Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Mleta mada hujaweka wazi haswa ni vitu gani mnalipia ambavyo wewe unadhani havina sababu ya kulipiwa?

Orodhesha hapa ili wenye dhamana wajue, weka total ya gharama zote ili wananchi waone na kufanya hitimisho.
 
Kwa swali lako,umejiandaa kuupokea ukweli au kubishana tu?
Sijajua wewe upo kiubishani,kama ndivyo Mimi sipo huko hapa hatufukui makaburi.Mwenda zake kafanya yake Kenda, sasa tupo nyakati tofauti, na ni awamu tofauti.
 
Ukitaka elimu ya shilingi 100 ipo, ukitaka elimu ya buku ipo, ukitaia elimu ya buku 10 ipo, ukitaka elimu ya laki Moja ipo , ukitaka elimu ya m1 ipo , ukitake elimu m10 ipo na ukitaka elimu m100 ipo.

Uchaguzi ni wako
Hapa tunazungumzia shule za serikali sio, Sant marry au nyinginezo, ni za akiba Sisi si za akina wao
 
Mpeleke mwanao shule za Binafsi zipo nyingi tu, unataka waalimu wamnunulie Limu mwanao? Watoe copy Kwa hela zao? We mwenyewe unajua hali ya shule zilivyo............ unakuja kuwasimanga waalimu huku wakati wanapambania watoto wenu Kwa plan B.......wakiamua kuacha mtoto wako hatajua hata kusoma.

NB: Ningekuwa Mwalimu nisingehangaika na toto la mtu hasa hizi shule za Umma,mnawalaumu wakati anafundisha darasa halina hata miundombinu bora na Lina wanafunzi 150
Umekurupuka sana kujibu

Kila mwezi shule zinapokea hela selikal kuu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia nankujifunza (shajala)

Zile capitation ndo kazi yake kununua rim na poa wanapewa fedha za miradi kama ujenzi wa madarasa nk

Kila mwezi
Zinafanya nini?
 
Tanzania siasa ndo inasababisha watu kutowajibika.
Unazaa mtoto afu unataka usomeshewe bure
 
Ukitaka elimu ya shilingi 100 ipo, ukitaka elimu ya buku ipo, ukitaia elimu ya buku 10 ipo, ukitaka elimu ya laki Moja ipo , ukitaka elimu ya m1 ipo , ukitake elimu m10 ipo na ukitaka elimu m100 ipo.

Uchaguzi ni wako
Kaanzishe utatupata
 
Mleta mada hujaweka wazi haswa ni vitu gani mnalipia ambavyo wewe unadhani havina sababu ya kulipiwa?

Orodhesha hapa ili wenye dhamana wajue, weka total ya gharama zote ili wananchi waone na kufanya hitimisho.
Unafikiri michango yenyewe ni pesa nyingi ni fikira za ujamaa ndo zinazo wasumbua, na michango yenyewe husaidia watoto lakini wana lalamika unadhani wana lipa laki hawajazoea kusomesha.

1. Mitihani ijuuma 500@ kwa kila mtihani.

2. Shilling 300 za uji kila siku.

3. Mchango wa 1000 kwa study tour kuenda kitandani.

4.mchango wa 200 ya karatasi na kuchapisha mitihani

5. Mchango wa 500 kwa mwezi ya ulinzi.

6.Tuition ya masomo ya ziada ya hesabu 500 kila mwanafunzi kwa madarasa ya mttihani std 4 na std 7.
Hela ndogo lakini kelele njooni huku private mujuinee ada 3m inalipwa kwa awamu 3. Usafiri 200k tour 100k tunalipa na bado tuna smile.
 
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu,katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na kudaiwa pesa kila siku ambazo Waalimu uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu, je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?. Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote toka kwa wenye dhamana juu ya suala hili, hii inaonyesha kana kwamba wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa yeye utengeneza malipo mengine, tena ni lazima, mwanafunzi hasiye wakilisha pesa hiyo, basi stress zote za mwalimu zitamuishia mwanafunzi huyo.

Nawakilisha.
Kuna shule jirani hapa Kila mwezi unadaiwa buku ya kuingia chooni...Cha ajabu choo kimejengwa na wafadhili kutoka ujerumani.....wanawafool wazaz kuwa ni Hela ya usafi...sasa unajiuliza hivi wanafunz siku hiz hawafanyi usafi kweny mazingira Yao ikiwemo choo?
 
Mleta mada hujaweka wazi haswa ni vitu gani mnalipia ambavyo wewe unadhani havina sababu ya kulipiwa?

Orodhesha hapa ili wenye dhamana wajue, weka total ya gharama zote ili wananchi waone na kufanya hitimisho.
Kwani wewe unamjua ni vitu gani ambavyo mzazi anatakiwa kulipia Kwa mwalimu kila siku au wiki?
 
Mpeleke mwanao shule za Binafsi zipo nyingi tu, unataka waalimu wamnunulie Limu mwanao? Watoe copy Kwa hela zao? We mwenyewe unajua hali ya shule zilivyo............ unakuja kuwasimanga waalimu huku wakati wanapambania watoto wenu Kwa plan B.......wakiamua kuacha mtoto wako hatajua hata kusoma.

NB: Ningekuwa Mwalimu nisingehangaika na toto la mtu hasa hizi shule za Umma,mnawalaumu wakati anafundisha darasa halina hata miundombinu bora na Lina wanafunzi 150
aache kwani kuna mtu kasema atoe hela zake, aache kwanza sasa kutakuwa hakuna mitihani mpaka kidato cha nne
 
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu,katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na kudaiwa pesa kila siku ambazo Waalimu uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu, je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?. Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote toka kwa wenye dhamana juu ya suala hili, hii inaonyesha kana kwamba wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa yeye utengeneza malipo mengine, tena ni lazima, mwanafunzi hasiye wakilisha pesa hiyo, basi stress zote za mwalimu zitamuishia mwanafunzi huyo.

Nawakilisha.
Kama polisi na vituo vya polisi.
 
Kuna wazazi wapo radhi kulipa 3M+ kwa ajili ya Elimu lakini wewe kuchangia pesa ndogo (kiduchu) ya masomo ya ziada na mambo mengine unafungua hadi thread.

Kama unaona Elimu ni ghali basi jaribu ujinga inawezekana usiwe ghali
 
Umekurupuka sana kujibu

Kila mwezi shule zinapokea hela selikal kuu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia nankujifunza (shajala)

Zile capitation ndo kazi yake kununua rim na poa wanapewa fedha za miradi kama ujenzi wa madarasa nk

Kila mwezi
Zinafanya nini?
Asante
 
Kuna wazazi wapo radhi kulipa 3M+ kwa ajili ya Elimu lakini wewe kuchangia pesa ndogo (kiduchu) ya masomo ya ziada na mambo mengine unafungua hadi thread.

Kama unaona Elimu ni ghali basi jaribu ujinga inawezekana usiwe ghali
Kipato akilingani, wewe hata ukiweza fungua shule ndani ya ndege fungua zote ni anasa tu elimu ile ile, bora kichwa kiwe timamu.
 
Hilo swala lazima litakuwepo ukizingatia ufanisi duni uliopo kwenye elimu ya umma kwa sasa, hasa baada ya vigogo kuanza kusomesha watoto wao shule binafsi na kuacha kuwekeza kwenye elimu ya umma ikiwemo pia kujali maslahi bora ya walimu nk.

Sasa kinachotokea hapo ni hao walimu kuwafanya wanafunzi mtaji kwa kutengeneza hata kichapisho ambacho atawaagiza wanafunzi wakilipie na kila mwalimu atakuja na style yake kwenye kutumia huo mtaji wa wanafunzi.

Ukichanganya na usimamizi duni basi wazazi wanajikuta kila siku ni watu wa kudaiwa pesa za kupeleka shule.​
 
Back
Top Bottom