Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Mpendwa Baba Askofu Mwamakula!
Tunaomba msaada wa kumsaidia mwalimu Mohonia Joseph aliyekamatwa jana. Huyo ni mwalimu mwenzetu tusiokuwa na ajira ambao tulianzisha vuguvugu la kudai haki ya ajira. Alikamatwa jana majira ya saa 6 mchana na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Nyamagana, Mwanza na bado yupo ndani hadi sasa.
Hii imetokea baada ya sisi kutaka kuongea na waandishi wa habari (Press Conference) siku ya juzi siku ya Alhamisi ili kuueleza umma juu ya uhalisia wa maisha yetu pamoja na haki ya kuajiriwa. Ilishindikana kufanyika mubashara (LIVE) kama tulivyopanga kwa kuvurugwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza.
Hata hivyo ilifanyika baadaye lakini mwenzetu alikamatwa wakati akishughulikia utaratibu ili iachiwe kwa umma kupitia link ya mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali za habari nchini.
Kwa tetesi pia inasemekana wengine wenzetu waliofanikiwa kufika kwenye Press Conference nao wanasakwa ili kutiwa nguvuni mwa polisi.
Ndimi,
Mwakilishi wa walimu wasiokuwa na ajira,
12 Aprili 2025