MICHANGO YA HARUSI YA MTOTO WA MWENYE SHULE YA BAOBAB NI KERO.
Kwa kweli magufuli akifuta michango ya harusi nchi itaendelea at least ielekee kwenye Elimu,hapa shuleni kwetu Baobab secondary ni mwezi sasa tangu mtoto wa mwenye shule atangaze kuolewa.ajabu tukashangaa kuona bakuli la mchango linapita kwa wafanyakazi kitu ambacho kilitustaajabisha kwa kuwa kwanza wenzetu waislam huwa hawana mambo mengi na isitoshe kwa uwezo wa wamiliki hao ni wazi kuwa hawashindwi kugharamia hiyo harusi.
Kwa upande wangu mimi sasa hili swala naliona ni unyonyaji maana hata wafanyakazi wadogo wenye mishahara ya kima cha chini wamepangiwa viwango maalum vya michango,matokeo yake wengi wana madukuduku moyoni huku wale wapambe nuksi wakitumia nafasi hiyo kujipendekeza kwa wakuu.Pengine kinachoumiza zaidi ni kwamba binti huyo wa pekee kuolewa kwenye familia ambae alisoma hapahapa baobab na kupata alama za chini tuu kisha kwenda kusoma Saut na baadae alipomaliza akaajiriwa hapa shuleni ana tabia ya dharau na kujidai.
Hata walimu waliomfundisha kabla hawasalimii na kujiona yuko class ya juu.wakati alikuwa mwanafunzi kilaza tuu pengine ni nafasi ya wazazi wake ndio kapata kazi hapa ila angeweza kusota mtaani mwaka kwa tabia zake na uwezo mdogo.
Kinachoumiza zaidi ni wenye shule kuchukua list ya watoa michango na kuona nani na nani hawajachanga,na wale wafanyakazi wakawaida wenye kima cha chini mishahara wanavyolalama huku wakiwa hawana willing.katika maisha ya siku hizi kwenye suala la michango ya harusi kumekuwa na kasumba ya wengine kununiana kisa hujawachangia mchango ya harusi.wengine hufikia hadi kupunguza ukaribu.Katika hilo sijui kwa wale ambao hatutochanga maana hukawii kitengenezewa zengwe na Mwl Mkuu wa hapa maana ana fitna huyo kuliko kagame.ni kibaraka pandikizi.
Wito wangu ni kwamba watu wenye uwezo wajifunze kuwa responsible.michango ni kero,hali ya maisha ni ngumu huwezi kunipangia nitoe laki 1,bila ya utashi wangu kwa kudhani labda nitaogopa.na pengine iwe ni wito toka kwetu wenyewe.najua wale madictator watataka kunyanyasa watu sababu ya hili ila ifike mahali kuwe na masikilizano na sio kujifanya waungu watu.