DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

DOKEZO Walimu watakiwa kuhudhuria mafunzo ya mtaala mpya kwa siku 2 kwa malipo ya Tsh. 3,000 kwa siku!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kwahio mabadiliko haya hayakuhusisha wadau mpaka sasa yanavyokuja kuanza ni mafunzo ya siku mbili ndio yatawafanya wawe competent ?

Hii nchi kila kitu politics na ulaji, ingawa hawa wanapewa buku tatu kuna watu wametengeneza matrilioni kutokana na haya mabadiliko..., Na sababu wahusika wakuu hawana ufahamu hadi kuhitaji mafunzo ya siku mbili inaonyesha ni jinsi gani huenda mabadiliko haya yasiwe na tija....
 
Wajumbe WA CCM hapo Dodoma juzi walichukua milioni mbili na.ngapi!!!???????🤣🤣🤣😂😂😂
Hii nchi
Ptuuuu
Hivi wale walilipwa? Siku wale wajumbe kutoka Zanzibar wanarudi nlikuwa bandarini... walikua wamewekewa utaratibu wa kupita free pale Azam aisee walikua wamechoka, hawapo nadhifu ukiwaangalia unaweza sema ni mtu aliyeeenda kulima Kiteto baada ya wiki tatu ndo karudi mjini😁
 
Serikali imebadili mtaala na kuanzia mwaka huu, wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kusoma mtaala mpya. Hivyo Serikali imeamua kuwapa semina walimu ili kuendana na kasi ya mtaala mpya.

Walimu kutoka Halmashauri X wametakiwa kuhudhuria semina ya mtaala mpya ambapo malipo yao ni sh. Elfu tatu kwa siku.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili jumla kila mwalimu atalipwa kitita cha sh. 6,000/=

Mimi ni mjumbe tu, na mjumbe hauwawi.

Hatari.. wamezidi kuwadharau walimu sana.
 
Ndiyo lakini sambamba na ngazi ya mshahara

Ila Walimu wengi wanaangukia kwenye extra duty ya 30,000 hadi 40,000
Kuna semina ilikuwaa ni elf 70 Kwa siku na Ilikuwa siku 6 ilisimamiwa na wizara na watoaji semina walitoka Baraza haikupita halmashauri ndio unafuu kidogo sijasikia Tena 😃😃😃
 
Serikali imebadili mtaala na kuanzia mwaka huu, wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kusoma mtaala mpya. Hivyo Serikali imeamua kuwapa semina walimu ili kuendana na kasi ya mtaala mpya.

Walimu kutoka Halmashauri X wametakiwa kuhudhuria semina ya mtaala mpya ambapo malipo yao ni sh. Elfu tatu kwa siku.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili jumla kila mwalimu atalipwa kitita cha sh. 6,000/=

Mimi ni mjumbe tu, na mjumbe hauwawi.

Huu ni upuuzi
Wagome kwenda
 
Hivi wale walilipwa? Siku wale wajumbe kutoka Zanzibar wanarudi nlikuwa bandarini... walikua wamewekewa utaratibu wa kupita free pale Azam aisee walikua wamechoka, hawapo nadhifu ukiwaangalia unaweza sema ni mtu aliyeeenda kulima Kiteto baada ya wiki tatu ndo karudi mjini😁
😀😀😀
 
Walimu kwa kweli ni dampo la kila ujinga,kama hawakujiandaa kuanzisha mtaala mpya si wangesubiri tu
 
yaani hiyo Afu tatu ni chai, unakunywa supu 1500 chapat mbili 6000, maji lita 1.5 bajeti mpata mwisho wa kikao 800. Jumla 2900 chenji inabaki 100.

Nauli unajitegemea...

chakula cha mchana unajitegemea....

Na tunataka watoto wafaulu kwa viwango vya divisheni wani......

Lakini kuna Watu wanalipana sitting alowance.

cc LIKUD
 
Back
Top Bottom