Lucha
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 14,516
- 50,658
Acacia hayupo tena bulyanhulu walishindwana na serekali sahiv karudi barrick mwenyeweHawa wangepelekwa mgodini Bulyanhulu kwa acacia wawape darasa safi la ulinzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acacia hayupo tena bulyanhulu walishindwana na serekali sahiv karudi barrick mwenyeweHawa wangepelekwa mgodini Bulyanhulu kwa acacia wawape darasa safi la ulinzi
Kumbe acacia ashalala mitini!Acacia hayupo tena bulyanhulu walishindwana na serekali sahiv karudi barrick mwenyewe
Pole sana mkuu. Nadhani pia mazingira yao ya kazi hayawaruhusu kufikiri sana.Waliwahi niweka mtu kati kuanzia sa8 usiku Hadi sa3 asubuhi!! Utawala wa College of Education kisa chenyewe hakina kichwa Wala miguu, Mbaya zaidi mmoja wao akanipa namba yake aseeeh, Nilimtukana sijawahi tukana Wala kudharau kazi ya mtu Kama nilivyofanya kwa huyo, SUMAJKT
nchi ina mikasa kweli hiiWengine wapo bandarini pale wanapigishwa vibarua halafu wanalipwa buku sita tu kwa shift.......wakati vibarua wenzao ambao si watu wa suma wanalipwa zaidi ya iyo yani full unyonyaji kutoka kwa mabosi zao....wenyewe wanadai wao hulipwa 50 elfu tu kwa mwezi walitarajia pale bandari wangepata posho sawa na wenzao ili hata wajiendeleze kumbe wakubwa zao wamewageuza kitega uchumi cha kupiga ela za bandari.....
Huwezi kuamini. Suma jkt guard kuna vijana wasomi wazuri tu.
Suma ya miezi hii sio ile Suma ya wakati wanaanza kuchukua tenda za malindo ya kwenye taasisi. Wale wa mwanzo walikua ni wakali sana halafu uelewa wa mambo ulikua ni mdogo sana.
Vijana wenzangu wa Suma JKT guard msikate tamaa ya maisha. Wote hamuwezi kuwa polisi, magereza au JW. Tumieni kipato kidogo mnachopata kujiendeleza kwa fani mbalimbali za stadi za maisha lakini kupata mitaji.
Wengi wenu bado ni vijana wadogo. Nawasihi muache umalaya sio mzuri, kuna ukimwi na homa ya ini. Kuweni makini sana vinginevyo mtakwisha.
Hilo la kwanza, la pili ni namna walivyojiunga!Umeandika ukweli mtupu chief, hawa vijana walimezeshwa ndoto zenye mafanikio makubwa sana. Hivyo ilipelekea wakawekeza nguvu na akili zote kwenye kujitolea, then leo wamerudi kitaa wakiwa hawana mitaji, hawana ajira na wametoka mikono mitupu.
Wakiangalia wenzao waliokuanao mitaani, shuleni na JKT wamepiga hatua kubwa kimaendeleo....
Lazima wachanganyikiee
Siku hizi udom mnalindwa na suma jkt?Waliwahi niweka mtu kati kuanzia sa8 usiku Hadi sa3 asubuhi!! Utawala wa College of Education kisa chenyewe hakina kichwa Wala miguu, Mbaya zaidi mmoja wao akanipa namba yake aseeeh, Nilimtukana sijawahi tukana Wala kudharau kazi ya mtu Kama nilivyofanya kwa huyo, SUMAJKT
Yes, Kwa College ya Education na TIBA walichelewa kidogo kuja, ila huko kwingine nimewaona tangu First yr nahisi, TIBA wamekuja Nikiwa Finalists, then Education nimewakuta juzi Kati nimefata makaratasi yangu!!
NIC ya wapi hiyo maana nimefanya kazi hapo mbona washkaji wapo poa tuWalinzi wa Suma JKT hapa NIC Life House ni kichefuchefu kabisa, Kwanza ni wezi
mkuu , huu ujumbe kama hujaumalzia aseeSITOSAHAU JKT MKATABA ULIVYOISHA NA TUKALUDISHWA NYUMBANI-- "OP MAGUFULI"
ilikuwa ni mwaka 2016 naelekea kikosi cha mafunzo ya jkt kwenye gali unapiga mwimbo wa darasa -muziki... kozi ikaanza na hatimaye ikamalizika miezi 6 baadaye nkawa service man kikosi furani nyanda za kaskazini kuishi kwa taabu na mawazo ya lini ntapata ajira nkijitazama sina kitu chochote wala home sikuacha chochote ata kuku m1 wa kienyeji....
Miaka mitatu inakata tunasikia tetesi za tarehe furani tunaludi home wenzangu wakawa wanatoloka wanaludi makwao kupambana na vitu.vingine kabla kipenga rasmi hakijaliaa mimi npo nacheki mambo mpaka tone la mwisho hatimaye tukaambiwa tukusanye kila mali ya jeshi haraka iwezekanavyo hapa ni kombati,sahani,kikombe ,kofia na mkanda kama unao
Wasichana wakaanza kulia vilio c vya nchi hiii wanaenda wapi kukaa warudi tena home kukaa wengi hawakurudi mimi nkasema narudi kupambana kitaani kwetu na ntakaa home mpaka nipate mtaji hapa ndo MOVIE inapoanzaa.
Mkuu umeongea ukweli mtupu kiukweli inasikitisha sana.Habari!
Ukichukua matukio machache yaliyofanywa na hawa vijana wa SUMA JKT GUARD utagundua kuna kitu hakiko sawa. Kuna upepo umepunguza akili zao.
Majuzi Jangwani walimpiga yule jamaa wa African sports na kupelekea kifo chake, tena tunapokea taarifa kuwa wamemuua mwananchi asiye na hatia aliyekuwa akilima shambani kwake karibu na msitu wanaoulinda.
Juzi jioni wakati natoka kazini narudi nyumbani njiani nikakutana na kijana wa suma kabeba Kirungu, manati, pingu na vikorokoro vingine anatembea akiekekea lindoni. Jinsi alivyojifanyia camouflage utadhani yupo vitani kumbe anakwenda kulinda kaeneo kadogo tu.
Wale vijana wa SUMA wengi wao ni vijana wa JKT waliomaliza mikataba yao na kurudi nyumbani bila mitaji. Marafiki zao wengi ni vijana waliokuwa nao JKT ambao sasa ni watumishi wa JWTZ, TISS, ZIMAMOTO , UHAMIAJI, MAGEREZA na POLISI.
Wenzao wanakopa wanajenga, wananunua magari na kusaidia ndugu huku wao vijana wa SUMA wakilipwa kitapeli na kampuni yao ya ulinzi. Take home yao haifiki hata 250k, hawakopesheki benki, ajira yao kufukuzwa ni rahisi, hawana uhakika wa maisha ya uzeeni.
Muda wa kazi ni mwingi.
Hawa vijana wa SUMA wasaidiwe .
Ni vijana waliokosa dira, sasa wamebaki kujitutumua tu ili nao wahesabike kama wanajeshi.
Unajua JKT mtiti wake ni mzito sana, miezi 6 unakula kozi ngumu huku ukiendelea kulima kwa bidii, then umemaliza unaendelea kulimishwa zaidi kila siku. Unavumilia ukijua utafanikiwa mwisho wa siku unapewa nauli tu urudi kwenu, lazima uchanganyikiwe.
Hakuna anayekwenda JKT eti akajitolee tu kisha arudi nyumbani. Basi serikali itoe mitaji kwa vijana wanaotoka JKT bila ajira ya uhakika ili wakaendeleze fani walizojifunza huko makambini. Wa kufuga samaki au kuku akafuge, wa kujenga akajenge n.k
Hata chizi huwa hajijui kama yeye ni chiziHahahaa mbona mimi sina matatizo ya akili