Habari gani ndugu zangu,
Mimi ni mwalimu nimekuwa nikifanya mchakato wakubadilishana vituo vya kazi na mwenzangu tangu mwaka jana na mwezi uliopita TAMISEMI wametoa majina yetu (awamu ya tatu) kwenye tovuti yao.
Baada ya hapo tukawa tunasubiri vibali vyetu. Kilichonileta hapa ni kwamba wiki iliopita nilipigiwa simu na PS wa mkurugenzi wangu na kuniuliza kama mwenzangu ameshapata kibali chake nikamwambia bado,, akaniambia mwenzangu akipata kibali na kikishasainiwa na mkurugenzi wake nikipige picha au kukiscan alafu niende nacho halmashauri kwangu.
Nikamuuliza vpi kwani changu kimeshatoka akasita kidogo kisha akaniambia chako kipo njiani kinakuja, ila akasema cha mwenzio kikitoka tu wewe piga picha alafu uje nacho huku. Kwaharaka nikahisi huenda kibali changu kimeshatoka ila wanahisi nisije ondoka huku alafu mwenzangu asije .
Naombeni ushauri wenu ndugu zangu nafanyaje kwenye hili maana sielewi nafanya nini na naanzia wapi maana utaratibu wote nimeshafuata na uhamisho ni haki yangu.