Walimu wanawekwa ndani, wanadhalilishwa sababu ya ujenzi wa madarasa wakati si wakandarasi wala mafundi ujenzi. Nini maoni ya CWT kama chama?

Kwa hili TAMISEMI kaeni mfikiri upya mzigo mnao watwisha walimu ukiachilia mbali mzigo wa vipindi walio nao si haki na si sawa

Na CWT mpo kimya hata hamfuatilii mkaona ni madhila gani walimu walio chini ya chama chenu wana nyanyasika na kusurubishwa kwa kazi ambayo hawakuisomea na wala hawana ujuzi nayo.

Wakuu wa Wilaya wanadhalilisha walimu , wanawaweka ndani na maneno ya dhihaka sababu ya ujenzi wa madarasa? Mlifikiriaje kuwatwisha mzigo huu walimu?

Kwanini hizo pesa za ujenzi msiziingize kwenye account za vijiji au kata au hata halmashauri ili walimu waendelee na kazi yao ya kufundisha watoto? Mda mwingi walimu wanahangaika na mambo ya ujenzi hao wananchi wenyewe ushiriki wao duni sana sababu mmesha ingiza siasa huko, kwanini mnawaongezea majukumu walimu tena mazito yenye masimango na kuviziana?

Nasema kuviziana sababu vitu vingi vilivyo andikwa kwenye BOQ zenu haviakisi uhalisia wa bei zilizoko sokoni pia kuna vitu vingi sana havipo kwenye BOQ zenu wakati katika uhalisi vina gharimu pesa tena sana

Wakuu wa wilaya wana waweka ndani walimu kisa ujenzi umechelewa au upo chini ya kiwango, jaman hivi mwalimu aliye jifunza kushika chaki na kupiga kelele na wanafunz darasa la pili leo anahangaika na size za nondo ? Anahangaika na ratio za cement , ahangaike na mafundi wezi na wadokozi ambao ukipepesa macho tu wameshafichaa kilo 2 za misumari yaani siku nzima upo na ujenzi hayo kayasoma wapi kwenye cheti chake hata akastahili kusimangwa nankuwekwa mahabusu akiyakosea?

Lakini pia swala hili limeathiri sana ufundishwaji wa watoto huko madarasani maana mda mwingi ni vikao vya kamati na kuandaa mihutasari ya vikao kusimamia mafundi bado asimamie mitihani na asahihishe na kupanga matokeo ya mitihani ya wanafunzi hapo achilia mbali kuingia darasani kufundisha vipindi vyote tabu tupu huko.

Kibaya zaid TAMISEMI tarajieni kupata majengo ya hovyo kuwahi kutokea kwa sababu zifuatazo

1. Kuna baadhi majengo yamejengwa na tofali mbichi kabisa
2. Hatua za ujenzi kitaalamu hazikuzingatiwa kabisa kwenye majengo mengi kwa sababu:-
  • Mkuu wa wilaya naye ni makandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Mkurugenzi naye ni mkandarasi akienda site naye anamaelekezo yake
  • Afisa elimu naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Ofisa tarafa naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Mwenye kiti CCM wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake hapo bado mkuu wa mkoa, afisa tawala mkoa, Mwenyekiti wa Ccm mkoa na wengineo yaan miluzi hadi mbwa haelewi aende wapi.
  • Engineer wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye anatoa maelekezo yake tena ya kitaalam
lakin Cha ajabu mkuu wa wilaya anaweza kupinga maelekezo ya engeneer na akataka yafuatwe yakwake sababu yeye ndiye yeye [emoji28][emoji28][emoji28].
Tofali inafyatuliwa leo kesho inajenga [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] speed ya mwanga bora majengo na sio majengo bora kila mkuu wa wilaya anataka kabla tarehe 15 decemba 2021 awe wakwanza kukabidhi bora jengo sio jengo bora.

muwe na huruma nyie watu fedha hizi ni za mkopo tutalipa wakati majengo yatabomoka ndani ya miaka 5-10.

USHAURI: Kwanini TAMISEMI fedha hizi msiingize mapema sana ili kupunguza huku kufanya kazi kwa pressure kubwa na speed ambayo inachochea kabisa kupata majengo majengo yasiyo bora kabisa?

Lakini pia kwanini TAMISEMI msiingize fedha hizi kwenye account za vijiji au kata ili wao waunde kamati zao huko za vijiji na wananchi wasimamie ujenzi na walimu muwaache waendelee na wajibu wao ambao ni mzito sana kulingana na wingi wa wanafunzi? Hebu kaeni mlitafakari upya na kwa umakini swala hili hali si nzuri hata kidogo.
Ni wilaya gani limetokea hili la Walimu kuwekwa ndani na Wakuu wa wilaya? Tusaidie tupate ushahidi Mkuu.
 
Walimu wanateswa na kale ka msemo
‘Utafanya kazi ya kufundisha na majukumu mengine utakayopangiwa na muajiri wako’
Sasa hayo majukumu mengine ndio yanatesa kuliko kazi aliyonayo!
 
Ndio Kazi yao.Mimi Nina jamaa zangu wakandarasi na Wana maduka ya hardware walikataa hizo ofa za mil.20 kwa darasa full tena walipewa madarasa. 4 kila mja.

Hizo Kazi hazina faida labda uwe mjinga,walau bei zingekuwa 25-30 mil.kwa chumba kimoja full na furniture zake la sivyo waendelee kutumia wafungwa maana materials ziko juu Sana kuliko pesa ya ujenzi.
Afu unaambiwa pamoja na madawati au viti meza na kwa nchi mzima ni flat rate as if mazingira yanafanana
 
Ningekutajia mmoja kwa majina yake na kituo chake cha kazi hapa sema nitafichua utambulisho wangu.
Wife ni mwalimu kuna wakati anajisahau na kuniambia kilichotokea humo kwenye kura
Kuna Rafiki yangu nilikutana naye siku chache baada ya uchaguzi llikua weekend tukaenda Kupata moja moto moja badiri nikamnunulia Kvant tukagonga duh alifunguka ogopa sana walimu
 
Kuna wajinga atakuuliza " una ushahidi"? Wakati kinondoni watoto waliitwa na ccm kwenda kupiga kura siku mbili kabla ya uchaguzi. Waliahidiwa kulipwa 5000/= walioenda kufanya hivyo ni wadogo zetu, wapwa nk
 
Tunavuna zaidi ya tulichopanda ukipanda kilo moja unavuna magunia mengiiii
 
Acha muendelee kunyooshwa tu na CCM mpaka mtakaponyooka
 
Hayo ysnasababishwa na walimu wenyewe kukubali kutumikishwa na wanasiasa.Na hili la madarasa litapeleka walimu wengi sana lupango ksma sio kunyanyasika.Na matatizo ya walimu niyasiku nyingi ila bado hawapati akili yakuweza kurudisha heshima yao mbele ya jamii na wanasiasa.Lakini pia naona kama hii nchi imekua kubwa sana kiasi kinachofanya mambo mengi kufanywa kwa njia za zima moto.Viongozi wanapanga mipango ya haraka haraka bila kujali ubora na ufanisi ndo maana mtu anakuja na wazo la ovyo la mwalimu kusimamia ujenzi wa darasa.Walimu wawe makini na hili maana wataangushiwa sana jumba bovu wasipojitambua.
 
Nina kijiwe Cha welding,walikuja walimu kunipa kazi ya dawati 120 niifanye kwa siku 3 nime kataa,ni kitu kisicho wezekana.
Bora ulikataa kwasababu lazima ungefanya kazi chini ya kiwango alafu badae waje kukudhalilisha nakujichukulia ujiko wakisiasa kupitia mgongo wako kwakujionyesha mbele ya waandishi wa habari kua wamekamata fisadi uliyelipua kazi ya umma.
 
Uendeshaji wa Shule umewekewa sheria na kanuni. Hakika inashangaza kuona kukithiri kwa uvunjwaji wa sheria hizo kunakofanywa na watu ambao hawajatajwa kisheria katika usimamizi wa elimu.
Kuna kamati/Bodi za shule, Kuna idara za elimu na ukaguzi wa Shule. Kwa hali ya sasa naona Kuna haja ya kupitia upya sheria na kanuni za Uendeshaji wa Shule zetu. Kwa hakika mfumo wetu wa elimu umeparaganyika.
Mbaya zaidi, siasa zimeingia mashuleni, Shule zimekuwa sehemu za wateule na wanasiasa kutafutia umaarufu. Inasikitisha. Na mbaya zaidi, hao wanasiasa wenyewe waliowengi Shule zilikuwa shidi kwao na failures.
Wizara tafadharini, pitieni muundo wa usimamizi wa Shule na elimu kwa ujumla.
Umeongea jambo la msingi sana
 
Haya huwa ni mawazo ya mtu ambaye bado anawaza kizamani sana

Katika picha zote zilizo kuwa zinatumwa za wizi wa kura 2020 ulimuona mwalimu hata mmoja akifanya hilo? Mie nliwaona askari zaid , Mwalimu sikuwaona na wala sijaona picha hata moja ya mwalimu akifanya hicho unacho dai wewe sijui wewe mwenzangu kama uliona labda tuambie.
Walimu na watumishi wote wa serikali waliosimamia uchaguzi ndiyo vinara wa kuvuruga uchaguzi wa 2020 kwa kuingiza kura feki na kuchakachua matokeo ya majumuisho.
 
Mambo ya uchaguzi yana husiana nini na uzi wangu?
 
Kwa hili TAMISEMI kaeni mfikiri upya mzigo mnao watwisha walimu ukiachilia mbali mzigo wa vipindi walio nao si haki na si sawa

Na CWT mpo kimya hata hamfuatilii mkaona ni madhila gani walimu walio chini ya chama chenu wana nyanyasika na kusurubishwa kwa kazi ambayo hawakuisomea na wala hawana ujuzi nayo.

Wakuu wa Wilaya wanadhalilisha walimu , wanawaweka ndani na maneno ya dhihaka sababu ya ujenzi wa madarasa? Mlifikiriaje kuwatwisha mzigo huu walimu?

Kwanini hizo pesa za ujenzi msiziingize kwenye account za vijiji au kata au hata halmashauri ili walimu waendelee na kazi yao ya kufundisha watoto? Mda mwingi walimu wanahangaika na mambo ya ujenzi hao wananchi wenyewe ushiriki wao duni sana sababu mmesha ingiza siasa huko, kwanini mnawaongezea majukumu walimu tena mazito yenye masimango na kuviziana?

Nasema kuviziana sababu vitu vingi vilivyo andikwa kwenye BOQ zenu haviakisi uhalisia wa bei zilizoko sokoni pia kuna vitu vingi sana havipo kwenye BOQ zenu wakati katika uhalisi vina gharimu pesa tena sana

Wakuu wa wilaya wana waweka ndani walimu kisa ujenzi umechelewa au upo chini ya kiwango, jaman hivi mwalimu aliye jifunza kushika chaki na kupiga kelele na wanafunz darasa la pili leo anahangaika na size za nondo ? Anahangaika na ratio za cement , ahangaike na mafundi wezi na wadokozi ambao ukipepesa macho tu wameshafichaa kilo 2 za misumari yaani siku nzima upo na ujenzi hayo kayasoma wapi kwenye cheti chake hata akastahili kusimangwa nankuwekwa mahabusu akiyakosea?

Lakini pia swala hili limeathiri sana ufundishwaji wa watoto huko madarasani maana mda mwingi ni vikao vya kamati na kuandaa mihutasari ya vikao kusimamia mafundi bado asimamie mitihani na asahihishe na kupanga matokeo ya mitihani ya wanafunzi hapo achilia mbali kuingia darasani kufundisha vipindi vyote tabu tupu huko.

Kibaya zaid TAMISEMI tarajieni kupata majengo ya hovyo kuwahi kutokea kwa sababu zifuatazo

1. Kuna baadhi majengo yamejengwa na tofali mbichi kabisa
2. Hatua za ujenzi kitaalamu hazikuzingatiwa kabisa kwenye majengo mengi kwa sababu:-
  • Mkuu wa wilaya naye ni makandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Mkurugenzi naye ni mkandarasi akienda site naye anamaelekezo yake
  • Afisa elimu naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Ofisa tarafa naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake
  • Mwenye kiti CCM wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye ana maelekezo yake hapo bado mkuu wa mkoa, afisa tawala mkoa, Mwenyekiti wa Ccm mkoa na wengineo yaan miluzi hadi mbwa haelewi aende wapi.
  • Engineer wilaya naye ni mkandarasi akienda site naye anatoa maelekezo yake tena ya kitaalam
lakin Cha ajabu mkuu wa wilaya anaweza kupinga maelekezo ya engeneer na akataka yafuatwe yakwake sababu yeye ndiye yeye 😅😅😅.
Tofali inafyatuliwa leo kesho inajenga 😅😅😅😅 speed ya mwanga bora majengo na sio majengo bora kila mkuu wa wilaya anataka kabla tarehe 15 decemba 2021 awe wakwanza kukabidhi bora jengo sio jengo bora.

muwe na huruma nyie watu fedha hizi ni za mkopo tutalipa wakati majengo yatabomoka ndani ya miaka 5-10.

USHAURI: Kwanini TAMISEMI fedha hizi msiingize mapema sana ili kupunguza huku kufanya kazi kwa pressure kubwa na speed ambayo inachochea kabisa kupata majengo majengo yasiyo bora kabisa?

Lakini pia kwanini TAMISEMI msiingize fedha hizi kwenye account za vijiji au kata ili wao waunde kamati zao huko za vijiji na wananchi wasimamie ujenzi na walimu muwaache waendelee na wajibu wao ambao ni mzito sana kulingana na wingi wa wanafunzi? Hebu kaeni mlitafakari upya na kwa umakini swala hili hali si nzuri hata kidogo.
Wakati wanajenga nyumba zao nani huwa anafundisha ujenzi?
Shida itakua ni tamaa ya pesa wazionapo kwenye account za shul ma akili zinawaruka.
Hao waalimu ndo wanafundisha ma engineer sasa iweje wao washindwe kusimamia, hapo ni tamaaa ya pesa tu.
 
Comment kama ya mtoto wa darasa la kwanza 😅😅😅😅😅
 
Wakati wanajenga nyumba zao nani huwa anafundisha ujenzi?
Shida itakua ni tamaa ya pesa wazionapo kwenye account za shul ma akili zinawaruka.
Hao waalimu ndo wanafundisha ma engineer sasa iweje wao washindwe kusimamia, hapo ni tamaaa ya pesa tu.
Basi kama walimu ndo wanafundisha mainjinia.

Naomba upite hapo shule ya msingi Miembeni kuna mwalimu Madudu mwambie akufanyie oparesheni ya ubongo😎
 
Back
Top Bottom