Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Gari Moshi

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
680
Reaction score
421
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu,katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na kudaiwa pesa kila siku ambazo Waalimu uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu, je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?

Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote toka kwa wenye dhamana juu ya suala hili, hii inaonyesha kana kwamba wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa yeye utengeneza malipo mengine, tena ni lazima, mwanafunzi hasiye wakilisha pesa hiyo, basi stress zote za mwalimu zitamuishia mwanafunzi huyo.

Nawakilisha.
 
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu.Katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na pesa kila siku ambazo WALIMU uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu,je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?. Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote Toka Kwa wenye dhamana juu ya sualq hili, hii inaonyesha wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa

Nawakilisha.
 
Mpeleke mwanao shule za Binafsi zipo nyingi tu, unataka waalimu wamnunulie Limu mwanao? Watoe copy Kwa hela zao? We mwenyewe unajua hali ya shule zilivyo. Unakuja kuwasimanga waalimu huku wakati wanapambania watoto wenu Kwa plan B. Wakiamua kuacha mtoto wako hatajua hata kusoma.

NB: Ningekuwa Mwalimu nisingehangaika na toto la mtu hasa hizi shule za Umma,mnawalaumu wakati anafundisha darasa halina hata miundombinu bora na Lina wanafunzi 150
 
Nimeliandika mara zote hili. Kero kabisa. hasa hawa walimu wa shule za msingi.
Changieni elimu japo kidogo kwa ma teacher,wwe chukulia Kama motisha tu,hata Kama huna nenda shule au andika ki memo kwa teacher kua hauko vizuri akuache kwanza,atakuelewa tu!!
 
Ila walimu wetu hawa wa shule za serikali/umma na bure ni wabunifu sana(wasanii?).Wanapenda sana kuwachangamsha wazazi na walezi wa wanafunzi wao.

Hawataki wazubae kabisa. Hadi imefikia sehemu wazazi na walezi wamekuwa kama wanaangalia sinema za kutisha/horror movies! Jasho linawatoka tu. Funny,huh?
 
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu.Katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na pesa kila siku ambazo WALIMU uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu,je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?. Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote Toka Kwa wenye dhamana juu ya sualq hili, hii inaonyesha wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa

Nawakilisha.
Kama elimu ni gharama kanunue ujinga

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hela unazozisemea ukizikusanya kwa Mwezi zinaweza kufika 20,000?

Ungejua tunaosomesha Watoto private schools tunalipa kiasi gani hata usingejali kuhusu hizo 500 mia tano mnazochangishwa.

Waacheni Walimu wapate Morale ya kufundisha, mnataka hata baada ya kazi kubwa ya kuwafundishia watoto wenu wakose hata hela ya Bando ya Kuingia JF?
 
Hapana umekosea , hoja yake ni nzuri Sana na tunapaswa kui uliza serikali kwanini imekuwa hivi, hiyo michango ni halali ili Hali serikali Ina gharamia . Wazazi wengi Ina waghalimu hii
Mimi nimejibu hoja yaje kama alivyoileta, nina sababu ya kumuuliza niliyomuuliza.

Mantiki yangu ni kwamba, hizo shule za bure, ubure wake unasababisha maslahi mabovu mno kwa walimu, mwalimu take home ya 50k ataishi vipi? Sasa hao walimu hawawezi kukubali kufa njaa huku wanajiona, lazima watape tape kama mfa maji, sasa badala ya kuendelea kuwarushia kamba kama hizo za michango ili wasife, nyie mnataka serikali izidi kuwazamisha kwenye maji.

kama hizo shule michango ni mingi, mpeleke shule ya kulipia, huko hakuna michango.
 
Back
Top Bottom