Njoo Bukoba -DC nije
Ilemela
Nyamagana
Tanga Jiji
Kilimanjaro (Moshi mjini)
au
Bagamoyo ...idara sec0785373410
 
Mwl CORNERY yupo MWANZA-MAGU idara sec anatafuta mwl mwenzake wakubadilishana nae kutoka DODOMA MJINI,CHALINZE,KIBAHA,BABATI au MOROGORO.
NO:0753467270.
 
Njoo Arusha DC nije morogoro manispaa.idara sekondari.nafundisha ilboru sec. Mawasiliano 0764776655, au 0658221998
 
Watanga rudini kwenu mstaafu vizuri...njoo tanga kilindi nije iringa..mbeya mjini au rungwe...songea...bagamoyo...moro mjini..gairo...kilosa...mkuanga...rufiji....kisarawe...kibaha...ruvu....chalinze....rudini kwenu wanatangaaaaa....
 
[h=1]UTARATIBU WA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA[/h]
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1. Mamlaka za Uhamisho
Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003 Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na
Kwa maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yamekasimiwa kwa;

  1. Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
  2. Katibu Tawala Mkoa kwa uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na;
  3. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja kwenda kingine ndani ya Halmashauri.
2. Aina za Uhamisho
Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

  1. Uhamisho wa Kuomba
    1. Taratibu za Kuomba Nafasi:-
    2. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
    3. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo
    4. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake mwombaji atawasilisha maombi yake kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za yeye kuomba uhamisho huo.
    5. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake kwa barua akimweleza kupatikana kwa nafasi hiyo kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi.
    6. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
    7. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia. Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyoAngalizo:
      Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.
      Upatikanaji wa Majibu:-
    1. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
    2. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka ili kuepusha mwingiliano wa majukumu katika vituo vya kazi kwa mwaka.
    3. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
    4. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba.
    5. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.
  2. Uhamisho wa Kawaida
    • Uhamisho huu ni wa kawaida ambapo Mwajiri au Msimaimizi wa kazi anafanya uhamisho kwa sababu za kuboresha utendaji.
      Hata hivyo ili uhamisho huo ufanyike pia Mamlaka za uhamisho zinatakiwa kujiridhisha uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri anayohamishiwa mtumishi wa hakusababishi upungufu katika Sehemu mtumishi anakotoka au anakohamia.
      Uhamisho huu kwa kawaida unagharamiwa na Halmashauri inayompokea mtumishi na ile inayomruhusu kwa kumlipa gharama za kufunga mizigo kama ilivyoelezwa kwenye Kanuni L (8 na 13) ya Utumishi wa Umma ya Kudumu toleo la 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2010 kwa wakati. hivyo ni muhimu Mamlaka za Uhamisho kijiridhisha na uwezo wa Halmashauri kugharamia uhamisho huo ili kuepuka kuzalisha madeni kwa Serikali
      Pamoja na utaratibu wa uhamisho kuwa ni uhamisho kufanyika mara mbili kwa mwaka, uhamisho huu wa kawaida unaweza kufanyika wakati wowote katika jitihada za kunusuru utendaji katika kituo alichopo mtumishi au anachohamishiwa mtumishi kwa manufaa ya umma.
      Angalizo:
      Mtumishi atakayebainika kughushi saini za viongozi, kuomba au kupokea rushwa katika ngazi yoyote atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumfikishwa mbele ya vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
      Ni muhimu kwa Waajiri kujiridhisha na majibu ya barua za uhamisho kutoka katika Mamlaka za uhamisho ili kuona kama maombi yake yalifuata taratibu sahihi na watumishi waliopata majibu wanatayarishiwa mapema data sheet na kumbukumbu za utumishi na mshahara ili kuepusha usumbufu kwa watumishi na waajiri wanaowapokea watumshi.
      S
      O
      U
      R
      C
      E

      T
      A
      M
      I
      E

      B
 
[h=1]Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa[/h]
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1.0 Utangulizi
Usimamizi wa Watumshi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika masuala ya upandishwaji vyeo, mafunzo na uhamisho yameelezwa katika Sheria ya Utumshi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002, ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na Taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na Miongozo na Nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali. Kwa sasa taratibu za kusimamia masuala hayo ni kama ifuatavyo:-
2.0 Kupandishwa Vyeo
Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.
2.1 Nini kifanyike kabla na baada ya mtumishi kupandishwa cheo?

  • Mamlaka ya Ajira yaani Halmashauri inapaswa kutenga fedha na nafasi kwa ajili ya nafasi za vyeo vinavyaotakiwa kupandishwa kwa mujibu wa Miundo yao ya Utumishi na sifa za watumishi wanaotarajiwa kupandishwa vyeo.
  • Mwajiri anapaswa kuhakikisha watumishi wake wanapimwa utendaji kazi kwa kutumia mfumo wa Upimaji na tathmini ya wazi ‘OPRAS' ili kujua hali ya utendaji wao. Mtumishi atakayezembea katika hili asipopandishwa cheo, halitakuwa kosa la mwajiri bali ni kosa la kiutendaji la mtumishi husika.
  • Ukubwa kazini yaani elimu na uzoefu wa kazi pia ni kigezo muhimu katika kuwafikiria watumishi kupandishwa vyeo licha ya kuwa miundo ya utumishi iko kimya katika hili.
  • Ni muhimu idhini ya kupandishwa watumishi vyeo baada ya Kamati za Ajira za Halmashauri kumshauri Mkurugenzi awasilishe taarifa kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri husika ili litoe idhini, vinginevyo vyeo vilivyopandishwa vitakuwa ni batili.
  • Ni muhimu Vyama vya Wafanyakazi mahali pa kazi kupitia Mabaraza ya kazi vikashirikishwa katika maandalizi ya kupandisha watumishi vyeo ili kuepuka manung'niko yasiyo ya lazima mahali pa kazi.
  • Ni muhimu kwa watumishi wote wa Mamalaka za serikali za Mitaa kufahamu kuwa nafasi zozote za kupandishwa vyeo hazitaombwa mpaka pale itakapolazimika Mwajiri kuzitangaza.
2.2 Taratibu za kujaza nafasi za Uteuzi
Katika utumishi wa umma kuna Taratibu na Miongozo inayotumika kujaza nafasi wazi na vyeo vya uteuzi. Taratibu hizo ni kama zilivyofafanuliwa hapa chini:-

  • Nafasi za uteuzi zinapotokea katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ilivyo kwa taasisi zingine serikalini Waajiri watapaswa kutoa taarifa na mapendekezo ya maafisa wanaoweza kufikiriwa kushika nafasi hizo (majina yawe kati ya mawili na matatu) kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua za upekuzi kisha baada ya kupokea majibu ya upekuzi, Mamlaka za uteuzi zitaendelea na uteuzi na kutoa taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
  • Pale inapotokea ni lazima nafasi za uteuzi ikaimiwe, kabla ya kupata kibali cha kukaimu nafasi hiyo, ni muhimu baada ya Mtumishi kukaimishwa na Mamlaka ya Uteuzi, Mamlaka hiyo kuomba kibali cha kuwakaimisha Watumishi wenye sifa za kukaimu na kupata kibali cha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa umma kwa ajili ya malipo ya posho zao za kukaimu na kuwezesha zoezi la upekuzi kuendelea wakati wahusika wanakaimu.
  • Mara baada ya watumishi kupandishwa vyeo Waajiri wanapaswa kuhakikisha kuwa watumishi wanapewa barua zao za kupandishwa vyeo na wanabadilishiwa mishahara yao kwa wakati bila kuzalisha madeni kwa Serikali.
  • Mtumishi aliyepandishwa cheo atapaswa kuwa katika kipindi cha majaribio na atathibitishwa katika cheo alichopandishwa baada ya miezi sita tangu tarehe ya kupandishwa cheo.
  • Iwapo itaonekana mtumishi ameshindwa kumudu majukumu ya cheo alichopandishwa atajulishwa na kupewa sababu na nafasi ya kujieleza kwanini asivuliwe cheo hicho na kulingana na maelezo hayo anaweza kuongezwa muda wa majaribio.
2.3 Nini kifanyike iwapo Mtumishi hajaridhika na utaratibu uliotumika kumpandisha cheo?
Iwapo mtumishi ataona hakutendewa haki na Mamlaka yake ya ajira katika suala la kupandishwa cheo atapaswa kuchukua hatua zifuatazo;

  • Kumjulisha Mwajiri Malalamiko yake kwa barua,
  • Iwapo Mtumishi hataridhika na majibu ya Mwajiri, atapaswa kutoa malalamiko yake kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa uamuzi ambapo nakala ya barua yake itatumwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Pages: 1 2
 
[h=1]Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa[/h]
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

1.0 Utangulizi
Usimamizi wa Watumshi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika masuala ya upandishwaji vyeo, mafunzo na uhamisho yameelezwa katika Sheria ya Utumshi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002, ikisomwa pamoja na Kanuni zake za mwaka 2003 na Taratibu za uendeshaji za mwaka 2003, pamoja na Miongozo na Nyaraka mbalimbali zilizotolewa na Serikali. Kwa sasa taratibu za kusimamia masuala hayo ni kama ifuatavyo:-
2.0 Kupandishwa Vyeo
Mamlaka ya kupandisha vyeo watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa isipokuwa Walimu kwa mujibu wa Kanuni ya D. (f) na (g) ya Kudumu ya mwaka 2009 ni Halmashauri yenyewe.
2.1 Nini kifanyike kabla na baada ya mtumishi kupandishwa cheo?

  • Mamlaka ya Ajira yaani Halmashauri inapaswa kutenga fedha na nafasi kwa ajili ya nafasi za vyeo vinavyaotakiwa kupandishwa kwa mujibu wa Miundo yao ya Utumishi na sifa za watumishi wanaotarajiwa kupandishwa vyeo.
  • Mwajiri anapaswa kuhakikisha watumishi wake wanapimwa utendaji kazi kwa kutumia mfumo wa Upimaji na tathmini ya wazi ?OPRAS? ili kujua hali ya utendaji wao. Mtumishi atakayezembea katika hili asipopandishwa cheo, halitakuwa kosa la mwajiri bali ni kosa la kiutendaji la mtumishi husika.
  • Ukubwa kazini yaani elimu na uzoefu wa kazi pia ni kigezo muhimu katika kuwafikiria watumishi kupandishwa vyeo licha ya kuwa miundo ya utumishi iko kimya katika hili.
  • Ni muhimu idhini ya kupandishwa watumishi vyeo baada ya Kamati za Ajira za Halmashauri kumshauri Mkurugenzi awasilishe taarifa kwenye Baraza la Madiwani la Halmashauri husika ili litoe idhini, vinginevyo vyeo vilivyopandishwa vitakuwa ni batili.
  • Ni muhimu Vyama vya Wafanyakazi mahali pa kazi kupitia Mabaraza ya kazi vikashirikishwa katika maandalizi ya kupandisha watumishi vyeo ili kuepuka manung?niko yasiyo ya lazima mahali pa kazi.
  • Ni muhimu kwa watumishi wote wa Mamalaka za serikali za Mitaa kufahamu kuwa nafasi zozote za kupandishwa vyeo hazitaombwa mpaka pale itakapolazimika Mwajiri kuzitangaza.
2.2 Taratibu za kujaza nafasi za Uteuzi
Katika utumishi wa umma kuna Taratibu na Miongozo inayotumika kujaza nafasi wazi na vyeo vya uteuzi. Taratibu hizo ni kama zilivyofafanuliwa hapa chini:-

  • Nafasi za uteuzi zinapotokea katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kama ilivyo kwa taasisi zingine serikalini Waajiri watapaswa kutoa taarifa na mapendekezo ya maafisa wanaoweza kufikiriwa kushika nafasi hizo (majina yawe kati ya mawili na matatu) kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais -Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa hatua za upekuzi kisha baada ya kupokea majibu ya upekuzi, Mamlaka za uteuzi zitaendelea na uteuzi na kutoa taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
  • Pale inapotokea ni lazima nafasi za uteuzi ikaimiwe, kabla ya kupata kibali cha kukaimu nafasi hiyo, ni muhimu baada ya Mtumishi kukaimishwa na Mamlaka ya Uteuzi, Mamlaka hiyo kuomba kibali cha kuwakaimisha Watumishi wenye sifa za kukaimu na kupata kibali cha Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa umma kwa ajili ya malipo ya posho zao za kukaimu na kuwezesha zoezi la upekuzi kuendelea wakati wahusika wanakaimu.
  • Mara baada ya watumishi kupandishwa vyeo Waajiri wanapaswa kuhakikisha kuwa watumishi wanapewa barua zao za kupandishwa vyeo na wanabadilishiwa mishahara yao kwa wakati bila kuzalisha madeni kwa Serikali.
  • Mtumishi aliyepandishwa cheo atapaswa kuwa katika kipindi cha majaribio na atathibitishwa katika cheo alichopandishwa baada ya miezi sita tangu tarehe ya kupandishwa cheo.
  • Iwapo itaonekana mtumishi ameshindwa kumudu majukumu ya cheo alichopandishwa atajulishwa na kupewa sababu na nafasi ya kujieleza kwanini asivuliwe cheo hicho na kulingana na maelezo hayo anaweza kuongezwa muda wa majaribio.
2.3 Nini kifanyike iwapo Mtumishi hajaridhika na utaratibu uliotumika kumpandisha cheo?
Iwapo mtumishi ataona hakutendewa haki na Mamlaka yake ya ajira katika suala la kupandishwa cheo atapaswa kuchukua hatua zifuatazo;

  • Kumjulisha Mwajiri Malalamiko yake kwa barua,
  • Iwapo Mtumishi hataridhika na majibu ya Mwajiri, atapaswa kutoa malalamiko yake kwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa uamuzi ambapo nakala ya barua yake itatumwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Pages: 1 2
 
Eti wanajamvi kuna walimu ambao wanahama ju kwa ju kwa njia ya panya au corrupt?
 
njoo MUSOMA v
Nije PWANI
DAR
TANGA
ARUSHA
DODOMA
MOROGORO
KILIMANJARO
idara ya msingi
# 0653 351265
# 0753 629314
# 0785 077035
 
Njoo LUSHOTO nije KOROGWE, MUHEZA au TANGA MJI. Elimu Sekondari. 0717008771
 
Njoo Arusha DC nije morogoro manispaa.idara sekondari.nafundisha ilboru sec. Mawasiliano 0764776655, au 0658221998
 
NJOO KATAVI NIJE SUMBAWANGA. Idara sekondari. Mawacliano 0766842187
 
Njoo Lushoto Tanga idara ya msingi nije Moshi vijijini, Moshi mjini, Hai, Siha, Rombo. kama upo tayari 0758121353, 0717690221, 0684533627.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…