Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Waliojenga mwaka 2021 tunaomba uzoefu wenu

Kama mpaka hapo umetumia 10M umeupiga mwingi sana maana vifaa ni kichaa Nondo ndio usiseme yaani ni balaa fire, hapo ukitaka iwe ya kuingia hata kwa shida shida unatakiwa isipungue 10M nyingine maana ukiguza mbao za treated na zenyewe ni balaa na nusu, hujaongelea bati hapo maana kadirio la chini kwa mjengo huo sio chini ya 3.5 Alaf
Jengeni...tunasubiri mkufe..tuungane na wake zenu ..mtajua hamjui
 
Mlango upo direct koridoni
Nimemaanisha kuwe na kama step 1 ya kuingia kama kajikorido ndo malango.
Sio mlango ukifungua inabidi kujihakikishia hakuna anayepita..
Lakini kama umeona upo sawa hamna shida
noted asante kwa ushauri mkuu
 
Kujenga ni technique..nilipigwa nyumba ya kwanza lakini sasa nimejifunza, kifupi jiweke kidalali sio kiboss..
1. Msingi nawauzia vibarua, tunakubaliana, alafu fundi anasimamia
2. Tofali namuuzia fundi sh 300 japo za juu wengine wanadai nyongeza kidogo
3. Kokoto, nanunua kifusi cha kokoto alafu nachambua..hapo napata kifusi na kokoto
4. Tofali nanunua 950
5. Nondo naenda scrap yard napima zilizopo alafu zile pande ndefu nanunua..
6. Grill nachukua nondo hapo hapo scrap yard nanunua bomba za pembeni tu
7. Mbao za kuezekea nachukua buguruni, ukitaka kuwaweza madalali..nenda na mwanao tu alafu mfanye yy ndio boss, waite pemben waambie nimemleta boss, watakupa bei halisi
8.Bati mara nyingi hazina shortcut
9. Tiles kama unahitaji box chache..mafundi wanazo tena konk sana
10. Wire, mafundi wanazo nzuri tu sema earth rod kanunue copper inakuwa na bei kidogo kwenye 45k kwenda juu..chini ya hapo kafukue chuma hicho
11.Nenda mwenyewe dukani
NB: Nyumba inahitaji usimamizi wako, sio ndugu au rafiki, utalaumu watu bure
Kuwa mkali sana kwenye mali zako, simamia kila eneo..
Nyumba sio kitu unaweza jenga kila mwaka so mambo ya kuwa cheaper sijui nondo ambazo zipo scraping yard utakuja kulia pale nyumba itakapoanza kupasuka ni bora kuwa mvumilivu na kutumia bidhaa zenye ubora unaotakiwa … kumbuka labda hiyo ndio nyumba pekee utayoweza jenga Maisha yako yote
 
Nyumba sio kitu unaweza jenga kila mwaka so mambo ya kuwa cheaper sijui nondo ambazo zipo scraping yard utakuja kulia pale nyumba itakapoanza kupasuka ni bora kuwa mvumilivu na kutumia bidhaa zenye ubora unaotakiwa … kumbuka labda hiyo ndio nyumba pekee utayoweza jenga Maisha yako yote
Kwamba nondo zinazokuwa pale zinakuwa sio bora?...
Alafu nyumba ukisubiri upate pesa ndio ujenge, hutakaa ujenge maisha yako yote..angalia bei ya vifaa vya ujenzi leo, linganisha na miezi sita iliyopita
 
Back
Top Bottom