Yeye mwenyewe mwalimu, Ila nampenda ni mwalimu anayejielewa na kuumizwa na Hali ya walimu wenzie....manake muda mwingine na sie tunazingua, unakuta mwalimu hajipendi, yupo yupo anavaa Kama halipwi mshahara....Yani chizi si chizi, ukiuliza mazingira....khaaa sasa mazingira ndo yanakuzuia kujipenda?
Kwenye Kazi sasa, mwalimu anategea Kazi, hafundishi ipasavyo....kila siku yeye ana udhuru, kutwa kukaa chini ya mti kupiga majungu walimu wenzie na mwalimu mkuu. Akimaliza muda wa Kazi linabaki shuleni kuendelea majungu akiswitch mada ni Simba na Yanga.....haumizi kichwa kutafuta shughuli nyingine ya kuingiza kipato au kufanya professional development.....afu kutwa kupiga miayo kusubiri nyongeza ya mshahara, Kwa Kazi ipi ulofanya?
Walimu tujirekebishe!