Kwahyo unataka tuamini mtu mwenye kitambi na ambae umri wake umesogea kama hawa jamaa wetu ni wepes mno kuliko watu wasio na vitambi na wenye mazoezi?umeanza vizuri lakini umemaliza kienyeji sana Kwa mtazamo wako binafsi tu tena dhaifu ambao Haujazingatia data za kitaalam kama ulizotoa huko juu
Tofautisha mwili mkubwa na kitambi kitambi hata watu wenye mwili wa kawaida wapo wengine wana vitambi , pia unatakiwa kujua unapozungumzia ulinzi (protection) na usalama(security) unazungumzia matumizi ya AKILI,SILAHA NA MWILI
AKILI hapa ndio zinatumika zile zinazoitwa hisia 6 au "sixth sense"
Kila binadamu ana body sensitivity 3 ila wanausalama wanakwenda kusomea zingine tatu ndo inakuja kuwa 6 kwani unatakiwa kujua duniani kuna aina tatu za elimu
1 Elimu ya kidini
2 Elimu ya kidunia hii ndio tunafundishwa mashuleni
3 Elimu ya utambuzi elimu hii wanafundishwa watu wachache ambao wanakuwa trained kwa ajili ya kudeal na watu wenye elimu hzo mbili yani ya dini na kidunia
nikutajie kuanzia hisia ya 4 mpka 6 kwa ufupi
4 Ni uwezo wa kumsoma mtu kwa sura yake
kwa kumwangalia tu tutakubaliana ya kuwa sura inaongea sura inaweza elezea kila kitu kinachotokea ndani ya mwili wako mfano furaha,huzuni,shauku,hofu,jazba na kukata tamaa
5 Ni uwezo wa kumsoma mtu kupitia moyo wake hapa napenda kuwaelezea kidogo na kuwapa mfano juu ya usomaji wa moyo mtu aliyeiva ktk maswala ya ujasusi anauwezo mkubwa wa kujua ata anapomtongoza mwanamke anajua atajibu nini au anawaza nini kihisia juu yake kwan lipo somo maalumu kwa ajiri ya wanawake ktk tasinia ya ujasusi inamtambua mwanamke kama ni silaha ya maangamizi ( Weapons of Mass Distraction)
6 Ni uwezo wa kumsoma mtu ndani ya ubongo pia tunatakiwa kujua ubongo ndio command center ya mwili wa kila mwanadamu command zote zinatoka ndani ya ubongo na ukiweza kufuzu vizuri somo ili ambazo pass mark zake ni 70% utakuwa unawezo mkubwa sana wa mambo wa ujasusi
SILAHA hapa inatakiwa kujua matunizi sahihi ya silaha za aina 5 tofauti pili huwe na uwezo wa kulenga shabaha kwani kila risasi utakayo piga ni lazima uhit target , kwani kazi yako unaifanya kwenye mikusanyiko ya watu wengi kwani mara nying viongozi huwa kwenye mikusanyiko ya watu so ni lazima adui tu ndie adhibitiwe si watu wasio na hatia
MWILI hapa ndo linapokuja swala fitness ya mwili na fitness inapatikana kwa kufanya mazoezi ya ukakamavu si mazoezi ya kujaza au kupunguza mwili sasa ninaposema wepesi inatakiwa huwe mwepesi wa mwili na akili (smart thinker) na ndo maana nakwambia hakuna kipengere kinachosema mlinzi wa viongozi ni lazima huwe ni mwembamba au mwili mkubwa ila unatakiwa huwe mkakamavu na utayali wa kukabili tukio lolote kwa wakat wowote