Walimu wa kiswahili wa shule za sekondari kuna mahali mnafeli pakubwa

Walimu wa kiswahili wa shule za sekondari kuna mahali mnafeli pakubwa

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Hivi mtoto wa fomfour miaka 17 hadi 20 inakuwaje hawezi kutofautisha Kati ya "r" na "l"
"Karibu" mtoto anaandika " kalibu"

👉Kwenye matamshi ya lugha binafsi siwezi tupa lawama hii ni kutokana na athari za kimakabila/kilugha

Lakini swala zima la maandishi imekuwa ni changamoto sana

👉Matumizi ya 'x" badala ya s
Matumizi ya vifupisho kwa Kila neno
👉Matumizi ya neno "h" hayazingatiwi kabisa kwa baadhi ya maneno
Mfano "haraka" mtu anaandika "araka"

Nitoe Rai kwa walimu wa kiswahili
👉Naomba muwe wakali sana kwa wanafunzi wenu. Msiweke vema tu bali mzingatie sarufi.

👉Kama hamuwezi kuwa wakali ebu kagueni sana miandiko ya wanafunzi wenu ni aibu mtoto anakaa shule zaidi ya miaka 11 hajui maandishi ya kiswahili vizuri na ni lugha mama?

👉Mbinu ya mwisho, andaeni midahalo ya kiswahili, lakini pia mwalimu tumia njia ya uhamasishaji "hali" kwa kutumia zawadi kwa mwanafunzi mzuri zaidi.

Ona tu huu uandishi huu👇
 
Attachments

  • Screenshot_20241203_101813.jpg
    Screenshot_20241203_101813.jpg
    105.4 KB · Views: 9
Wewe mwenyewe umeandika mfafeli
badala ya mnafeli, halafu bado unakosoa wenzako.
 
Wewe mwenyewe umeandika mfafeli
badala ya mnafeli, halafu bado unakosoa wenzako.
Sawa kakosea lkn haimaanishi ama haileti tija kukosea kwake ndio kurasimishe uandishi wa hovyo wanavyoandika hao wanafunzi wasasa!.

Hoja ya mweka mada ipo sahihi kabisa, ni kweli kuna shida ya uandishi tena ni kubwa sanasana hichi kizazi cha 1990 na 2000!. tena zaidi hawa wa 2000 ni majanga sana!.
Nafikiri pia hawajibidiishi ktk kujifunza na pia wanababaika na usasa ambao hauna tija, vilevile sio wasomaji wa vitabu maana vitabu hukuza uelewa wa lugha pia nje na maarifa pamoja na burudani.

Rai yangu ni lazima kifanyike kitu mbinu za ufundishaji ziimarishwe, pia wafundishaji wasishughulike na pesa tu, wao ni nguzo ktk hilo.
 
Kitu unachoandika kinaanza kutamkwa kwenye ubongo. Sasa ubongo hauwezi kutamkwa L halafu ukaandika R. Tatizo hili la matamshi ni uritthi kutoka ulipojifunza lugha utotoni. Ni ngumu sana kumrekebisha mwanafunzi hata utumie fimbo ya chuma. Kamuulize Magu akuelezee vizuri
 
Akikua ataacha.
Ila namna unavo tamka ndivyo unavoandika.

Wengine hata iweje R lazma atamke L .
 
Mkuu mimi menyewe nimezaliwa familia ambayo tunachanganya r na l lakini nilijatahidi sana kuishinda hii yote yanawezekana
Kitu unachoandika kinaanza kutamkwa kwenye ubongo. Sasa ubongo hauwezi kutamkwa L halafu ukaandika R. Tatizo hili la matamshi ni uritthi kutoka ulipojifunza lugha utotoni. Ni ngumu sana kumrekebisha mwanafunzi hata utumie fimbo ya chuma
 
Kitu unachoandika kinaanza kutamkwa kwenye ubongo. Sasa ubongo hauwezi kutamkwa L halafu ukaandika R. Tatizo hili la matamshi ni uritthi kutoka ulipojifunza lugha utotoni. Ni ngumu sana kumrekebisha mwanafunzi hata utumie fimbo ya chuma. Kamuulize Magu akuelezee vizuri
Inawezekana ni urithi lakini walimu wangekuwa wanasimamia hilo. Unaandikiwa insha mwanafunzi anatumia l badala ya r anatakiwa kuwekewa kosa ili ajirekebishe. Kuanzia elimu ya msingi hadi form six lazima mwanafunzi atakuwa ameshaelewa.
Inakera sana kuona mtu kamaliza chuo level ya masters au PHd afanye kosa kama hilo.
 
Kuna mikoa hata kiswahili tu ni shida, walimu wanatumia nguvu kubwa mno kufundisha , wengi unakuta wameathirika na lugha za asili.
 
Sasa kwa hawa walioishia njiani maybe form two or form four? Kwanini maandishi yawapige chenga darasani wamekaa zaidi ya miaka 8
Inawezekana ni urithi lakini walimu wangekuwa wanasimamia hilo. Unaandikiwa insha mwanafunzi anatumia l badala ya r anatakiwa kuwekewa kosa ili ajirekebishe. Kuanzia elimu ya msingi hadi form six lazima mwanafunzi atakuwa ameshaelewa.
Inakera sana kuona mtu kamaliza chuo level ya masters au PHd afanye kosa kama hilo.
 
Kwa nini tusikubaliane tu ukisema araka sawa ukisema haraka nayo pia sawa ili mradi tumejua unamaanisha nini. Mbona wasukuma maji wanaita magi lakini hatusemi.
 
Mi nilijua unaambatanisha mtihani labda sasa wewe hizo screenshot za mtu aliyeacha shule darasa la nne ndio umeona uwe ushahidi wako huyo mtu wako ni kwamba hata kusoma ni kwa tabu
 
Ukiona binti anatumia L badala ya R kwenye kuandika jua hapo kuna UTI sugu.

Mtu wa hivyo ki ukweli siwezi chati nae..

Na nikiona mwanaume unatumia L badala ya R yaani akilini nakuona kama Ume left group vile
 
Mi nilijua unaambatanisha mtihani labda sasa wewe hizo screenshot za mtu aliyeacha shule darasa la nne ndio umeona uwe ushahidi wako huyo mtu wako ni kwamba hata kusoma ni kwa tabu
Lakini mkuu nina imani watu kama hao umekutana nao
 
Back
Top Bottom