Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

[emoji16][emoji16][emoji16]

Hakuna kitu kimewasumbua raia wanaogopa namba kama topiki ya Probability
Ilinitesa hadi chuo lakini sioni umuhimu wake kwenye maisha ya kawaida
 
wakati nasoma hii comment nimepata shida kuielewa kama ilivyokuwa kwenye kipindi cha hesabu kipindi kile
 
Hiyo hesabu ndo inayokuwezesha sasa hivi kutumia simu ya mkononi na kupata high speed data rate kiwango cha 4G na kuendelea aligunduwa Bwana Claude Shannon miaka ya 1940s
 
Ilinitesa hadi chuo lakini sioni umuhimu wake kwenye maisha ya kawaidaView attachment 1964966
Kosa tunalifanya ni kufundisha wanafunzi wetu kuelewa vitu, badala ya kuwafundisha wanafunzi wetu wajue kujifunza kuelewa vitu. Nina uhakika tusingewafundisha kwa staili ya sasa, hiyo hesabu ingekuwa imeishatafutiwa njia nyingine rahisi na inayovutiwa na vijana wetu!

Mimi, nikuchekeshe nilifanikiwa kuelewa probability kupitia kipindi cha Television cha learning kilichokuwa kina rushwa kwenye channel ya DSTV!

Probability na kada nyingine za kimahesabu zinahitaji nguvu ya hali ya juu ya 'real imagination'. Yaani kufikiria kichwani na kutengeneza taswira sahihi. Hii ni yakufanyia kazi hasa. Wanafunzi wa kihandisi wanapata tabu sana kwa kukosa nguvu ya ' imagination'. Na asikwambie mtu, usipoelewa ukakariri tu, hutakaa uelewe kutatua tatizo linalohusiana na jambo ulilokariri.
 
Elimu yetu ni shida ukiachana na advanced level. Chuo tulifundishwa proba distribution kama 30 hivi normal, binomial, poisson,chi, t, f distribution etc na mpaka leo sijui matumiz yake kwenye real life.

Yaani mtu anafundishwa sijui differential eq akitoka hapo kibongo bongo inamsaidia nini.
 
Nyie ndio mlisoma Bwege Akimbia Mathematics (BAM)?
 
Wale waliosoma accounting na finace kidogo wako njema hesabu zao zinatumika
Yaani mtu unafundishwa hyperbolic function au numerical method halafu ukitoka hapo [emoji38][emoji38][emoji38]
 
Elimu yetu ni shida ukiachana na advanced level. Chuo tulifundishwa proba distribution kama 30 hivi normal, binomial, poisson,chi, t, f distribution etc na mpaka leo sijui matumiz yake kwenye real life.
Mkuu, hizo makitu zinakazi yake kwenye utafiti. Zinasaidia sana kupata majibu ya kitakwimu ili ujenge hoja ya kufanya hitimisho la kitafiti za kisayansi.


Yaani mtu anafundishwa sijui differential eq akitoka hapo kibongo bongo inamsaidia nini.
Hii nayo inakazi yake sehemu mbalimbali. Mfano kwenye kutafuta upenyaji wa nishati joto kwenye kuta mbalimbali zilizotengenezwa na yabisi, kimiminika ama gesi.
=====
Kwa ujumla, ilitakiwa mambo haya yafundishwa kwa pamoja, yaani kanuni na theories zake na matumizi ya theories hizo. Ukweli, chuoni mpagilio wa silabasi ulikuwa hivyo, mfano kwamba ukijifunza differential ama ordinary ama partial lazima ufundishwe na mambo ya heat and mass transfer ambayo ni application yake kwenye semister hiyo ama inayofuata. Sasa unaweza kukuta, mwalimu wa hesabu anamaliza topic zake, yule wa heat ama fluid anarukaruka tu hamalizi ama na wahesabu anarukaruka! Kibaya wote wakirukaruka ni mtiti kwa mwanafunzi.

Pia sina hakika kama TCU, kwenye kupitisha mitaala yote nchini kwa vyuo vikuu kama huwa wanazingatia logic niliyoeleza hapo juu.

Mkuu, nakushukuru sana kwa kuniwezesha kufunguka. Ha ha haaa!
 
Dah.... Wazungu watatutawala sana, kama mtazamo kwenye mahesabu ndo tuko hivi basi tena!

Kimsingi Albet Einstein alifuatwa ili awe Rais wa kwanza wa Israel, jamaa kwa akili alizonazo akajibu siasa ni ngumu kuliko fizikia. Akagoma kabisa, japo waisrael wenyewe walimkubali sana kiakili!
 
Acha ujinga mkuu na hadithi za kusadikika aka abunuwasi.
Na kompyuta unayoitumia imeletwa na viumbe eti?
Dunia ya sasa ina innovations kubwa sana kuliko ma pyramid ambayo hayana kazi yoyote ya maana.
Kiukweli hesabu ilotumika kwenye mapiramidi haijavunjiwa rekodi mpaka leo!
 
Umenena kweli mkuu
 
Walikuwa wanatafuta kipenyo
 
Hutumika kukokotoa aina za kani za kiumeme (electrical power triangle), mfano reactive, apparent, na real power hizi unalazimika kutumia sin, cos ama tan kuzipata!!! Pia power factor za mashine za umeme!
Dah.... Uko vizuri, complex maths imetumika sana kwenye kuunda helicopter walicheza sana na angular momentum mzee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…