Sera ya elimu bure ni ngumu sana kuitekeleza,unakuta shule yenye watoto 800 inapokea ruzuku ya sh 260,000 kwa ajili ya maswala ya steshenari kwa mwezi,pesa hiyo hiyo ununue chaki,karamu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia mfano lesson plan na scheme of work kwa walimu,baada ya hapo njoo kwenye mitihani ya robo mhula na nusu mhula,mtihani mmoja uliochapwa kwa watoto 800,tuchukulie uwe na page 3 kwa bei ya sh 50@ page =2400 pages x 50 = 120,000 kwa somo moja tu,je kwa masomo Tisa ni sh ngapi? Ni almost 1,000,000,wakati huo ukumbuke kuwa ruzuku kwa ajili ya steshenari ni 260000 kwa mwezi.
Hivyo 260,000 Mara 6 Months ni almost 1.5M,wakati mtihani mmoja tu wa robo mhula unagharimu 1M,je chaki,karamu na vifaa vingine vinatoa wapi pesa?
Hiki kitu ni kigumu sana,naongea kwa uzoefu wangu kama nwalimu,sasa ili kukidhi mahitaji lazima mwanafunzi achangie walau ream moja kwa mwaka.
Njoo kwa walimu wa part time,lazima walipwe,Njoo kwenye uji na pesa ya kumlipa mpishi.
Kiufupi Sera ya elimu bure inachangamoto sana.
Hivyo ukiona ni gharama acha kusomesha mwanao,lakini pia gharama hizi hazizidi 50,000 kwa mwaka.