Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Waliogundua hesabu ngumu walikuwa wanatafuta nini na walizigunduaje?

Ilinitesa hadi chuo lakini sioni umuhimu wake kwenye maisha ya kawaidaView attachment 1964966
Kwenye maisha ya kawaida proba ina application muhimu ila huwezi kuona kwa jicho la kawaida. Kwenye uwanja wa medani utengenezaji wa silaha na madhara inayoweza leta silaha iyo kama itatumika au utengenezaji wa vitu viwandani na kupima ubora wa bidhaa.
Komaa jamaa hayo madude yanatesa kama bawasiri asee
 
Na hesabu ngumu kuliko zote duniani ni ipi na hiyo hesabu inakuwa ngumu ikitafuta kitu gani?
Hesabu ngumu ni mfano wa hii:
Ikiwa Basi limebeba abiria 40 wenye uzito wa wastani wa kilo 65 kwa Kila abiria na uzito wa Basi ni tani 3.5,
Taja uzito wa taili mbili za mbele iwapo zikitolewa upepo
 
Applications zipo nyingi mkuu..Hata utengenezaji wa barabara pindi gari inapotembea ktk curved path huangaliwa CENTRIPETAL FORCE inabidi iwe kubwa kuliko CENTRIFUGAL FORCE..Nisahihisheni km nimekosea.
 
Hizo hesabu zilianza kugunduliwa kwa kufanya assumptions nyepesi tuu. Mfano calculus aliyezigundua alikuwa anajaribu kutafuta Gradient(slope) ya mstari ambao haujanyooka (curve) maana hapo mwanzo gradient(slope) ilikuwa inatafutwa kwa mstari ulionyooka( straight line).
So far nadharia nyingi za kimahesabu zimeonekana kuwa ni mwendelezo au marekebisho au ugunduzi mpya wa wanafunzi fulani kutoka awali walipoishia waalimu wao au wakubwa wao katika kazi.
Mfano THOMSON alikosolewa na mwanafunzi wake Ernest Rutherfod. So far Rutherford nae alikosolewa na mwanafunzi wake James Chadwik.

Isaack Newton alipata kufundishwa na mwalimu wake ambaye nae alikuwa mtaalamu wa mahesabu Isaac Barrow. Tafiti nyingi za Newton zilitokana na kukosoa tafiti za waalimu wake.
wakati nasoma hii comment nimepata shida kuielewa kama ilivyokuwa kwenye kipindi cha hesabu kipindi kile
Apply log mtu wangu. Utaielewa.... au tumia Chi square table of distributions😂😂😂
unanipiga na kitu kizito kichwani🤣
 
Kwenye maisha ya kawaida proba ina application muhimu ila huwezi kuona kwa jicho la kawaida. Kwenye uwanja wa medani utengenezaji wa silaha na madhara inayoweza leta silaha iyo kama itatumika au utengenezaji wa vitu viwandani na kupima ubora wa bidhaa.
Komaa jamaa hayo madude yanatesa kama bawasiri asee
Hiyo ilikuwa 2018 mkuu
 
Hizi mambo za mahesabu magumu ndio zilinifanya niache shule niingie kwenye biashara ya majeneza huku hakuna hesabu maana mtu mzima akifa urefu wake unajulikana na hata mtoto pia
 
Waafrika ni vilaza wa kugundua fomula za hesabu ila wanaweza kuzikariri. Unakuta mtu ni Prof ila hajawahi gundua formula yoyote ya maana.
Kuna jamaa anaitwa Terence Tao ndio mchawi wa hesabu wa kizazi cha sasa.
Waafrika tunatia huruma sana ndio maana hatuna teknolojia za maana.
Sisi tuambie mdumange, gobogobo,mahngoma, mchiriku,amapiano, singeli, ndomboro nk mzungu zmanasibiri.
Hapo unesahau vumbi la kongo
 
Ya kuamka asubuhi kwenda kazini na kurudi jioni
lugha nzuri ungesema hujui umuhimu wake, maana ukisema huoni inamaana unafahamu applications zake ila hujaona popote kwe maisha yako ya kila siku, mfano kwe ujenzi wa barabara na majengo makubwa upimaji wa angles na heights hutumia principles za trig sa inawezekanaje mtu ukawa hupiti barabaran kwe maisha yako ya kila siku?
 
Mimi machinga pale karume na trig wapi na wapi
 
Kwenye kona Atasema anaongeza centripetal force [emoji23][emoji23]
Hahaa centripetal na centrifugal forces mara nyingi inatumika sana kwenye round about, Daah umenikumbusha mambo ya Physics.
 
Dah.... Wazungu watatutawala sana, kama mtazamo kwenye mahesabu ndo tuko hivi basi tena!

Kimsingi Albet Einstein alifuatwa ili awe Rais wa kwanza wa Israel, jamaa kwa akili alizonazo akajibu siasa ni ngumu kuliko fizikia. Akagoma kabisa, japo waisrael wenyewe walimkubali sana kiakili!
Sijihusishi na hoja ya Wazungu kututawala hapa. Bali naitizama Hoja ya A. Einstein na Urais wa Taifa la Israel. Kwa kweli jamaa alikuwa sahihi kabisa - Tena MNO!. Hebu jiulize aisee, ni nani mwanafizikia aliyewahi kupigwa marisasi kwa sababu ya fizikia yake? Ni nani aliyewahi kuwekewa sumu kwa ajili ya Mathematics zake? Ukiwa mwanasiasa e.g. Urais ujue kwamba saa yoyote usioijua Unaweza kuwekwa Lock-up, kumiminiwa risasi, Kupotezwa a.k.a kutupwa, kuwekewa sumu, utajadiliwa na kudhihakiwa sana/mno kwenye mitandao n.k.
Namkumbuka mzee Pythagora ambaye Maaskari walimuua kwa sababu alikuwa amechora pembetatu mraba(Right-angled Triangle) barabarani na ameinamia kutaka kujua uhusiano kati ya mistari yake (urefu ) na kwa bahati mbaya hao majamaa(Askari) walikuwa wanapitisha Gwaride lao hapo. Pythagora aliwataka wasiukanyage mchoro wake bali wapite pembeni kidogo. Alipokataa kuwapisha na akawa mbishi wakamwua bila kujua alikuwa anasolve a2 + b2 = c2.
Siasa naiogopa mno kuliko UVIKO 19.
 
wenyewe wa PCB na PCM wanakwambia hesabu ndio ya kupumzikia[emoji28][emoji28][emoji28]

kweli duniani tuko tofauti sana.
yaani aliyefaulu masomo yote alama za juu anaonelea bora akapumzike kwenye hesabu PCM kuliko kukumbana BIOLOGY ya PCB.
Kwa mtu wa PCM Hesabu ndo slope. Na hata ukichekia matokeo utaona Mathe wanaburuza.

Achana na mziki wa PHYSICS asee!
 
Ni rahisi mtu wa sayansi kubutua A ya Mathematics kuliko physics na Binafsi ule msuli wa kujiandaa kuingia form 5 ulinionya mapema kuwa physics huiwezi nikaaimia zangu EGM na bado Math nikaosha A 😀😀😀
 
Kwa mtu wa PCM Hesabu ndo slope. Na hata ukichekia matokeo utaona Mathe wanaburuza.

Achana na mziki wa PHYSICS asee!
Kipindi napiga msuli wa kujiandaa kuingia form 5 niliona Physics siiwezi kabisaaa na nikaachana nayo.
 
Sasa mkuu unamuwazaje mtu mwenye PhD ya hisabati....[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...yaani huyo namba zikimuona zinaanza kujipanga zenyewe ktk mtiririko wa jibu...[emoji23][emoji23][emoji23]....
 
Back
Top Bottom