Waliofariki ajali Morogoro wapo Wanandoa

Mkuu hapo maslahi makubwa lazima yaangaliwe. Kupoteza familia na baba na mama kwa wakati mmoja ni hatari sana
So ukiwa na family car watu wasipande pamoja..kila mtu awe na gari lake. Ajali ni ajali yaweza tokea popote..Kuna nyumba Huwa zinaungua wanafamilia wote wanateketea so tutunge na sheria ya wanafamilia kutokuishi nyumba Moja?
 
Tatizo polisi wakigundua wewe ndo umekosea ata kama ulichomekewa watakuambia wewe ndo unamakosa..wakikuta chupa za bia ndani ya gari watasema dereva alikuwa mlevi ata kama ulikuwa hujanywa..inawezekana kweli jamaa alikuwa na makosa but ukiwa dereva mzuri na makini unaweza rekebisha makosa ya dereva mwenzako Ili wote mfike salama..
 
Hiyo gari ndogo siyo IT, ina namba T695DNN ingawa IT kupakia abiria ndio zao japo hawaruhusiwi..High speed kills! Dereva kawaponza wenzie kwa misifa
Ubishi ni jadi yetu, endeleeni na ligi na RPC wenu mpaka mshindi apatikane
 
Ajali kama hizi zitaendelea hadi kutakapokuwa na sheria moja kwa magari yote barabarani.
 
So ukiwa na family car watu wasipande pamoja..kila mtu awe na gari lake. Ajali ni ajali yaweza tokea popote..Kuna nyumba Huwa zinaungua wanafamilia wote wanateketea so tutunge na sheria ya wanafamilia kutokuishi nyumba Moja?
You missed the whole point. Na mfano uliotoa ni wa kipuuzi sana. Mimi nazungumzia ajali za barabarani ambazo ni nyingi familia nyingi zimepoteza Baba na mama kwa pamoja kwenye ajali. Sio kila mtu ni kichwa ngumu wafata sheria wapo. Ipigwe marufuku baba na mama kusafiri pamoja.
Nikikupa takwimu za miaka mitatu iliyopita unaweza ukaelewa ninachosema. Na kuacha kuandika hovyo kama muuza bangi
 
Hiyo gari ndogo siyo IT, ina namba T695DNN ingawa IT kupakia abiria ndio zao japo hawaruhusiwi..High speed kills! Dereva kawaponza wenzie kwa misifa
Umeacha namba moja hapo, 4 kabla ya DNN, IT6654DNN. Hapo utaelewa kuwa sio gari local kwa kuwa local zina tarakimu 3 tu, hiyo DNN kaweka kama mbwembwe tu
 
Kwahyo mkuu hivi hapo nani atalipa fidia ya hiyo gari
 
Unaongelea kusafiri kwako wewe unamaanisha Nini? Ajali inaweza tokea popote mkuu...unaweza toka kimara kwenda Ubungo pia ukapata ajali..sasa kuzuia familia zisikae kwenye usafiri mmoja ni wazo ambalo halina mashiko kutokana na ugumu wake katika utekelezaji...Kuna watu wanaishi maeneo ambayo barabara zinapita nao utawazuia wasipande chombo kimoja Cha usafiri..coz na wao pia wapo kwenye risk kubwa ya kupata ajali...wanaweza pata hizo ajali kutokana na highway kupita maeneo Yao..mfano watu wanaoishi pembezoni kwa morogoro road..
Pia Kuna maeneo yanachangamoto ya usafiri gari Moja asubuhi gari Moja jioni..sasa hapo utazuiaje marufuku wanafamilia kupanda Hilo gari Moja...haya Kuna wengine wanasindikiza wagonjwa, misiba au wanashughuli za kifamilia sasa utawambiaje ni marufuku kusafiri pamoja..kinachotakiwa hapo ni kuboresha miundombinu..Hilo eneo linasifika kwa ajali za mara kwa mara kutokana na ufinyu wa barabara na si kwa kuwa familia zinapanda usafiri mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…