Walio Tuambia Shule Ni Ufunguo Wa Maisha Wametupiga

Walio Tuambia Shule Ni Ufunguo Wa Maisha Wametupiga

Elimu ya darasani sio elimu ya mtaani, darasani theory mtaani field.
Aliyesomea market hawezi kumshinda machinga mbinu za kuuza
Ni sahihi kabisa ndio maana hata waajili wanataka watu wenye uzoefu

Hata injinia aliyetoka darasani pamoja na usomi wake kuna mambo kwa ground atamhitaji mwenye uzoefu site
 
Hatusomi ili tuajiriwe bali tuelimike ndo kitu ambacho waafrika wengi hawajui
Mtu yeyote aliyesoma na kuelimika haswa kamwe huwezi mkuta analalamika maswala ya ajira sababu maarifa atakua nayo

Waengine wanasoma ili wapate vyeti hawa ndo kama mleta uzi,
Sijajua nani alitudanganya watanzania kua lengo la Elimu kufanya watu wapate ajira wakihitimu masomo..
 
Sijajua nani alitudanganya watanzania kua lengo la Elimu kufanya watu wapate ajira wakihitimu masomo..
Mt anaituhumu elimu ilihali mda huo huo simu anayotumia, dawa aliyotoka kunywa mda sio mrefu ni matokeo ya research za miaka mingi sana unajua wafrika tunashida sana ya kifikra kubwa mno

Haiwezekani elimu hii hii iwasaidie watu wengine wengi alafu sisi ishindwe ukweli ni kwamba shida ipo kwetu na sio kwenye elimu
 
Kwa Taarifa Tulio nayo mpaka sasa
1. Tajiri no. Moja Duniani Ako na Masters
2. Tajiri no. Moja Tanzania ana Masters.

Kazi kwako, Upite njia ya Wasomi au Ya wasio wasomi akina Mondi Muhimu tukutane sheli tujaze mafuta
 
Back
Top Bottom