Tetesi: Walinzi wa Prof. Lipumba waanza utekaji wa viongozi wa CUF

Tetesi: Walinzi wa Prof. Lipumba waanza utekaji wa viongozi wa CUF

kuna ushahidi gani umetolewa kuwa prof anahusika na tukio hilo?
acheni zenu bhannna,
hizo ni movie mnatuletea hapa,
story za paukwa pakawa
 
Hili tukio kwa kweli ni la ukweli ila mleta taarifa hakujipanga au ushabiki ulizidi. Ukweli ni kwanza watuhumiwa wamekamatwa, wasingekamatwa tungekuwa na mashaka, kama ni movie inakuwaje mlinzi wako anakusaliti na kwenda kuigiza na adui yako kukuchafua. Hivyo kwa kuwa watuhumiwa wamekamatwa sheria itawabnnana na ukweli utajulikana.
 
Sishabikii upuuzi lakini nadhani CUF tafuteni njia nyingine ya kufukuzana. Achaneni na vitimvi vaeni uhodari tuikomboe nchi. Matumbo yana mwisho wake. Mlishauvuka mpaka wa udini, uvisiwani na ubara. Mbona hili la Lipumba ni dogo sana?
Profesa, hata ungerudi kesho, usidhani utagombea tena urais 2020. Tulizana au nenda ACT au anza kingine cha Uramboni uwe m/kiti na Sakaya Katibu mkuu wako. Acheni njaa zenu mnamnufaisha adui.
 
ZITO KABWE kipindi anataka kukuzwa CHADEMA aliundiwa kila aina ya zengwe na propaganda walikuja hadi jukwani kutangaza kwa watu ZITO alivomsaliti lakini kwa tuhuma zote hakuna aliyetoa ushaidi hadharani za tuhuma za zito zaidi ya blaa blaa na kila aina ya propaganda.

Hivyo basi sasa hivi hiki chama cha CUF kinaungana na chama wenye wababe na waunda mizengwe ya kila aina maisha ya profesa lipumba CUF naisi ndiyo mwisho ukizingatia yuko tofauti na viongozi wa juu wa vyama vyote 2.

Watu ambao hadi picha ya mkutano wa kampeni wanatengeza na kuaminisha umma kuwa ya ukweli! Hivi kumfukuza profesa lipumba watashindwa? Jibu ni hapana profesa lazima ataondoka kwa kila aina ya hujuma lakini tumuombee huyu mchumi nguli kwenye vita hii nzito katika maisha yake
Tumia akili sio ushabiki tu, kwani ni nani ayejiuzuru uenyekiti, na ukijiuzuru siku Ukiwa na hamu nao tena unawaambia watu basi nautaka tena .
 
Hiii sasa na zaidi ya dhihaka kwamba Leo CHADEMA wanamachungu sanaa na CUF kuzidi profesa lipumba aliyepigwa,kuteswa na kulala mahabusu akiipigania chama chake. Maalim kama kawaida yake hawezi kuwepo kwenye matukio yenye historia ya utetezi wa waziwazi dhidi ya watu wa CUF na watanzania kwa ujumla.

Hii inayofanyika sasa hivi ata tukiendelea kubisha na kupotosha umma ukweli ni kuwa kuna hujuma dhidi ya profesa lipumba msione wanachama wamenuna la asha wana ya moyoni ipo siku watasema na hii siku kuna moja kati ya profesa au Maalim atabatizwa kwa moto.

Ingekua vizuri hii vita tuwaachie wenyewe wapambane kuliko kuweka propaganda nyingi mtandaoni na pia wana chama wa CHADEMA wasipike chakula ambayo hawatakuja kula ipo siku nao mambo kama haya haya yatawapata na wataanza kumtafuta mchawi lakini hawatampta kamwe ni wao tuuh ndo wanajiloga wenyewe.

Etii leo MTATIRO na genge lake wanaijua CUF kumzidi profesa lipumba hapa ndipo unaona siasa za Afrika bado kabisa Tena anatumia mda wake kushirikiana na marafiki zake kupotosha na kuficha ukweli wa ndani ya CUF Mimi yangu macho ila nawashauri CHADEMA waache vita kati ya maalim & lipumba wapambane wawili!!!
Hivi wewe ni kijana au mzee ?
 
ZITO KABWE kipindi anataka kukuzwa CHADEMA aliundiwa kila aina ya zengwe na propaganda walikuja hadi jukwani kutangaza kwa watu ZITO alivomsaliti lakini kwa tuhuma zote hakuna aliyetoa ushaidi hadharani za tuhuma za zito zaidi ya blaa blaa na kila aina ya propaganda.

Hivyo basi sasa hivi hiki chama cha CUF kinaungana na chama wenye wababe na waunda mizengwe ya kila aina maisha ya profesa lipumba CUF naisi ndiyo mwisho ukizingatia yuko tofauti na viongozi wa juu wa vyama vyote 2.

Watu ambao hadi picha ya mkutano wa kampeni wanatengeza na kuaminisha umma kuwa ya ukweli! Hivi kumfukuza profesa lipumba watashindwa? Jibu ni hapana profesa lazima ataondoka kwa kila aina ya hujuma lakini tumuombee huyu mchumi nguli kwenye vita hii nzito katika maisha yake
Hv lipumba kafukuzwa au aliondoka mwenyewe
 
Hahhahahah le professor si akaandike ma desa tu mchumi wa dunia /gunia
 
Aibu aibu sana!! Polisi wasipo kuwa wanapokea amri toka juu hi kesi mbaya zaidi kutokea Tanzania na sheria ifuate mkondo wake kwa kweli!! Iwe fundisho ila kama tu wanapokea amri toka juu.....wataiua hii kesi na kusema mambo ya uongo! Tusubiri
 
Ili naona uongo unasema walizingirwa na wananci wakajaa wakaliekea magogo mbele na nyuma police wakaitwa wakafika eneo la tukio mmoja akatoroka uongo uliokubuuu kabisa
Hugo mmoja alitoroka mbele ya umma wrote huo na
Nimekuelewa ndugu
Hoja ya msingi hiyo

Halafu eti walifanikiwa kumwingiza ndani ya gari katibu wa mpunga, akapambana halafu akapiga yowe
Inamaana hiyo gari ilikuwa imesimama tu?
 
ZITO KABWE kipindi anataka kukuzwa CHADEMA aliundiwa kila aina ya zengwe na propaganda walikuja hadi jukwani kutangaza kwa watu ZITO alivomsaliti lakini kwa tuhuma zote hakuna aliyetoa ushaidi hadharani za tuhuma za zito zaidi ya blaa blaa na kila aina ya propaganda.

Hivyo basi sasa hivi hiki chama cha CUF kinaungana na chama wenye wababe na waunda mizengwe ya kila aina maisha ya profesa lipumba CUF naisi ndiyo mwisho ukizingatia yuko tofauti na viongozi wa juu wa vyama vyote 2.

Watu ambao hadi picha ya mkutano wa kampeni wanatengeza na kuaminisha umma kuwa ya ukweli! Hivi kumfukuza profesa lipumba watashindwa? Jibu ni hapana profesa lazima ataondoka kwa kila aina ya hujuma lakini tumuombee huyu mchumi nguli kwenye vita hii nzito katika maisha yake
Lakini mi nadhani profesa aachane nao aje aturekebishie uchumi wa nchi
Michango yake kwenye uchumi inasaidiaga sana
 
Leo majira ya 2:30 asubuhi vijana wa Prof Lipumba wamefanya jaribio la kutaka kumteka MKURUGENZI WA UCHUMI NA FEDHA WA CUF ambaye ni K/NAIBU MKUU CUF BARA Mhe. Joran Bashange wakati akitoka nyumbani kwake eneo la Buguruni. Watekeji hao wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba ya Usajili T 760 CEX (pichani).

Baada ya jaribio la kumteka, walifanikiwa kumuingiza katika gari hiyo ya NOAH iliyokuwa na vioo TINTED. Bashange alipambana na kuomba msaada kwa kuita watu waliojirani kwa yowee la kuita "Majambazi" ndipo wananchi wakalizingira gari hilo na kuweka mawe na magogo na Polisi wakaitwa.

Polisi walipofika wakawakagua vijana hao na kuwakuta na pingu na silaha kadhaa na kitambulisho feki cha polisi.

Vijana watatu wamekamatwa na mmoja amefanikiwa kukimbia.
Mmoja kati ya vijana waliokamatwa ni mlinzi wa karibu wa Prof. Lipumba aitwaye HAJI "Mrangi" ambaye ni maarufu anajulikana kwa ushiriki wake wa vitendo vya kihuni na kiharamia kama hivi.

Katika mahojiano ya awali mmoja wa vijana hao ametoa ushirikiano na kueleza kuwa wametumwa na Abdul Kambaya na kuwa anayeongoza oparesheni yao hiyo ni mtu aitwaye Athumani (Mganga wa Kienyeji na Mwalimu wa mafunzo ya Kareti) aishiye Ilala akisaidiwa na watu wengine wanaojulikana Abubakar Fambo, Mohamed Ibrahim na Hassan Kingwele ( Mlinzi wa Magdalena Sakaya (MB).

Vijana hao waliokamatwa wanakiri kuwa mipango yote hiyo Prof. Lipumba anaijua kama vile walivyoongoza mpango wa kuhujumu Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF ulioahirishwa pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.

Mhe. Joran Bashange ameumizwa maeneo kadhaa ya mwili na anaendelea na matibabu na taarifa za ndani zinaonesha kuwa wahusika walielekezwa kumshambulia vibaya na kumuua ikiwa wangelifanikiwa kuondoka naye. Tukio hili linafanana na matukio kadhaa yaliyotokea huko nyuma na mfano utekwaji wa Dr. Ulimboka, Absalom Kibanda , Salma Said Kubenea na wengine.

Vijana waliohusika na utekaji huo na gari lao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Buguruni.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) kinalaani sana kitendo hicho na kinachukua hatua stahiki. Chama kinaamini kuwa kwa sasa Prof. Lipumba na watu wake wamekusudia kuendesha HUJUMA za wazi na kuvuka mipaka ya ushindani wa kisiasa za ndani ya Chama na kujivika joho la 'Uintarahamwe na Umungiki' wa wazi dhidi ya Chama na kuhatarisha na kutishia usalama wa maisha ya viongozi wa Chama.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma.
16 Septemba 2016.
Habari hii sio nzuri kwa CCM na vijana wao wa mtandaoni
 
NgugiAchebe said:
Ili naona uongo unasema walizingirwa na wananci wakajaa wakaliekea magogo mbele na nyuma police wakaitwa wakafika eneo la tukio mmoja akatoroka uongo uliokubuuu kabisa
Hugo mmoja alitoroka mbele ya umma wrote huo na

Nimekuelewa ndugu
Hoja ya msingi hiyo

Halafu eti walifanikiwa kumwingiza ndani ya gari katibu wa mpunga, akapambana halafu akapiga yowe
Inamaana hiyo gari ilikuwa imesimama tu?

Ni wengi mno waliotoroka chini ya ulinzi mkali, mfano rahisi tu ni kuwa mwaka 1982 waliokuwa watuhumiwa wakuu wa kesi ya uhaini ( marehemu Lugangira na marehemu Macghee) ya kutaka kumpindua aliyekuwa Raisi wakati huo hayati Julius Kambarage Nyerere walitoroka toka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi Tanzania - Ukonga na watuhumiwa wenyewe wakiwa na walinzi maalumu ndani ya magereza.
 
Back
Top Bottom