Wenzio wanaongelea facts, wewe unaongelea hisia. Uwe unafuatilia mambo kwa weledi siyo kwa hisia na mihemko ya unachokitaka.
Ni kweli kuwa Urusi ina jeshi kubwa zaidi, na bila shaka silaha nyingi zaidi, na pesa nyingi zaidi, LAKINI hiyo haijaondoa ukweli kuwa imeshindwa kuipiga Ukraine. Ndiyo maana unaona kila mara mpaka inafanyika mipango ya kubafilishana askari mateka. Hiyo ina maana kuwa Russia kuna wakati inazidiwa kiasi cha askari wake kujisalimisha.
Tena kabla hata ya msaada wowote kutoka nchi za Magharibi, ikiwa inatumia askari wenye ujuzi wa juu, Urusi iliingia Kiev, ikakimbia baada ya kupoteza askari wengi, tofauti na plan yake ya kumaliza vita ndani ya siku tatu.
Mtaalam mmoja wa vita aliwahi kusema kuwa unapoanzisha vita, unajua itakavyoanza, lakini huwezi kujua itakavyokwisha. Na ndiyo kinachowatokea Russia. Wanajua tarehe waliyoanza vita lakini hawajui itaisha lini na itaisha kwa namna gani.