mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Walimu wanabezwa sana, hii siyo sawa! Kila anayelalamika anabambikizwa kuwa mwalimu kana kwamba ualimu ni kazi ya kudharauliwa! Sisemi kuwa walimu hawajalalamikia hii nyongeza ya ajabu ajabu ya mshahara, ila siyo kweli kuwa watumishi wengine hawalalamiki.
Tunajenga taswira kuwa ualimu ni kazi ya hadhi ya chini yenye kipato kidogo kuliko kazi zingine zote wakati si kweli! Nasema hii tabia ikome na ikome kabisa!! Kutokuheshimu walimu ni sawa na kutokuheshimu wazazi, matokeo yake ni laana tu.