Ahsante mkuu. Lakini kamwe usitishwe na maneno ya watu wala usitake kwenda kwa mwendo wa watu wengine.
Furahia kila hatua unayopiga kwenye maisha, hata ikiwa wengine wanaona hausogei au mwendo wako wa taratibu, hakikisha haukatishwi tamaa.
Nilichojifunza.
1. Fundi anakuvuta kadri awezavyo uingie king, ukishaingia lazima kazi imalizike. Namaanisha atakupa makadirio madogo na kuna baadhi ya vitu hatakwambia awali ili upate moyo wa kuanza. Hapo ndio utakapoanza kupewa bill ndogo ndogo na hauwezi kuishia njiani.
Msisitizo, pitia mara mbili mbili na uliza maswali ya kutosha ukishapewa makadirio. Pia tafuta wengine wawili ili ulinganishe gharama na makadirio.
2. Sio lazima fundi unaeanza nae umalize nae. Wengine akishaona amekamata mradi anajua ndio pa kukupiga na anafikiri unapesa za mchezo. Mie msingi alijenga mwingine. Boma akapandisha mwingine. Finishing wengine, kuezeka wengine. Kuweka dari wengine kabisa. Hata hawahusiani.
3. Simamia manunuzi ya vifaa mwenyewe. Fundi akikupeleka sehem kununua vitu usijekufikiria uwe makini, kuna mmoja alikua anaenda kuongea na jamaa kabla sijaenda ili nipigwe bei kisha cha juu achukue yeye. Uzuri nilikua na mahusiano mazuri na mwenye duka, akanishtua, nilimfukuza kabla hajamaliza msingi na tulimalizia na kibarua wake.
Huyo alinipiga kwenye tofali.
Mwingine akanipiga kwenye mbao. Huyo nae nikafukuzilia mbali. Kwanza alinipa running meter utafikiri naenda kuezeka shule, mie nikipiga hesabu, napata 380, yeye ananiambia 620 kibarua kikaota nyasi.
Hauwezi kukwepa kabisa kupigwa ila unaweza kupunguza maumivu.