Waliofariki ajali Morogoro wapo Wanandoa

Waliofariki ajali Morogoro wapo Wanandoa

Mkuu hapo maslahi makubwa lazima yaangaliwe. Kupoteza familia na baba na mama kwa wakati mmoja ni hatari sana
So ukiwa na family car watu wasipande pamoja..kila mtu awe na gari lake. Ajali ni ajali yaweza tokea popote..Kuna nyumba Huwa zinaungua wanafamilia wote wanateketea so tutunge na sheria ya wanafamilia kutokuishi nyumba Moja?
 
Taarifa ya polisi inasemaje kuhusu chanzo cha ajali?

Ni barabara finyu?
Ni ubovu wa gari?
Ni dereva kukosa uzoefu?
Ni alama za barabarani hazionekani au hazipo?
Ni ukosefu wa huduma za uokoaji?

Ifike mahali tukubali uzembe wetu ni mkubwa tunapotumia barabara hasa tunapojifanya tuna haraka.
Tatizo polisi wakigundua wewe ndo umekosea ata kama ulichomekewa watakuambia wewe ndo unamakosa..wakikuta chupa za bia ndani ya gari watasema dereva alikuwa mlevi ata kama ulikuwa hujanywa..inawezekana kweli jamaa alikuwa na makosa but ukiwa dereva mzuri na makini unaweza rekebisha makosa ya dereva mwenzako Ili wote mfike salama..
 
Hiyo gari kama naona vifaa vimeibwa mfano taa nk,yani zimefunguliwa, hazijapasuka
1672191447975.png
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro , Fortunatus Musilimu alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa Desemba 26,2022, eneo la Iyovi, Kata na Mikumi, wilayani Kilosa, ikihusisha gari ndogo aina ya Toyota Allion yenye namba IT 6954DNN, iliyogongana uso kwa uso na kwa uso na gari kubwa la mafuta aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili RAE 518C yenye tela namba RL 2686.
Hiyo gari ndogo siyo IT, ina namba T695DNN ingawa IT kupakia abiria ndio zao japo hawaruhusiwi..High speed kills! Dereva kawaponza wenzie kwa misifa
Ubishi ni jadi yetu, endeleeni na ligi na RPC wenu mpaka mshindi apatikane
 
Ajali-new246d6a2c4c26-1-780x470.jpg
Watu watano waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Morogoro wametambuliwa wakiwemo mume na mke, ambao pia ni wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro , Fortunatus Musilimu alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa Desemba 26,2022, eneo la Iyovi, Kata na Mikumi, wilayani Kilosa, ikihusisha gari ndogo aina ya Toyota Allion yenye namba IT 6954DNN, iliyogongana uso kwa uso na kwa uso na gari kubwa la mafuta aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili RAE 518C yenye tela namba RL 2686.

Amesema gari ndogo iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Tunduma, ilikuwa ikiendeshwa na Festo Eliuzima Shoo na gari kubwa lililokuwa likitokea Iringa kuelekea Morogoro lilikuwa likiendeshwa na Muthoni Richard raia wa Rwanda.

Musilimu alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo, kutaka kuyapita magari mengine bila tahadhari, ndipo wakakutana uso kwa uso, ambapo dereva huyo wa gari ndogo ni miongoni mwa waliofariki.

Wengine ni Grayson Ng’obo mkazi wa Mbeya na Janeth John Luvanda (40), ambao kwa mujibu wa Kamanda huyo taarifa walizopata Grayson na Janeth ni mume na mke.

Aliwataja wengine waliofariki dunia ni Oswald John Luvanda (42) mkulima na mkazi wa Mbeya, ambaye ni ndugu wa Janeth Luvanda na John Davis Haule (37) Mwalimu wa shule ya Wanging’ombe iliyopo mkoani Mbeya.

Katika hatua nyingine uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kanda ya ya Mbeya umetoaa taarifa kuwa Grayson Ngogo na Janeth Luvanda waliofariki kwenye ajali hiyo ni wanafunzi wa chuo chao.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa wanafunzi hao walifariki kwenye ajali iliyotokea mkoani Morogoro na kuwa taratibu nyingine zitaendelea kutolewa.
Ajali kama hizi zitaendelea hadi kutakapokuwa na sheria moja kwa magari yote barabarani.
 
So ukiwa na family car watu wasipande pamoja..kila mtu awe na gari lake. Ajali ni ajali yaweza tokea popote..Kuna nyumba Huwa zinaungua wanafamilia wote wanateketea so tutunge na sheria ya wanafamilia kutokuishi nyumba Moja?
You missed the whole point. Na mfano uliotoa ni wa kipuuzi sana. Mimi nazungumzia ajali za barabarani ambazo ni nyingi familia nyingi zimepoteza Baba na mama kwa pamoja kwenye ajali. Sio kila mtu ni kichwa ngumu wafata sheria wapo. Ipigwe marufuku baba na mama kusafiri pamoja.
Nikikupa takwimu za miaka mitatu iliyopita unaweza ukaelewa ninachosema. Na kuacha kuandika hovyo kama muuza bangi
 
Hiyo gari ndogo siyo IT, ina namba T695DNN ingawa IT kupakia abiria ndio zao japo hawaruhusiwi..High speed kills! Dereva kawaponza wenzie kwa misifa
Umeacha namba moja hapo, 4 kabla ya DNN, IT6654DNN. Hapo utaelewa kuwa sio gari local kwa kuwa local zina tarakimu 3 tu, hiyo DNN kaweka kama mbwembwe tu
 
Hii ajali style yake ndio ile ile jamaa anafukuza gari ya mbele yake ili aikate ile ameifikia kuikata tu akawa kwenye blindspot mbele kona kali anaimaliza kona tu semi hii hapa kujiokoa akakimbilia ubavuni kwenye ngema ya mlima huo unaonekana maana upande wake kushoto kuna korongo angeitupa gari mtoni kwenye majabali.

Ukiangalia Utaona gari imebonyezwa zaidi upande wa abiria manaake [emoji597] ilianza na abiria wa koshoto kisha ikamalizana na dereva ilivyojibamiza ukingoni mwa mlima.

Hio ajali sio uso kwa uso bali ni uso kwa kiuno cha semi. Mwenye tanker alitanua ila haikumsaidia mwenye IT maana kajibamiza kwenye ngao kisha ubavuni kwenye matairi ya lorry.
Kwahyo mkuu hivi hapo nani atalipa fidia ya hiyo gari
 
You missed the whole point. Na mfano uliotoa ni wa kipuuzi sana. Mimi nazungumzia ajali za barabarani ambazo ni nyingi familia nyingi zimepoteza Baba na mama kwa pamoja kwenye ajali. Sio kila mtu ni kichwa ngumu wafata sheria wapo. Ipigwe marufuku baba na mama kusafiri pamoja.
Nikikupa takwimu za miaka mitatu iliyopita unaweza ukaelewa ninachosema. Na kuacha kuandika hovyo kama muuza bangi
Unaongelea kusafiri kwako wewe unamaanisha Nini? Ajali inaweza tokea popote mkuu...unaweza toka kimara kwenda Ubungo pia ukapata ajali..sasa kuzuia familia zisikae kwenye usafiri mmoja ni wazo ambalo halina mashiko kutokana na ugumu wake katika utekelezaji...Kuna watu wanaishi maeneo ambayo barabara zinapita nao utawazuia wasipande chombo kimoja Cha usafiri..coz na wao pia wapo kwenye risk kubwa ya kupata ajali...wanaweza pata hizo ajali kutokana na highway kupita maeneo Yao..mfano watu wanaoishi pembezoni kwa morogoro road..
Pia Kuna maeneo yanachangamoto ya usafiri gari Moja asubuhi gari Moja jioni..sasa hapo utazuiaje marufuku wanafamilia kupanda Hilo gari Moja...haya Kuna wengine wanasindikiza wagonjwa, misiba au wanashughuli za kifamilia sasa utawambiaje ni marufuku kusafiri pamoja..kinachotakiwa hapo ni kuboresha miundombinu..Hilo eneo linasifika kwa ajali za mara kwa mara kutokana na ufinyu wa barabara na si kwa kuwa familia zinapanda usafiri mmoja.
 
Back
Top Bottom