Waliochelewa kuripoti JKT wakataliwa kupokelewa

Wameshajenga cv tayari,uko mbeleni akiulizwa kama alifika jkt,jibu ni ndio.cheti karatasi tu
 
Wame kataliwa kwa mjibu wa sheria ipi? Wstanzania hatuko serious kabisa kuchelewa siku moja sio kubwa kiasi hicho.
Kijeshi kuchelewa dakika moja ni dhambi isiyosameheka.

Pia tujifunze kuzingatia muda. Binafsi nawapongeza kwa hatua waliyochukua ili kuwa funzo kwa wengine.
 
Kwani hao walio chelewa walikua wanajeshi tayari?
 
Wahitimu wa kidato cha sita waliochelewa kuripoti kambini tarehe 11/6/2023 wamezuiwa kuripoti na kuungana na wenzao. Zaidi ya vijana 150 katika kambi ya JKT Mafinga wamerejeshwa wakati wakiripoti jana 12/6/2023 siku moja baada ya tarehe ya mwisho.

Kwa wale waliofika jana jioni walipewa hifadhi mpaka asubuhi kwaajili ya usalama wao na leo asubuhi wametakiwa kurejea kwao. Nidhamu ya jeshi ni msingi wa jeshi imara! walidhani ni kule sekondari mtu anavuta wiki mbili mbele baada ya shule kufunguliwa.

Wazazi kama mwanao alienda JKT tarehe 12/6 wasiliana naye ama mtumie nauli yupo nje anapunga upepo!
Kwani walikuwa wamefuata ajira Jeshini?
Kwenda kufanya kazi Za bure !
Warudi tu
 
Wame kataliwa kwa mjibu wa sheria ipi? Wstanzania hatuko serious kabisa kuchelewa siku moja sio kubwa kiasi hicho.
Nadhani Uongozi wa Jeshi katika kila Kambi unapaswa kumhoji kila mtu mmoja mmoja juu ya sababu zilizofanya Mwanafunzi kuchelewa kuripoti kambini katika muda uliopangwa kuliko kuwarudisha nyumbani wote pamoja kwa ujumla.
Yawezekana kabisa wapo baadhi ya Wanafunzi wenye sababu za msingi kabisa (reasonable and genuine reasons) zilizowakwamisha wasiripoti kambini kwa wakati muafaka.
Huu ni mtazamo wangu, I stand to be corrected or to be criticised.
Kuhoji ili udanganywe?
 
Yaani ingekuwa mie ndio nafika naambiwa umechelewa rudi nyumbani!! Weeeeh nisingesubiri hata amalizie sentensi, ningetimka kama mwizi niwaache na upuuzi wao.
 
Wahitimu wa kidato cha sita waliochelewa kuripoti kambini tarehe 11/6/2023 wamezuiwa kuripoti na kuungana na wenzao. Zaidi ya vijana 150 katika kambi ya JKT Mafinga wamerejeshwa wakati wakiripoti jana 12/6/2023 siku moja baada ya tarehe ya mwisho.

Kwa wale waliofika jana jioni walipewa hifadhi mpaka asubuhi kwaajili ya usalama wao na leo asubuhi wametakiwa kurejea kwao. Nidhamu ya jeshi ni msingi wa jeshi imara! walidhani ni kule sekondari mtu anavuta wiki mbili mbele baada ya shule kufunguliwa.

Wazazi kama mwanao alienda JKT tarehe 12/6 wasiliana naye ama mtumie nauli yupo nje anapunga upepo!
Mbona huku kwetu Tanga wanazidi kuriport?
 
Warudi mtaani kuendelea kuchakata/kuchakatwa.....!
Maisha sio lazima JKT.
 
Kuhoji ili udanganywe?
Penye ukweli uongo hujitenga na Njia ya muongo ni fupi.
Huwezi kuacha kuhoji eti kisa unaogopa usidanganywe, siyo kweli hata kidogo na wala si kutenda haki kwa wahusika.

Watu wakataliwe kujiunga na Jeshi endapo kama zipo sababu za msingi zinazofanya mtu huyo kukataliwa. Kusiwepo na hila, ghilba, ukiritimba au dhulma katika kuwakataa watu wanaotaka kujiunga na Jeshi, Haki Itendeke kwa Wahusika.
 
Wame kataliwa kwa mjibu wa sheria ipi? Wstanzania hatuko serious kabisa kuchelewa siku moja sio kubwa kiasi hicho.
Kuchelewa hata dakika moja ni kubwa sana. Badilikeni watanzania
 
Wahitimu wa kidato cha sita waliochelewa kuripoti kambini tarehe 11/6/2023 wamezuiwa kuripoti na kuungana na wenzao. Zaidi ya vijana 150 katika kambi ya JKT Mafinga wamerejeshwa wakati wakiripoti jana 12/6/2023 siku moja baada ya tarehe ya mwisho.

Kwa wale waliofika jana jioni walipewa hifadhi mpaka asubuhi kwaajili ya usalama wao na leo asubuhi wametakiwa kurejea kwao. Nidhamu ya jeshi ni msingi wa jeshi imara! walidhani ni kule sekondari mtu anavuta wiki mbili mbele baada ya shule kufunguliwa.

Wazazi kama mwanao alienda JKT tarehe 12/6 wasiliana naye ama mtumie nauli yupo nje anapunga upepo!
Hivi wanapewa nauli tuanzie hapo ili twende sawa usilaume bila kujua chanzo
 
Back
Top Bottom