Waliojipatia Milioni 280 kwa njia ya Mtandao watozwa Faini ya Laki Tano

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu Amiry Luwiso na Ashirafu Awadh waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Sh milioni 280 kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka yanayowakabili.

Hukumu hiyo iitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya washtakiwa hao kutimiza masharti ya makubaliano ya kukiri kosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Akiwasomea hukumu hiyo, Hakimu Mazengo alisema mahakama imetoa hukumu hiyo kwa kuzingatia kitendo cha washtakiwa hao kukiri mashtaka yao bila kuisumbua mahakamani na kwa kuzingatia makubaliano kati yao na DPP.

Chanzo: Habari Leo
Hii ni kuwaambia wezi na matapeli waendelewee na kazi kwa spidi ya G5.
TanzaGIZA!!
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu Amiry Luwiso na Ashirafu Awadh waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Sh milioni 280 kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka yanayowakabili.

Hukumu hiyo iitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya washtakiwa hao kutimiza masharti ya makubaliano ya kukiri kosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Akiwasomea hukumu hiyo, Hakimu Mazengo alisema mahakama imetoa hukumu hiyo kwa kuzingatia kitendo cha washtakiwa hao kukiri mashtaka yao bila kuisumbua mahakamani na kwa kuzingatia makubaliano kati yao na DPP.

Chanzo: Habari Leo
Mwenye pesa Huwa hafungwi
 
Yaani matapeli wanawaibia watu milioni 280, wanatozwa faini ya laki 5! Halafu yule masikini aliyekamatwa na nyama ya porini, alihukumiwa miaka 20 na yule Hakimu wa Mafinga!!

Hii nchi kwa hapa tulipofikia, tunahitaji Katiba Mpya.
Katiba mpya haina maana kama Taifaa halitapiga vita rushwa kwa nguvu zoteee... penye rushwaa sheria ni takataka tu
 
Nadhani hapo adhabu sio hiyo laki 5 wala miezi 6, adhabu kamili iko kwenye makubaliano na DPP.

Kinachoonekana ni kwamba walishakubaliana na DPP kama ni kulipa ama kurudisha pesa.

Hapo ilitakiwa yasomwe makubaliano ya hao jamaa na DPP ndio tuelewe adhabu kamili ni ipi.

Maana ukishakubaliana na DPP kinachofuata ni kupunguziwa adhabu tu.
nilikuwa natafuta comment kama hii kabla sijacomment, kwa vile umemaliza kila kitu sina haja ya kucomment tena.

hata hyo miezi sita au faini laki tano wameonewa tu.
 
hata singasinga wa iptl aliachiwa huru baada ya kufanya plea bargain na dpp, hakutozwa hata faini, sijui hata mnashangaa nn hapa
 
Yaani matapeli wanawaibia watu milioni 280, wanatozwa faini ya laki 5! Halafu yule masikini aliyekamatwa na nyama ya porini, alihukumiwa miaka 20 na yule Hakimu wa Mafinga!!

Hii nchi kwa hapa tulipofikia, tunahitaji Katiba Mpya.
...Na Katiba Wanaicheliwesha Makusudi na Sisi tunachekea TU kama Mabumunda !
Ya Niger yanatuhusu Sana sisi wakati kuondoa Ujinga kama huu...![emoji35][emoji35]
 
Nadhani hapo adhabu sio hiyo laki 5 wala miezi 6, adhabu kamili iko kwenye makubaliano na DPP.

Kinachoonekana ni kwamba walishakubaliana na DPP kama ni kulipa ama kurudisha pesa.

Hapo ilitakiwa yasomwe makubaliano ya hao jamaa na DPP ndio tuelewe adhabu kamili ni ipi.

Maana ukishakubaliana na DPP kinachofuata ni kupunguziwa adhabu tu.
...Kwa hiyo Wanaweza Hata kumkatia Nusu DPP ili awape Adhabu ya Kitoto hivi ? Ye DPP anachunguzwa na nani ??? [emoji35][emoji35][emoji35]
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imewahukumu Amiry Luwiso na Ashirafu Awadh waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya kuongoza genge la uhalifu kwa njia ya mtandao na kujipatia zaidi ya Sh milioni 280 kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Sh 500,000 kila mmoja baada ya kukiri mashtaka yanayowakabili.

Hukumu hiyo iitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo baada ya washtakiwa hao kutimiza masharti ya makubaliano ya kukiri kosa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Akiwasomea hukumu hiyo, Hakimu Mazengo alisema mahakama imetoa hukumu hiyo kwa kuzingatia kitendo cha washtakiwa hao kukiri mashtaka yao bila kuisumbua mahakamani na kwa kuzingatia makubaliano kati yao na DPP.

Chanzo: Habari Leo
Mahakama zetu kha

Yule msanii Chato aliyeshaeishiwa akiri asiisumbue mahakama wakamlima miaka kibao gerezani
 
Nchii hii inaongozwa na watu wa hivyo ningeishika mm Kuna watu wangehama hii nchi nisingecheka na nyani
Nchi za Afrika haziendelei kwasababu
1. Kuwepo kwa katiba mbaya ambayo inawaruhusu viongozi wawe na sauti kuliko katiba na sheria
2. Sheria mbovu
Hata wewe ungekuwa raisi usingeweza kusaidia bila kubadilisha katiba na sheria sbb wanadamu muda wetu wa kuishi ni mfupi sana. Utaondoka mambo yale yale
N.B
  • Bunge linatakiwa lijitegemee
  • Polisi wanatakiwa wawe na elimu kuanzia form diploma mpk chuo na polisi lijitegemee hakuna kufungamana na siasa
  • JWTZ linatakiwa liwe na watu waliomaliza diploma na degree
  • NEC inatakiwa ijitegemee
  • Katiba irekebishwe ambayo itamuondolea kiongozi kutokuwa na kinga ya kushitakiwa. Hapa raisi akifanya ufisadi au kusaini mkataba mbovu ashitakiwe na kutaifishwa mali zake. Hii kwa viongozi hadi wa chini.
  • Sheria zipitiwe upya mojawapo ya sheria ni kwamba mtu akifanya ufisadi anataifishwa, anafukuzwa kazi na kulipa faini km fidia
  • Kuwepo na vyuo vya ufundi
  • Kuwepo na vyuo vya mpira
 
Back
Top Bottom