Bwajilo
JF-Expert Member
- Dec 5, 2021
- 361
- 926
Nakuunga mkono. Wengi wa hao ni roho ya kwa Nini wakidhani wanawatajirisha walimu. Hakuna mzazi mwenye mtoto private ataongea ujinga huu.Unafikiri michango yenyewe ni pesa nyingi ni fikira za ujamaa ndo zinazo wasumbua, na michango yenyewe husaidia watoto lakini wana lalamika unadhani wana lipa laki hawajazoea kusomesha.
1. Mitihani ijuuma 500@ kwa kila mtihani.
2. Shilling 300 za uji kila siku.
3. Mchango wa 1000 kwa study tour kuenda kitandani.
4.mchango wa 200 ya karatasi na kuchapisha mitihani
5. Mchango wa 500 kwa mwezi ya ulinzi.
6.Tuition ya masomo ya ziada ya hesabu 500 kila mwanafunzi kwa madarasa ya mttihani std 4 na std 7.
Hela ndogo lakini kelele njooni huku private mujuinee ada 3m inalipwa kwa awamu 3. Usafiri 200k tour 100k tunalipa na bado tuna smile.
Juzi nimeenda kikao cha wazazi kumwakilisha toto la uncle, nimekuta mkuu wa shule ameomba wazazi wachangie 500 kwa mwezi ili wapate walimu wawili wa mathematics na physics ambao shule hawapo. Kushangaza wazazi hawataki eti bora wakae bure. Nikashangaa sana.