hiyo!

Sijui itokeeje umpate mtu alieichoka Dar kama mimi - bahati mbaya kwa JF hii simuoni, labda utangaze gazetini! Kina Bujibuji na Bishanga wahame Dar? Wamerogwa kwani!
Dr masawe specialist mzuri wa watoto
 
Kwa ambao niwapenzi wa kusini karibuni jogoo amewika.nami nirudi tanga.
IMG_20210512_122246_2.jpg
 
Wewe ni Mwalimu (Msingi, Sekondari n,k) na unahitaji mtu wa kubadilishana naye kituo cha kazi?

Weka ombi lako hapa na wengine watawasiliana nawe.

Ni muhimu kuzingatia kuwa, ukiweka baruapepe (email), namba yako ya simu mtandaoni haishauriwi (at your own risk). Njia bora inayopendekezwa na JamiiForums ni kwa PM (Private Messages) ndani ya JF - kwa usalama wako na usiri zaidi.

MUHIMU: Ni vema kusema UPO wapi na ungependa KWENDA wapi ili wale wenye kutaka kuwasiliana nawe wapate urahisi wa kukutafuta ili kurahisisha mchakato.

Tunakutakieni utumishi mwema.

JamiiForums
Nipo Tabora manispaa (sec.) nahitaji kuhamia Korogwe DC au Tanga jiji.

[emoji96] PDF Files | HII HAPA ORODHA YA MAJINA YA WAFANYAKAZI WA SERIKALI WALIOPATA UHAMISHO AWAMU YA KWANZA NA YA PILI 2021 | LIST YA MAJINA IKO HAPA [emoji1484]

[emoji186] Kwa updates zaidi [emoji1484]

[emoji3504] Download App ya ElimikaZaid [emoji1484]

SHARING IS CARING [emoji1753]
 
Back
Top Bottom