Tetesi: Walinzi wa Prof. Lipumba waanza utekaji wa viongozi wa CUF

Tetesi: Walinzi wa Prof. Lipumba waanza utekaji wa viongozi wa CUF

Leo majira ya 2:30 asubuhi vijana wa Prof Lipumba wamefanya jaribio la kutaka kumteka MKURUGENZI WA UCHUMI NA FEDHA WA CUF ambaye ni K/NAIBU MKUU CUF BARA Mhe. Joran Bashange wakati akitoka nyumbani kwake eneo la Buguruni. Watekeji hao wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba ya Usajili T 760 CEX (pichani).

Baada ya jaribio la kumteka, walifanikiwa kumuingiza katika gari hiyo ya NOAH iliyokuwa na vioo TINTED. Bashange alipambana na kuomba msaada kwa kuita watu waliojirani kwa yowee la kuita "Majambazi" ndipo wananchi wakalizingira gari hilo na kuweka mawe na magogo na Polisi wakaitwa.

Polisi walipofika wakawakagua vijana hao na kuwakuta na pingu na silaha kadhaa na kitambulisho feki cha polisi.

Vijana watatu wamekamatwa na mmoja amefanikiwa kukimbia.
Mmoja kati ya vijana waliokamatwa ni mlinzi wa karibu wa Prof. Lipumba aitwaye HAJI "Mrangi" ambaye ni maarufu anajulikana kwa ushiriki wake wa vitendo vya kihuni na kiharamia kama hivi.

Katika mahojiano ya awali mmoja wa vijana hao ametoa ushirikiano na kueleza kuwa wametumwa na Abdul Kambaya na kuwa anayeongoza oparesheni yao hiyo ni mtu aitwaye Athumani (Mganga wa Kienyeji na Mwalimu wa mafunzo ya Kareti) aishiye Ilala akisaidiwa na watu wengine wanaojulikana Abubakar Fambo, Mohamed Ibrahim na Hassan Kingwele ( Mlinzi wa Magdalena Sakaya (MB).

Vijana hao waliokamatwa wanakiri kuwa mipango yote hiyo Prof. Lipumba anaijua kama vile walivyoongoza mpango wa kuhujumu Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF ulioahirishwa pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.

Mhe. Joran Bashange ameumizwa maeneo kadhaa ya mwili na anaendelea na matibabu na taarifa za ndani zinaonesha kuwa wahusika walielekezwa kumshambulia vibaya na kumuua ikiwa wangelifanikiwa kuondoka naye. Tukio hili linafanana na matukio kadhaa yaliyotokea huko nyuma na mfano utekwaji wa Dr. Ulimboka, Absalom Kibanda , Salma Said Kubenea na wengine.

Vijana waliohusika na utekaji huo na gari lao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Buguruni.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) kinalaani sana kitendo hicho na kinachukua hatua stahiki. Chama kinaamini kuwa kwa sasa Prof. Lipumba na watu wake wamekusudia kuendesha HUJUMA za wazi na kuvuka mipaka ya ushindani wa kisiasa za ndani ya Chama na kujivika joho la 'Uintarahamwe na Umungiki' wa wazi dhidi ya Chama na kuhatarisha na kutishia usalama wa maisha ya viongozi wa Chama.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma.
16 Septemba 2016.
ZITO KABWE kipindi anataka kukuzwa CHADEMA aliundiwa kila aina ya zengwe na propaganda walikuja hadi jukwani kutangaza kwa watu ZITO alivomsaliti lakini kwa tuhuma zote hakuna aliyetoa ushaidi hadharani za tuhuma za zito zaidi ya blaa blaa na kila aina ya propaganda.

Hivyo basi sasa hivi hiki chama cha CUF kinaungana na chama wenye wababe na waunda mizengwe ya kila aina maisha ya profesa lipumba CUF naisi ndiyo mwisho ukizingatia yuko tofauti na viongozi wa juu wa vyama vyote 2.

Watu ambao hadi picha ya mkutano wa kampeni wanatengeza na kuaminisha umma kuwa ya ukweli! Hivi kumfukuza profesa lipumba watashindwa? Jibu ni hapana profesa lazima ataondoka kwa kila aina ya hujuma lakini tumuombee huyu mchumi nguli kwenye vita hii nzito katika maisha yake
 
Profesa kama katumwa atalindwa na waliomtuma. Naona wanakwenda mbali sasa.
 
CUF fanyeni mambo yenu kisomi sio kutengeneza movie zisizo na faida
Hizi movie za kutekana na "kujiteka" ni kujishushia heshima tu.
Na wengine washapiga muvi nyingi tu za kutekwa na "usalama wa taifa" kujipa kiki.
 
Lipumba hawezi kukamatwa na nawahakikishia hawa jamaa waliokamtwa wataachiwa tu mapema!
 
Kama Lowasa yupo upanda wenu sitashangaa kuona movie Mpya kila siku .
 
Lipumba unalo, mwezio Dau huyoooooooo Malasya! chapa lapa kaka nenda japo Morogoro Univesity ukagange njaa pale CUF huna lako tena!
 
Haingii kichwani eti waliweka magogo hapa mjini pia hawakumdhuru hadi polisi walipofika ina maana muda wote walikuwa wanatazamana tu hakuna magari mengine yanapita hapa dar isupokuwa huyo jama wa CUF peke yake insue ya kupikwa
 
Ili naona uongo unasema walizingirwa na wananci wakajaa wakaliekea magogo mbele na nyuma police wakaitwa wakafika eneo la tukio mmoja akatoroka uongo uliokubuuu kabisa
Hugo mmoja alitoroka mbele ya umma wrote huo na
Watu walitoroka Vikindu pamoja na silaha zote zile iwe mtaani ndio ushangae?
Huu mchezo Mungu kanusuru ili mtu aaibike, hao waliokatwa watasema yote. Ila nitasikitika na kishangaa sana kama Magreth Sakaya atakuwa kahusila au kujua jambo hili na kukaa kimya.
 
Kama Lowasa yupo upanda wenu sitashangaa kuona movie Mpya kila siku .
Hata Slaa anatamani kurudi kwenye game anashindwa aanzie wapi!!

Hao watu nje ya siasa hawana kitu cha kufanya!!!
 
Hii nayo ni move kama zilivyo zingine nawashauri mkaigize upya, hii niya uongo mchana kweupe, kumbe na CUF wanazijua hizi move!!!
 
Mh!! Labda ni kweli....maana akili za yule bwana anazijua yeye.
 
Wote waliohusika katika jaribio la utekaji wachukuwe hatua za kisheria. Pia nashauri vyama viache siasa za chuki na uhasama bali vitumie fursa kujijenga na kuwatumikia wananchi bila kuwabagua. Tunaamini chama cha CUF ni kikongwe na kusimamia haki na usawa
 
Back
Top Bottom