Walinzi wa kampuni ya SUMA JKT GUARD wana matatizo ya kisaikolojia

Pole sana mkuu. Nadhani pia mazingira yao ya kazi hayawaruhusu kufikiri sana.

Wanasema ukifikiri sana unampa mhalifu nafasi.
Kuna siku unaweza kutana na mwingine na akakusaidia sana mpaka ukabadili mawazo yako juu yao.
Mimi kuwekwa muda wote huo chini ya uangalizi sijui ningefanyaje dah!

Again, pole sana.
 
Reactions: apk
nchi ina mikasa kweli hii
 
Sawa poti
 
Hilo la kwanza, la pili ni namna walivyojiunga!

Wengi kwenye mchakato wa kujiunga walitozwa rushwa kubwa kubwa za kisiri, wakihamasishwa miujiza ya mafanikio pamoja na mambo yote uliyoyaeleza.

Tuseme nyakati zimebadilika pakubwa, enzi za utawala wa awamu ya4, vijana wengi walifanikisha ajira za vyombo mbali mbali vya ulinzi kwa njia hiyo, lakini leo ni tofauti.

Kama mtoa mada alivyosema, vijana hawa wanastahili kuangaliwa kwa jicho la 3, ama mfumo uliopo sasa ubadilishwe, iwe asipoajiriwa apewe kianzio.

Pia muda wote wakaapo chuoni wapewe angalao mshahara wa kiwango cha chini cha mfanyakazi wa serikali kuliko ilivyo sasa posho ya 50,000 wapewayo haitoshi hata kununulia suruali ya cadet.
 
Kwa upande Wangu Mimi naona wakome tu maana watanzania hawataki kujielewa Yani Alie Soma na ambae ajasoma wote no wale wale hamna utofauti

Kwanza nimeamua kua na roho mbaya mbele ya watu wasio jielewa hata kutoa msaada mpaka nikuhoji vyakutosha sio kirahisi rais na kuhusu hao vijana watachanganyikiwa Sana wakimalza hao kuchanganyikiwa

Watafata WAHITIMU wa vyuo mbali mbali maana hawana hata maarifa unakuta WAHITIMU kumi wa engineering wameshndwa hata kubuni kiwanda Cha vikombe vya plastic sasa hapo huruma ya nini

Tena chamsing kila MTU apambane na familia yake tu hawa watu wengne ni kuwakazia tu hakuna ujamaa jamaaa mwsho wake no kurudishana nyuma tu. [emoji41][emoji41][emoji41]
 
yaani wanapopita kusoma nyuzi kama hizi ndio mnazidi kuwatoa kwenye reli.

lakini jamani kwenye hizi kampuni za ulinzi kuna wizi nyiee!!!acheni kabisa.

mtu anaingia tenda ya kulindwa na askari anapigiwa hesabu ya laki 900k kila mlinzi.mlinzi anakuja kukabidhiwa 180k!!kweli!!!!wapo vijana nilikuwa nawahoji wa Guardaworld,wanakatwa mifuko ya hifadhi pesa hazipelekwi huko.

mawaziri mizigo wapo,manaibu mizigo wapo,wakurugenzi wapo,wakuu wa idara gani sijui wapo kazi ni kufuga matumbo na kuvaa miwani tu.
 
Reactions: apk
Siku hizi udom mnalindwa na suma jkt?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu , huu ujumbe kama hujaumalzia asee
 
Kuna kituko hapo Dodoma kwenye stendi zote mbili za mabasi, stendi kuu na pale kwenye soko kuu la Job, wapo hao vijana yaani ni tatizo kwa mustakabali wake!.
 
Mkuu umeongea ukweli mtupu kiukweli inasikitisha sana.
Wale watu mshahara wao ni laki 2 na take home ni laki 1 na 80.
Mtu ana mke na mtoto, amepanga room.
Nyuma ya pazia kampuni ya SUMA inavuta mkwanja sio chini ya 500K na baadae inatoa gawio ili isifiwe na watu.

Mwafrika ni kiumbe wa kipekee sana, yaani vijana wananyonnywa ili watu wakatoe gawio wasifiwe tu.

Hivi karibuni serikali ilitangaza kima cha chini cha mshahara ni 270K lakini serikali hiyo hiyo iko kimya watu wanalipwa 180K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…