Walimu wapya walioripoti makazini Halmashauri ya Mbinga wahenyeshwa

Bwana mdogo nakushauri upunguze speed mana nahsi pia Upo under probation kwa mwaka mmoja, hii approach ya kuja kumshitaki Mwajiri wako mitandaoni sio njia nzuri najua hata ofisi kwake hujafika kupata maelezo yake, naamini ungefika na kujieleza hata kidogo ungepewa kusukuma siku ila kuja kujiliza hapa inaonesha ni jinsi gani hujawa matured na huwezi ata kuwa na siri za vitu vya ndani
 
kweli hata nilichoandika hujaelewwa hata A wala B. Mimi sijawahi uwa mwalimu wala kuajiriwa na serikali hata kwa bahati mbaya hizo shida za serikali siijui. Sijacompare mishahara nilichouliza, ndiyo utaratibu yani unavyoongea ni kama vile kufanyiwa hivyo ni sawa na ndiyo utaratibu.
Usidhani kila mtu ana maisha magumu mimi si mwajiriwa wa serikali na wala sina kipaji cha kuwa mwalimu.
 

Nakushangaa unaongea kama uko nje ya nchi.
 
Nakushangaa unaongea kama uko nje ya nchi.
Nimeuliza hivyo wanavyotendewa mpaka mtoamada anasema asilalamike anashambuliwa ndiyo utaratibu? Maana ni kama vile watu mnakubaliana na mambo ambayo kimsingi siyo utaratibu kisa ni mazoea. Haijalishi yawe ni mazoea, kama siyo utaratibu wa mambo basi si sawa mtu akilalamika aonekane kama kakosea na hilo ndilo linafanya hadi watu nchi hii wachapwe viboko lakini lionekane ni jambo la kawaida tu
 
Angalau wewe unaona uhalisia... Nakumbuka niliajiriwa mwanzoni Kama mwalimu... Huwezi amini tulikua miezi minne Bila Mshahara na pesa ya kunikimu tulitanguluziwa 50,000 nyingine walilipa baada ya mwaka na zaidi... Kama Kuna kitu kilinivunja Moyo mapema Ni Hayo mazingira ya kudharauliwa na wakuu kuonekana sii chochote...
 
Sasa hii ipo Kisheria.. Je mtu asidai haki yake?? Hivi unajua Kada ya ualimu Imebeba watu wengi wanaotoka familia za vipato vya chini?? Kuna wengine wanahoji kabla ya ajira mtu uliishije... Sawa inaweza alikua anajishughulisha na shughuli ndogondogo... Lakini tukumbuke Ni Mazingira mapya na mageni kwake... Halafu Siyo kwamba pesa hazipo.. Tatizo Halmashauri nyingi hazina vipaumbele.
 

Rais mwenyewe aliacha ualimu akaenda kwenye siasa we unajifunza nini Chief [emoji23][emoji23]
 
Nchi hii inahitaji ukombozi mkubwa wa fikra aisee.
 
Nchi hii inahitaji ukombozi mkubwa wa fikra aisee.
Inasikitisha sana, na hizo ndizo fikra za waliobahatika kusoma, je waliokoo huko vijijini hawana exposure!
 
Posho imeanzishwa kisheria na serikali ajabu haitekelezwi na wanaopaswa kuitekeleza. Mtu anapotaka itekelezwe anaambiwa avumilie atalipwa baadaye.

Yaani sheria inavunjwa, anayepinga uvunjwaji huo anabezwa na kuambiwa ni kawaida avumilie.
 
Kazi ya ualimu ndo ilikuwaga kazi ya ndoto yangu ila maisha hayana formula nikajikuta nipo uku...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…