WALIMU: Kwa wale wanaotaka kubadilishana vituo vya kazi
Kiongozi hii inamaanisha kwa sisi ambao mchakato unaendelea kwa mkurugenzi unasubiri uhakiki upite au laa? Nauliza hivi kwa sababu mimi nimeshapata nafasi halmashauri ninayotaka kuhamia lakini nilipopeleka barua kwenye halmashauri yangu nilipo sasa nikaambiwa barua haitashuhulikiwa kwa sasa hadi vibali vitakapotolewa tamisemi. kwa maelezo yako hapo juu inaonekana wao wa halmashauri wanaweza kuandika tu barua ya kuomba kibali kwa katibu tawala na barua ikaenda kusubiria kibali Tamisemi. Tafadhali nielimishe zaidi isije ikawa halmashauri yangu inanicheleweshea uhamisho wangu.

Asante sana.
Hakuna uhamisho unaofanyika nje ya mkoa kwa sasa.Nimeuliza TAMISEMI kwa uhakika.Nasisitiza hakuna...Chanzo Changu ni cha kuaminika.
 
Ofa ofa ofa

Njoo NJOMBE MJI aje
1.kibaha
2.temeke
3.ubungo
4.kigamboni
5.chalinze

Eneo lolote kati ya yaliyotajwa hapo.

commred Chichimizi
 
NARUDI KULETA UPDATES ZA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA,
HAKIKISHA UNAELEWA VIZURI MAANDIKO YANGU
H
iv karibuni nilitoa updates kuhusu uhamisho wa watumishi wa umma.
Uhamisho ulishafunguliwa baada ya uhakiki kumalizika mwezi March 2017,

Kuna baadhi ya wakurugenzi wanawasumbua watumishi kwa kusema hawana barua na sababu zingine hao wakurugenzi waambieni watimize wajibu wao na ikiwezekana, waombeni wasaini hizo barua hata kwa kutoruhusu uhame, na ukisha ipata ipeleke mkoani wakitaa muombe akukatalie kwa maandishi yaani akusaini na kuweka recomendetion yake,

Ukisha maliza hapo njoo mwenyewe TAMISEMI NA BARUA ZAKO,
Kama unavigezo vya kuhama kibali kinatoka baada ya wiki mbili tu,

NB
KWA WALE WANAFUATA MKE AU MUME LAZIMA AWE NA CHETI CHA NDOA HALALI
NADHANI NIMEELEWEKA WATUMISHI
 
Kwa kawaida mwalimu anaefanya kazi jiji au Manispaa ni rahisi Sana kuhamia Manispaa au jiji na mwalimu Wa kutoka halmashauri ni ngumu kuhamia jijini au manispaa....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NARUDI KULETA UPDATES ZA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA,
HAKIKISHA UNAELEWA VIZURI MAANDIKO YANGU
H
iv karibuni nilitoa updates kuhusu uhamisho wa watumishi wa umma.
Uhamisho ulishafunguliwa baada ya uhakiki kumalizika mwezi March 2017,

Kuna baadhi ya wakurugenzi wanawasumbua watumishi kwa kusema hawana barua na sababu zingine hao wakurugenzi waambieni watimize wajibu wao na ikiwezekana, waombeni wasaini hizo barua hata kwa kutoruhusu uhame, na ukisha ipata ipeleke mkoani wakitaa muombe akukatalie kwa maandishi yaani akusaini na kuweka recomendetion yake,

Ukisha maliza hapo njoo mwenyewe TAMISEMI NA BARUA ZAKO,
Kama unavigezo vya kuhama kibali kinatoka baada ya wiki mbili tu,

NB
KWA WALE WANAFUATA MKE AU MUME LAZIMA AWE NA CHETI CHA NDOA HALALI
NADHANI NIMEELEWEKA WATUMISHI
Mkuu japo siwezi kupinga taarifa yako Ila kote hakuna taarifa za uhamisho kuwa unaendelea kama kawaida.

Ndio maana Wakurugenzi hawapitishi barua yeyote Wala huko TAMISEMI hawapokei barua na kufanyia kazi uhamisho kwa sasa.

Tusiwape matumaini ambayo hayapo kwa walimu.Uhamisho ukirudi kama kawaida itajulikana kwa watu wote
 
Back
Top Bottom