Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

CCM kitambi noma sipoti kilabu.
Matatizo yote yanaletwa na mkongo wa mawasiliano wa Taifa.
Ukikomenti tu wewe ni mchochezi
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kwahyo walinz wetu ni sawa kuwa na miili ya kizembezembe sababu ni wa magu sio wa putin?
Nani kakwambia ni wazembe??? Usidharau mtu kwa muonekano...dont judge a book by its cover my friend..hao watu wameiva wanajua ukujaribu utabroo...na Rais ana mambo mengi sio kila unauona hapo ni mlinzi wengine wana ditect hatari na wengine wanalinda sio kama mnavyodhani nyie
 
Kupata mafunzo haraf hufanyi mazoez ya mara Kwa mara kubaki na fitness yako haikufanyi kuwa fiti
Ni Kweli...

Ndo maana nkasema ao Walinzi wa bwana Putin wanaweza kupambana zaidi ya SAA bila kukata Punzi, kwa kua Wenye Vitambi watambana vyema tu Ila wataishiwa punzi mapema........

Kwa ujumla wake aipendezi Askari kuwa na Kitambi, Huwa nashangaa sana aka kautamaduni ka hapa nyumbani........!
 
Ulinzi wa raisi sio mchezo kama wengine wanavyochukulia hapa hao wanaoonekana ni sehemu tu, raisi anaweza kwenda sehemu watu wakajaa wewe ukachukulia wale wote waliojaa ni wa kuja tu kumbe nusu yao ni walinzi wa raisi.
 
Wa kawaida sana hao... sema tu nchi yetu haina misukosuko ya viongozi
amani imetutawala
 
Vigezo vya ulinzi wa viongozi au VIP protection huwa vinafanana na vinakuja kutofautiana kwenye Technology na protection clearance level kwa viongozi, clearance level kubwa kabisa ya kidunia ni 5 pia ulinzi wa viongozi unategemea na maeneo ambayo kiongozi yupo, threat zinazoweza kujitokeza kwa mazingira ambayo kiongozi yupo ,pia hali ya usalama wa nchi husika mfano ulinzi wa viongozi wa nchi za mashariki ya kati ni tofauti na ulinzi wa viongozi wetu mfano huku kwetu wanaobeba silaha za kuonekana kabisa ni FFU, lakini wale wavaa suti wanabeba lakini zinakuwa zimejificha lakini ukienda baadhi ya nchi wote wanabeba tena wengine mpaka machine gun

Vigezo huwa ni 6 kwa level ya kidunia hata vyuo vingi dunian vya mafunzo ya VIP protection wanafundisha lakini kuna nchi wanaviongeza mpaka 10 ila US yeye anavyo mpaka 15 na hii inatokana na uwezo wa rasilimali za nchi na Technology wao wanatumia presidential protection clearance level zote 5 kwa wakati mmoja na kumfanya rais wa US kuwa mwanadamu wenye ulinzi mkubwa duniani tofauti na viongozi wengine wanaotumia level of clearance kuanzia 2 - 4 na hii wanafanya wamarekani kutokana na rasilimali fedha na rasilimali technology waliyonayo mfano ndege ya Air force pekee kukaa angani ni $228,000 per hour to fly. na ziko ndege mbili zinafatana kila sehemu trip moja ya rais US inakadiliwa kuwa ni kati ya dola 15 - 20 milion kwa trip moja na hii inatokana na uwezo wa rasilimali za fedha na technology pia US ndo nchi pekee ambayo kiongozi wake anatembea na vifaa vyake vyote bajeti tu ya ulinzi wa rais na makamu wake kwa mwaka ni $1.4 billion.

Mtu yeyote mwenye kazi hii ni lazima kuwa fit physical & mental pia wanasema kuwa angalau uwe na elimu ya chuo na wanapendekeza kuanzia GPA ya kuanzia 3.5 na kuendelea kwani matumizi ya mwili,silaha na akili ni mkubwa sana pia husiwe na criminal background vipo vingi sana lakini kwa uchache ni hivyo

Walizi wa viongozi wanatakiwa kuwa fiti kimazoezi hasa ya kutumia silaha na matumizi wa mwili yani mikono na miguu pia wanapendekeza sana huwe na shabaha kwani wanasema huweze kuhit target ,hata kwenye kundi la watu wengi pia kila risasi inayotoka ni lazima ifanye madhara kwa adui

Pia wanasema huwe Smart thinker si great thinker . Kwani wanaitaji mahamuzi sahihi tena kwa muda mfupi kwani Smart thinker ni yule mwenye mahamuzi sahihi kwa muda mfupi kwa wakati wowote lakini great thinker unaweza kuwa na mahamuzi sahihi kwa wakati fulani anadhani yeye kuwa ni sahihi

Pia hakuna kipengere kinachosema mlinzi wa viongozi ni lazima kuwa mwembamba,mnene au wakawaida wanachotaka ni kuwa mwepesi tu na ni ukweli usiofichika kuwa watu wanamwili mkubwa lakini ni wepesi kuliko mwenye mwili mgodo pia ukakamavu haujalishi aina ya mwili aidha mwembamba au mnene
 
Mimi hao watu huwa sina mashaka nao kabisa wewe kama unataka uwajue siku moja jidai kichaa nenda ushike rais ,utaona ule msemo wa hata kazi tu
 
Maumbile hayawezi kukupa picha ya fitness ya mtu?au fitness unailewaje labda?au hujui kwamba kitambi ni dalili ya mtu asiyefanya mazoezi au asiyefanya mazoez ya kutosha?haijalishi picha imepigiwa wap muonekano unabaki palepale una kitambi una kitambi tu haijalishi umepigwa picha mjini au chato.haraf hata umri wao unaonekana kusogea pia,hawa hawapungui miaka arobaini na kitu,sasa jiulize kama umri huo bado ni umri wa kukurukakara za kiulinzi zikijitokeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…