PreGE2025 Waliodukua ukurasa wa Polisi X (Twitter), wadukua ukurasa wa CCM, Airtel, Simba SC, TRA, EWURA na zingine

PreGE2025 Waliodukua ukurasa wa Polisi X (Twitter), wadukua ukurasa wa CCM, Airtel, Simba SC, TRA, EWURA na zingine

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika tukio la kushangaza na kusikitisha, kurasa mbalimbali maarufu mtandaoni zimelengwa na wadukuzi wasiojulikana walioteka akaunti rasmi ya Polisi Tanzania kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ukurasa wa Airtel Tanzania kwenye X, akaunti ya YouTube ya klabu ya Simba SC, ukurasa wa X wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (YouTube), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) pamona na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zote YouTube.

Katika hujuma hizo, taarifa ya uongo kuhusu kifo cha Rais Samia, imesambazwa na wahalifu hao wa kimtandao.

Jeshi la Polisi wamsaka aliyesambaza taarifa za upotoshaji katika ukurasa wao wa X (Twitter)

Pia, Soma

Ni rahisi Sana kudukua Server za mitandao ya mawasiliano ya kidijiti Tanzania
 
Acha , wanadownload security softwares kwa matumizi ya kitaifaa??🫣🫣🫣
Kwani natania??hukuona makao makuu ya polisi email address wanatumia gmail?? Sio kwamba wajuzi hawapo ila nafasi wanapewa kwa kujuana,utakuta mkuu wa kitengo ana masters ya computer science na physics kasoma marekani ila kukiwa na tatizo la network wanatafuta wahuni wa mtaani,..wanachofikiri serikali IT ni vyeti,..waige wenzetu wanavyotoa ajira..
 
Katika tukio la kushangaza na kusikitisha, kurasa mbalimbali maarufu mtandaoni zimelengwa na wadukuzi wasiojulikana walioteka akaunti rasmi ya Polisi Tanzania kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ukurasa wa Airtel Tanzania kwenye X, akaunti ya YouTube ya klabu ya Simba SC, ukurasa wa X wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (YouTube), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chama cha Mapinduzi (CCM) pamona na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zote YouTube.

Katika hujuma hizo, taarifa ya uongo kuhusu kifo cha Rais Samia, imesambazwa na wahalifu hao wa kimtandao.

Jeshi la Polisi wamsaka aliyesambaza taarifa za upotoshaji katika ukurasa wao wa X (Twitter)

Pia, Soma
Hatari sana, possibly, Hawa washenzi wapo nchi jirani!, inaogopesha sana wanaweza hark account ya Mtu asiye na hatia wala hajui lolote, waka kufitinisha na vyombo vya dola, ukapata matatizo ya BURE, very sad.
 
Imeshatokea sana tu, multiple people wameshakuwa havked and if you dont know unaweza lipia service, wana hack na kuchukua taarifa za mtu unaetaka yoyote
 
Huo ni uongo, hakuna aliyedukuwa popote.

Hawa polisi huwa wanajikana hata wao wenyewe na bado wako sahihi, kipi kikufanye leo uwe na imani wanadukuliwa?

Hakuna kilicho sawa nchi hii, utasema na sisi tumedukuliwa?

Nyie ndio mnaamini hakuna watu wanatekwa, kuvunjwa miguu na kuuwawa, mnasema mmedukuliwa na nani?

Mambo yenu mnayakana wenyewe.
 
Inabidi tukubali kama nchi tumevuliwa nguo.

Wakati wenzetu wanainvest kwenye kutengeneza technocrats sisi tumejaza watu wasio na weledi na sifa kwenye mifumo na taasisi za umma.

Kwa kinachoendelea muda huu kwenye socio-media, inawezekana ikawa ndo the largest cybersecurity attack kuwahi kutokea Tanzania.
 
Back
Top Bottom