Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Tetesi: Walimu wamegeuza Shule za Serikali kuwa Vitega Uchumi vyao

Kipato Chao hakikidhi mahitajii na muda wakufanyaa mambo mengine njee ya shulee pia imekuwa ngumu kwao ,hvyo wameonaa Bora wale huko huko wanakofundisha...
Hatukatai ila wa rasmishe Ili ipitishwe kwenye taratibu za kishule, kama zamani kulikuwa na Tuition hakukuwa na muda wa ziada mashuleni, siku hizi shule hadi saa 12:30jioni watoto wapo shule. Kilicho takiwa warudishe Tuition kiu rasmi, maana ilikatazwa awamu ya tano, awamu ya sita hakuna tamko rasmi hivyo tuition imerudi Kiana yake.
 
Kipato akilingani, wewe hata ukiweza fungua shule ndani ya ndege fungua zote ni anasa tu elimu ile ile, bora kichwa kiwe timamu.
Uzi haujahainisha hiyo michango ambayo anaona ni kama kitega uchumi kwa walimu wa shule za msingi. Kama wanataka wachangie pesa ya masomo ya ziada na mzazi hataki kuchangia isiwe kesi asichangie ili mambo mengine yaendelee
 
Mleta mada hujaweka wazi haswa ni vitu gani mnalipia ambavyo wewe unadhani havina sababu ya kulipiwa?

Orodhesha hapa ili wenye dhamana wajue, weka total ya gharama zote ili wananchi waone na kufanya hitimisho.
Soksi
Traki suti
Viatu
Kiti
Meza
Limu
Calculator
Mathematical set
Counter book 15
Sweta
Tshirt ya michezo
Kotama/Fyekeo
Jembe
Kikombe cha uji
Rula
Kalamu
Tai
School bag
Mkanda
Shati
Suruali/Sketi



MICHANGO MINGINEYO


Mchango wa uji

Mchango wa mlinzi

Mchango wa kuinua taaluma

Mchango wa walimu wa ziada

Mchango wa Mwenge

Mchango wa chama.


Just to mention few!!

We never been serious! Let us joke and things be as usual
 
Kwani members wa jamiiforum si inaeleweka tuna pesaa..?? Mbona comments za walio wengi zimejaa malalamiko tena?? [emoji4]

Kwa huo msaada mdogo wanaouhitaji walimu hasa hawa wa shule za msingi hemu tuwasaidieni tu, wana life gumu sana hawa walimu wa hizi shule za serikali.
 
Hilo swala lazima litakuwepo ukizingatia ufanisi duni uliopo kwenye elimu ya umma kwa sasa, hasa baada ya vigogo kuanza kusomesha watoto wao shule binafsi na kuacha kuwekeza kwenye elimu ya umma ikiwemo pia kujali maslahi bora ya walimu nk.

Sasa kinachotokea hapo ni hao walimu kuwafanya wanafunzi mtaji kwa kutengeneza hata kichapisho ambacho atawaagiza wanafunzi wakilipie na kila mwalimu atakuja na style yake kwenye kutumia huo mtaji wa wanafunzi.

Ukichanganya na usimamizi duni basi wazazi wanajikuta kila siku ni watu wa kudaiwa pesa za kupeleka shule.​
Asante, lazima tuweke madaraja maana ndivyo tulivyo umbwa pia tupo kimadaraja, hatuwezi mlazimisha mtu awezaye ishi Manzese akaishi Osterbay, kila mtu aishi kadri ya uwezo wake, ndio maana kila kitu kina madaraja.
 
Magufuli ndo alifuta michango?? Ukithibitisha hili nipigwe ban ya week.

Cc mods
Wapo watakao kupa link hapa hapa nina hakika. Hakuna kitu ambacho Magu akutolea tamko, vitu alivyotaka visipuuzwe alitoa tamko yeye mwenyewe.
 
Mpeleke mwanao shule za Binafsi zipo nyingi tu, unataka waalimu wamnunulie Limu mwanao? Watoe copy Kwa hela zao? We mwenyewe unajua hali ya shule zilivyo............ unakuja kuwasimanga waalimu huku wakati wanapambania watoto wenu Kwa plan B.......wakiamua kuacha mtoto wako hatajua hata kusoma.


NB: Ningekuwa Mwalimu nisingehangaika na toto la mtu hasa hizi shule za Umma,mnawalaumu wakati anafundisha darasa halina hata miundombinu bora na Lina wanafunzi 150
Umeongea pointi sana, wazazi wengine vichwa vimejaa fikra za ajabu
 
Wewe tukupe shule ya umma uendeshe wiki moja tu utatamani ukimbie nchi shule inamambo mengi mdah mwingine ata ako ka mshahara ka feisal inabidi ukatumie huko hili mambo yaende jamani ualimu unachangamoto sana nchi yetu
 
Habari zenu wote wanajamii Forum wenzangu. Napenda kuwasilisha mshangao wangu kwenu,katika hii awamu ya sita nimeshuhudia kuwepo na kudaiwa pesa kila siku ambazo Waalimu uagiza wanafunzi kwenda nazo wakitoa sababu mbali zisizo na kichwa Wala miguu, je pesa zinazopelekwa na serikali hazitoshi?. Pia kinacho nishangaza hakujawa na tamko lolote toka kwa wenye dhamana juu ya suala hili, hii inaonyesha kana kwamba wenye dhamana hii wame ridhia.

Mimi naona kama elimu ilipo kuwa ikilipiwa ilikuwa ni nafuu kuliko sasa, Kwa sasa kila mwalimu wa somo lazima atengeneze mazingira ya kipato cha ziaza wakati ule ule ambao serikali inamlipa yeye utengeneza malipo mengine, tena ni lazima, mwanafunzi hasiye wakilisha pesa hiyo, basi stress zote za mwalimu zitamuishia mwanafunzi huyo.

Nawakilisha.
Toa ushahidi usibwabwaje tu na tetesi
 
Kweli

Mock darasa lasaba dar'salam ,Kila mwanafunzi anatakiwa kulipa

1) Hela ya mtihani 4000
2) chakula 3000
 
Wapo watakao kupa link hapa hapa nina hakika. Hakuna kitu ambacho Magu akutolea tamko, vitu alivyotaka visipuuzwe alitoa tamko yeye mwenyewe.
Swala la Elimu Bure maua ni ya Kikwete japo maana yake ni mbovu kama unavyoona mnachangishwa michango ya Ovyooo
 
Back
Top Bottom