balimar
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 7,743
- 13,657
1.0 Waungwana Habari zenu!!
Mimi nina wazo hivi kwanini hawa Walimu wetu waliomaliza Vyuo Miaka nenda rudi na hawa watu wa Afya tusifikirie kivingine kuhusu swala la Ajira.
Serikali inayo nafasi ya kuwasaidia hawa kwa mlango mwingine
Mathalani badala ya kuendelea kujenga shule na vituo vya Afya kwanini hawa wasingejiunga pamoja ili kukidhi vigezo vya kuanzisha hizo taasisi.
Maana kama serikali inaweza kutengeneza madarasa au Shule mpya kwanini wasiwajengee hawa hizo shule au vituo ya Afya kwa mikopo halafu wao waviendeshe kama private institutions na waanze marejesho ya mikopo hiyo itakayotolewa na serikali??
Nchi za wenzetu hili ni jambo la kawaida kuwasaidia graduates wao. Ndio maana humu wanochimba viwima virefu wahindi wamekopeshwa tu kwao mitambo na kazi inaendelea na kwetu hebu tubadilike jamani.
2.0 Nini faida ya mfumo huu?
Naona itasaidia kupunguza wahitimu wanaoranda randa mitaani kumbe wangeweza kuongeza tija kwenye kutoa huduma za Elimu na Afya kwenye jamii zetu bila kusahau kuwa hawa wamesomeshwa kwa gharama kubwa sana na hawajazalisha chochote
Serikali itapata mapato na pia mikopo hii itakuwa ni kama ni revolving fund. Maana hawa wakilipa zinafunguliwa Shule na Vituo vya afya vingine
Pia itasaidia kurejesha hata mikopo waliyopewa na HESLB kwasababu watakuwa wameajiliwa na watakuwa wanapata kipato
Kodi itaongezeka kwa kuongeza wigo wa walipa Kodi
Mwisho wataleta challenge dhidi ya taasisi za serikali hivyo itachochea ufanisi na hata hawahitimu itabidi wabanwe na sharti ya kujiunga na kuanzisha taasisi na wao ndio wataiendesha. Tungepata combination bora sana ya wahitimu wetu
3.0 Ninachoamini
Uwezo serikali yetu wa kufanya hivyo upo labda utashi wa kisiasa tu huo ndio haupo
Maana HAKUNA siku tutaacha kujenga madarasa kutokana na Ongezeko la watu ni Ubora iende kwenye kukopeshana wakishajiunga wapewe mikopo ya kujengewa madarasa au vituo vya Afya (Asset) na kamwe wasipewe hela wasaidiwe na vifaa vya kufundisha na vile vya tiba tiba
Hii inaweza kusaidia na ikumbukwe soon tuna ujenzi wa baya madarasa 8000 si mchakato uanzie tu hapo hapo tu jamani??