Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Wewe bado unsuliza bei tu?! Hutajenga. Ni hivi Tafuta floor plan Google. Changa ikifika 3m nenda kaanze na msingi then ukipata 300,000/4/5 unapandisha Boma mdogo mdogo. Trust utamaliza bila kujua umewezaje.
Sure ujenzi hutakiwi kusubiri uwe na hela yote hautakaa ujenge maana matatizo mengi na hela haikai, vifaa vya ujenzi vinapanda kila siku.
 
Komaa mkuu utatoboa tu mdgo mdgo! Nkushauri anza kununua tofali zote zinazohtajika then jichange muite fundi then akikisha upige mpka lenta, usiache boma muda mrefu bila lenta!
Hivi inamadhara boma kukaa mda bila lenta??
 
Hongera sana kamanda.
Ulinunua bati gani ? Bati Bomba, Simba dumu, sunshare au ipi ? Na kwa piece moja ulifanyiwa bei gani ?
Mkuu nasikitika kukwambia kwamba kwa wakati tuliopo bado jibu la swali lako halitakuwa na afya tena kutokana na vitu sokoni havieleweki bei atakayokupa hapa hata ukisema ni kwa makadirio tu ukifika dukani unakuta imeji-double.

Ni mtihani sana!
 
Kuzuia deflection ( ukuta kupinda kuingia ndani au kutoka nje) kutokana na subsidence ya ardhi unaweza usione kwa macho lkn utokea! Hi hali usababisha nyumba kuwa nyufa.
Nakazia
 
Kujenga ni technique..nilipigwa nyumba ya kwanza lakini sasa nimejifunza, kifupi jiweke kidalali sio kiboss..
1. Msingi nawauzia vibarua, tunakubaliana, alafu fundi anasimamia
2. Tofali namuuzia fundi sh 300 japo za juu wengine wanadai nyongeza kidogo
3. Kokoto, nanunua kifusi cha kokoto alafu nachambua..hapo napata kifusi na kokoto
4. Tofali nanunua 950
5. Nondo naenda scrap yard napima zilizopo alafu zile pande ndefu nanunua..
6. Grill nachukua nondo hapo hapo scrap yard nanunua bomba za pembeni tu
7. Mbao za kuezekea nachukua buguruni, ukitaka kuwaweza madalali..nenda na mwanao tu alafu mfanye yy ndio boss, waite pemben waambie nimemleta boss, watakupa bei halisi
8.Bati mara nyingi hazina shortcut
9. Tiles kama unahitaji box chache..mafundi wanazo tena konk sana
10. Wire, mafundi wanazo nzuri tu sema earth rod kanunue copper inakuwa na bei kidogo kwenye 45k kwenda juu..chini ya hapo kafukue chuma hicho
11.Nenda mwenyewe dukani
NB: Nyumba inahitaji usimamizi wako, sio ndugu au rafiki, utalaumu watu bure
Kuwa mkali sana kwenye mali zako, simamia kila eneo..
Umetisha [emoji1534]
 
RRONDO njoo nshapata floor plan wats next
Screenshot_20211216-223357_1639683539615.jpg
 
Back
Top Bottom