Waliofariki ajali Morogoro wapo Wanandoa

Waliofariki ajali Morogoro wapo Wanandoa

iyovi nilipoteza ndugu yangu mwaka 2018,gari yao iligongana na rungwe express ya mbeya. kuna msamalia mwema alitupigia simu wana familia kutuma taarifa kuwa amehifadhiwa hospitali ya kizito
 
Yale makona kukimbia sana na overtake sio salama hata kdg, miaka mingi toka primary nimesoma Iringa zile Kona sijawahi kua na amani tukipita....yan mpk utokeze ruaha darajani kule ndo unapata afadhali.na pale wanakimbia sn sababu pia hakuna askari wala tochi, ni pori kwa pori.
 
Hizo IT haziruhusiwi kupakia abiria. Ila watu kujidai Wana haraka haya ndio matokeo yake.
Mzee shida ni ile ile kubeti kwenye blindspots, overtakes za kwenye kona hizo. Subira ya dakika 5 ingeweza kuokoa maisha yao ila bwana Festo Shoo alitaka kuleta ujuaji na haraka isio na maana. He cost all passengers lives including himself.
 
December mwaka jana nilipoteza brother wangu katika ajali kama hiyo ya IT mkoani Iringa.

Toka hapo sijawahi shauri mtu kutumia usafiri huo maana si salama japo ni wa haraka.

Pole ziwafikie wafiwa wote.
Pole sana mkuu, hilo eneo halitaki ujuaji. Ni baya sana kama utakosa subira maana madereva wengi wako rough. Unaweza ukawa unachukua tahadhari ila wenzio wanavunja miiko ya udereva. Sema inasaidia kama utakua makini. Blindspots za Iyovi ni mbaya sana kwa ishu ya vicheche na stupid overtakes, mwendo wangu huwa ni 70-80kph mule for easy maneuvers and braking, overtake ukipata mnyooko.
 
Inaonekana alikuwa speed
Hii ajali style yake ndio ile ile jamaa anafukuza gari ya mbele yake ili aikate ile ameifikia kuikata tu akawa kwenye blindspot mbele kona kali anaimaliza kona tu semi hii hapa kujiokoa akakimbilia ubavuni kwenye ngema ya mlima huo unaonekana maana upande wake kushoto kuna korongo angeitupa gari mtoni kwenye majabali.

Ukiangalia Utaona gari imebonyezwa zaidi upande wa abiria manaake 🚛 ilianza na abiria wa koshoto kisha ikamalizana na dereva ilivyojibamiza ukingoni mwa mlima.

Hio ajali sio uso kwa uso bali ni uso kwa kiuno cha semi. Mwenye tanker alitanua ila haikumsaidia mwenye IT maana kajibamiza kwenye ngao kisha ubavuni kwenye matairi ya lorry.
 
Back
Top Bottom