Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

Walinzi wa rais wetu fitness yao vipi?

Kila mtu pale anakazi yake,kuna wa karibu,kuna wa mbele,nyuma na kila upande. Na wengi ni secret.Kumbe bila shaka wewe unaona aliekaribu unahukumu. Ngoma nzito hiyo mzee jaribu uone.
Mara nyingi haya ni maneno ya kuaminishwa na mnayameza na kuyaishi Bila hata kutumia critical mind,Yan hamtak kufikiri zaidi ya pale mlipoaminishwa
 
Floyd-Mayweather-Jr.jpg
 
Nani kakwambia ni wazembe??? Usidharau mtu kwa muonekano...dont judge a book by its cover my friend..hao watu wameiva wanajua ukujaribu utabroo...na Rais ana mambo mengi sio kila unauona hapo ni mlinzi wengine wana ditect hatari na wengine wanalinda sio kama mnavyodhani nyie
Mtu Ana kitambi na umri umesogea bado una Imani nae kwamba yuko fiti?ama kwel Kuna watu mna imani
 
Kwa hiyo umeleta Mada bila utafiti? Kwani si ujaribu kukatisha mbele yao kihasarahasara kisha utuletee mrejesho!
Huo ni uvivu wa kufikiri,sio lazima Kila kitu ukijaribu,nikijaribu naweza kuprove point yangu kwamba hawapo fiti lakini mwisho wa siku hayaishii hapo nitakumbana na mkono wa sheria pia
 
Ulinzi wa raisi sio mchezo kama wengine wanavyochukulia hapa hao wanaoonekana ni sehemu tu, raisi anaweza kwenda sehemu watu wakajaa wewe ukachukulia wale wote waliojaa ni wa kuja tu kumbe nusu yao ni walinzi wa raisi.
Ni kwel lakini wale wanaomzunguka ndio muhimu zaid sababu ndio wanaweza kukutana na threat wakiwa watu wa mwisho kabisa
 
Wamasai tena wametoka wap Acha ubwege wewe jadili mada husika bac wapelekee mkewo kama unaona ngombe wanafaidi

Mkuu;
Mbona tena unatoka nje ya mada?? Siasema wapelekwe wamasai. Jina tu lisikutoe ufaham mkuu. Soma tu taratiib utauona mchango wangu hapo. Siazungumzia wamasai kuwa bora nimesema; Kama mtu anatafuta wakimbiaji wawe walinzi wa rais, basi Tz kabila bora lenye mbinu ni wamasai. Sijasema walinzi wawe wamasai mkuu tafadhali sana. Tena mke wangu katokapi humu jf??
 
bodyguards sifa yao kuu ni kukubali kuutumia mwili wao kama kinga dhidi ya wanayemlinda!!anatakiwa awe tayari kufa yeye badala ya anayemlinda!!mamlaka husika zimekubali hao unaowaona wana sifa hizo stahiki!!jukumu lao sio kukimbizana na mhalifu!Binafsi Tanzania hii naweza kuhofia mambo mengine yooooooote lakini sio mambo ya ulinzi na usalama!Hapo dunia inaweza kuja kujifunza kutoka kwetu.
 
Vigezo vya ulinzi wa viongozi au VIP protection huwa vinafanana na vinakuja kutofautiana kwenye Technology na protection clearance level kwa viongozi, clearance level kubwa kabisa ya kidunia ni 5 pia ulinzi wa viongozi unategemea na maeneo ambayo kiongozi yupo, threat zinazoweza kujitokeza kwa mazingira ambayo kiongozi yupo ,pia hali ya usalama wa nchi husika mfano ulinzi wa viongozi wa nchi za mashariki ya kati ni tofauti na ulinzi wa viongozi wetu mfano huku kwetu wanaobeba silaha za kuonekana kabisa ni FFU, lakini wale wavaa suti wanabeba lakini zinakuwa zimejificha lakini ukienda baadhi ya nchi wote wanabeba tena wengine mpaka machine gun

Vigezo huwa ni 6 kwa level ya kidunia hata vyuo vingi dunian vya mafunzo ya VIP protection wanafundisha lakini kuna nchi wanaviongeza mpaka 10 ila US yeye anavyo mpaka 15 na hii inatokana na uwezo wa rasilimali za nchi na Technology wao wanatumia presidential protection clearance level zote 5 kwa wakati mmoja na kumfanya rais wa US kuwa mwanadamu wenye ulinzi mkubwa duniani tofauti na viongozi wengine wanaotumia level of clearance kuanzia 2 - 4 na hii wanafanya wamarekani kutokana na rasilimali fedha na rasilimali technology waliyonayo mfano ndege ya Air force pekee kukaa angani ni $228,000 per hour to fly. na ziko ndege mbili zinafatana kila sehemu trip moja ya rais US inakadiliwa kuwa ni kati ya dola 15 - 20 milion kwa trip moja na hii inatokana na uwezo wa rasilimali za fedha na technology pia US ndo nchi pekee ambayo kiongozi wake anatembea na vifaa vyake vyote bajeti tu ya ulinzi wa rais na makamu wake kwa mwaka ni $1.4 billion.

Mtu yeyote mwenye kazi hii ni lazima kuwa fit physical & mental pia wanasema kuwa angalau uwe na elimu ya chuo na wanapendekeza kuanzia GPA ya kuanzia 3.5 na kuendelea kwani matumizi ya mwili,silaha na akili ni mkubwa sana pia husiwe na criminal background vipo vingi sana lakini kwa uchache ni hivyo

Walizi wa viongozi wanatakiwa kuwa fiti kimazoezi hasa ya kutumia silaha na matumizi wa mwili yani mikono na miguu pia wanapendekeza sana huwe na shabaha kwani wanasema huweze kuhit target ,hata kwenye kundi la watu wengi pia kila risasi inayotoka ni lazima ifanye madhara kwa adui

Pia wanasema huwe Smart thinker si great thinker . Kwani wanaitaji mahamuzi sahihi tena kwa muda mfupi kwani Smart thinker ni yule mwenye mahamuzi sahihi kwa muda mfupi kwa wakati wowote lakini great thinker unaweza kuwa na mahamuzi sahihi kwa wakati fulani anadhani yeye kuwa ni sahihi

Pia hakuna kipengere kinachosema mlinzi wa viongozi ni lazima kuwa mwembamba,mnene au wakawaida wanachotaka ni kuwa mwepesi tu na ni ukweli usiofichika kuwa watu wanamwili mkubwa lakini ni wepesi kuliko mwenye mwili mgodo pia ukakamavu haujalishi aina ya mwili aidha mwembamba au mnene
Kwahyo unataka tuamini mtu mwenye kitambi na ambae umri wake umesogea kama hawa jamaa wetu ni wepes mno kuliko watu wasio na vitambi na wenye mazoezi?umeanza vizuri lakini umemaliza kienyeji sana Kwa mtazamo wako binafsi tu tena dhaifu ambao Haujazingatia data za kitaalam kama ulizotoa huko juu
 
Probably kitambi sio issue. Yule Comandoo wa JWTZ mmemsahau?!😀
Yule ni mtoa show tu kaka na mkufunzi,hatumwi kwenye majukumu ya Ana Kwa Ana ktk uwanja wa mapambano,umri wake umeenda na amezembea kujiweka fiti mpaka amefuga tumbo
 
Huo ni uvivu wa kufikiri,sio lazima Kila kitu ukijaribu,nikijaribu naweza kuprove point yangu kwamba hawapo fiti lakini mwisho wa siku hayaishii hapo nitakumbana na mkono wa sheria pia
Mimi mvivu wa kufikiri! Uko sahihi kwa uelewa wako na ndo maana umeleta wazo ambalo umeshalipangia jibu.

Kwamba wewe ni kapuku katika masuala ya ULINZI halafu unahoji uwezo wa watu waliozurura duniani kwa miaka yote ya maisha yao wakisomea masuala hayo halafu unaona wewe ni mwerevu wa kufikiri.

Kwamba mada yako imeelemea upande wa vurugu, eti asiye na kitambi ndiyo mlinzi mahiri wa mkulu kama kwamba ulinzi pekee wa Rais ni wa mapigano ya kimasai na wasonjo

Kwamba umetoa picha nyingi za mkulu ukionyesha unachodhani kwa uelewa wako wa kushabikia siasa ndo ulinzi wa mkulu bila kujua mazingira ya ulinzi wenyewe halafu unaona una uelevu wa kufikiri!

ASALALLEH!
 
Tatzo nitakuwa nimeijaribu na sheria pia
Sasa unataka kujua utamu wa asali bila kuonja wewe nenda chezea mzinga utawaona wenye mzinga (hapo sina wasiwasi hata akitembea kwa miguu toka dsm hadi tabora atakuwa salama kuliko unavyodhani)
 
bodyguards sifa yao kuu ni kukubali kuutumia mwili wao kama kinga dhidi ya wanayemlinda!!anatakiwa awe tayari kufa yeye badala ya anayemlinda!!mamlaka husika zimekubali hao unaowaona wana sifa hizo stahiki!!jukumu lao sio kukimbizana na mhalifu!Binafsi Tanzania hii naweza kuhofia mambo mengine yooooooote lakini sio mambo ya ulinzi na usalama!Hapo dunia inaweza kuja kujifunza kutoka kwetu.
Tunaishi Kwa mazoea na Imani ndani ya nchi hii,mara nyingi wadadisi wanaoenda mbali zaid ya Iman ya mazoea ndio hugundua mambo na kufichua uozo ktk mambo mengi,ulinzi ule unajumuisha mengi sio kujiwka kupigwa risasi tu
 
Mimi mvivu wa kufikiri! Uko sahihi kwa uelewa wako na ndo maana umeleta wazo ambalo umeshalipangia jibu.

Kwamba wewe ni kapuku katika masuala ya ULINZI halafu unahoji uwezo wa watu waliozurura duniani kwa miaka yote ya maisha yao wakisomea masuala hayo halafu unaona wewe ni mwerevu wa kufikiri.

Kwamba mada yako imeelemea upande wa vurugu, eti asiye na kitambi ndiyo mlinzi mahiri wa mkulu kama kwamba ulinzi pekee wa Rais ni wa mapigano ya kimasai na wasonjo

Kwamba umetoa picha nyingi za mkulu ukionyesha unachodhani kwa uelewa wako wa kushabikia siasa ndo ulinzi wa mkulu bila kujua mazingira ya ulinzi wenyewe halafu unaona una uelevu wa kufikiri!

ASALALLEH!
Uvivu wako wa kufikiri nimeugundua kutokana na Aina ya jibu ulilotoa ambalo halikuchangia chochote zaid ya kusema eti nikawajaribu,ina maana hukufikiri kwamba nikiwajaribu nitakuwa nimeijaribu na sheria pia?Kuna watu kwl wanachangia vizur Kwa kuweka data na uzoefu mbalimbali lakini wavivu wanaishia kusema kawajaribu
 
Back
Top Bottom