Tetesi: Waliofukuzwa uanachama CHADEMA waanza kugawanyika

Tetesi: Waliofukuzwa uanachama CHADEMA waanza kugawanyika

Respect decision zake mkuu,amebambikiwa kesi sijui amefanyaje ..hili ni swala personal yeye ndio anajua kwa nini despite everything bado akaona huo ndio upande anaoutaka...nakuomba u RESPECT hizo decisions kama ambavyo ningependa wewe au wengine waheshimu CHOICES you made in life.....

Halima ndio alichagua hio kazi,na alijua consequences zake..but challenges alizopitia ni nyingi na bado akazimudu kwa miaka 15!?! Jiulize wewe ndani ya miaka 15 umebadilisha kazi ngapi?? je kazi yako ingekua na challenges za mpaka kulala selo,ungeweza kudumu nayo?? be FAIR huyu ni JASIRI..........
Kuna mtu hapo juu amehoji kama account yako iko hacked or something?

Kwa majibu haya unayotoa, naomba niishie hapa kujadiliana nawe kwenye jambo hili.
 
Chadema akili kubwa, hata walioapishwa wana bow down to Chadema. Jana NEC ya CCM ilikaa kikao kujadili maamuzi ya Chadema.

Inawahusu nn sasa.wakati wanaiba ushindi wa kishindo awakufikiria umuhimu wa kubakisha upinzani wachache angalau wangewacha wabunge wapya na wasio wataka kina mbowe,Sugu,lema ndio wangewaondoa.
Aibu Sana kimataifa Hadi vyombo vyote vinajiingiza kufanya utoto na madudu Hadi fojali za sahihi ya katibu.
Du vyeti feki, kura feki, wabunge feki, mitano feki.
 
Kuna mtu hapo juu amehoji kama account yako iko hacked or something?

Kwa majibu haya unayotoa, naomba niishie hapa kujadiliana nawe kwenye jambo hili.

mkuu?? sema nimekukwaza wapi??
 
Inawahusu nn sasa.wakati wanaiba ushindi wa kishindo awakufikiria umuhimu wa kubakisha upinzani wachache angalau wangewacha wabunge wapya na wasio wataka kina mbowe,Sugu,lema ndio wangewaondoa.
Aibu Sana kimataifa Hadi vyombo vyote vinajiingiza kufanya utoto na madudu Hadi fojali za sahihi ya katibu.
Du vyeti feki, kura feki, wabunge feki, mitano feki.
Kwa kifupi Chadema ndiyo wanaendesha nchi na wafadhili wanawaelewa sana maana wamekataa kuitambua hii serikali.
 
Nani halali ucngizi wewe ccm huku unafuata nini
WAACHENIII MAKAMANDA WALE, WAKO WANAANDAA NONDO ZA KUWACHAPA NA UTAPELI WENU KWENYE KIGENGE CHENUU. SASA NAONA MUNAWEWESEKA BILA USINGIZIIII. MUMEWATIMUA KIKATILI WAMAMA HAO HATA BILA KUWASIKILIZA HUKU MKIWATISHIA VYA KUTOSHA MKIONGOZWA NA YULE TAPELI WAUBERIGIJI. SASA TULIENIII WAWAPE ZA USO MDA SI MREFU
 
Team Mdee wasimamie walichoamua kukisimamia. There’s no turning back; wasije wakageuka mawe bure!

Chama kiliingia completely kwenye catch-22 situation. A political loss was imminent, no matter how the party chose to respond. Tukisema Upinzani hawajakomaa kwenye hii sanaa ya siasa, wanaanza kuturushia matusi kama kawaida yao!
Sawa ni kweli hawajakomaa kwenye siasa lakini ndio muwaibie kura??
 
Unadai upinzan hawajakomaa halafu serikali yako inakodi mpaka majeshi toka ya burundi kupambana nao??., kwa vyovyote wewe ni mwehu pia ww n crazy.

Sikushangai; matusi na lugha isiyo ya staha ndiyo primary capital ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia ya Matusi (Chadema).

Tanzania inafahamika na kila international community kuwa ndiyo yenye uwezo wa kutoa msaada wa kijeshi pale palipo na uhitaji huo. Kufikiria kwamba Tanzania inaweza kukodi jeshi kutoka Burundi ni uvivu wa kufikiria!
 
SIMUMEWATIMUA KWA MBWEMBWE NA JAZBA NA FEDHURI, BILA KUWASIKILIZA, SASA MBONA MUNAWEWESEKA TENA? MBONA HAMULALI USINGIZI JUU YAO?

Waliitwa na kamati walipewa nafasi ya kusikilizwa wakagoma kuja Sasa hapo lawama kwa nani. Maana kwa waungwana baada ya dili kuvurugika ilitakiwa waitikie wito waandike barua na kuomba msamaha wangesamehewa na maisha yangeendelea. Sasa wao wamedanganywa na matiss na maccm watawalinda wawalinde sasa wawe sawa na trump hata aking'ang'ania madaraka anakuwa raisi hewa mifumo yote ya uraisi inajiondoa haimpi ushirikiano.
Mdee na ujanja wake woote kameza ndoano ya ccm.
Cdm ndio chuo cha siasa pekee kilichobaki Ina kina mdee zaidi ya 200 ambao ni upcoming. Soon wanasaulika Kama kina slaa, kaburu, nk. Cdm haitegemei ruzuku kusurvive hata ikikosa wabunge. Ni taasisi itaandika propals hata pesa za kuimarisha demokrasia nchini wanapata.
 
Dada Rebeca, kubali kuwa Halima kaharibu mno. Nadhani hata yeye haamini upepo ulivyogeuka. Aombe msamaha atasamehewa ila kamwe heshima yake haiwezi kurudi.
Becky ni emotional kwasababu Halima ni msichana mwenzake ana muunga mkono nimemuelewa.
 
Msiojua, kikao cha KK juzi kilikuwa na lengo la kukitoa chama ktk mtanziko. Kuwasimamisha uongozi wateule 19 ni wa kimkakati kutuliza sintofahamu ya wanachama kwa kosa walilofanya kupeleka majina NEC. Kama wateule hawa wataoma msamaha ujue ndio lengo la kikao kile. Kuonyesha kuwa sio viongozi waliopeleka majina na kuwa watuhumiwa wameomba msamaha sasa tuwasamehe. Chadema haijawahi kufukuza mwanachama kisha kumpa siku 30 atafakari, wamefanyamhivi safari hii kuiondoa Chadema ktk Aibu ya kula matapishi yao ya sitaki nataka. Ukweli wanavihitaji viti hivi lakini kwa uungwaji mkono na wanachama. Walikosea na njia ya kutokea ilikuwa lazima iwe hivi. Hawa wote ktk siku 30 walizopewa kimkakati wataomba msamaha na maisha yataendelea huku wanachama wakipiga makofi. Ukitaka kulijua hili jiulze kwa nini mbunge wa Mpanda hajachukuliwa hatua kwa kukiuka maagizo ya chama kutotambua matokeo? Jiulize mke wa Bananga (Kampeni meneja wa Lissu) inawezekanaje aende kuapishwa Dodoma bila mume wake kujua wala asiripotie uongozi mipango hii.
Akili yako haipo vizuri.
 
Haya mambo ya demokrasia za vyama vingi kwa mtizamo wangu si utamaduni wetu waafrica. Hivi pande mbili hizi zingekutana na kutafuta muafaka wa kitaifa si mambo yangeisha vizuri tu.

Tatizo tumekubali kufanya siasa kama ushabiki wa simba na yanga ndio maana kila upande unataka kutunisha misuli uonekane una nguvu matokeo yake tunaigawa nchi. Hili suala lingemalizwa kwa vyama vyote kukaa chini kutafuta muafaka tuendelee kuijenga nchi yetu lakini tunapoendelea kutafuta mshindi kwenye ili ndio tunaharibu zaidi na tunazidi kuonesha kiwango chetu duni cha kustaarabika.

Mimi naamini kabisa kwa nguvu iliyopo nyuma ya hawa watu 19, wanaweza wakabaki na ubunge wao japo wamevuliwa uanachama, lakini je jambo hili litaacha makovu kiasi gani miongoni mwa wananchi walio wengi? Je, baadae tutaendelea kuwaona watu si wazalendo kwa nchi yao? Nina mashaka sana mambo haya hayatotuacha na TAIFA kama busara isipoendelea kutumika.
 
Habari wadau. Yajayo yanafurahisha.

Waliokuwa Wabunge wa Viti Maalum 19 wakiongozwa na Halima Mdee wameanza kutofautiana hasa baada ya kufutwa Uanachama, na mapokeo ya maamuzi hayo kwa BAWACHA wenzao na Wanachama kwa ujumla.

Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Dada mmoja kutoka Mbeya ameungana na wenzake na wameanza kushinikiza ili waende kuonana na mwenyekiti ili kuomba msamaha.

Jambo hili limeathiri mpango wa pamoja wa kutoa tamko kulaani kuvuliwa uanachama, kutokana na baadhi kutokubaliana na matamshi yanayokinzana na misimamo yao.

Muda unakwenda kasi, muda si mrefu tutasikia mapya juu ya mchongo mzima wa jinsi suala hili lilivyokuwa, watasema wenyewe na tutaelewa vizuri.
Sophia Mwakagenda anakubalika sana na wana Rungwe!
 
Sawa ni kweli hawajakomaa kwenye siasa lakini ndio muwaibie kura??

Siwezi kuwashangaa sana Upinzani. Hata Donald Trump anaamini kuwa ameibiwa kura. Huu ni utamaduni wa wale wasiokubali kushindwa uchaguzi!
 
Back
Top Bottom