chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Wale wawekezaji wa michongo Sasa wanahaha, Chato Ina magesti house mengi saana na yamejengwa kwa mikopo, wengi waliojenga walitarajia mzee angekaa madarakani miaka mingi sana. Kuna makumi ya magesti hayajaisha, mengine yameisha.
Sasa yale yalioisha hayana wateja kabisa, yale yaliyokuwa yanajengwa yamesimama, mikopo ya kulipwa benki waliyokopa imeiva.
Kinachofata ni mashinikizo kwa wanasiasa na wakati mwingine wanawapa Hela ili angalau Chato iwe Mkoa warudishe mikopo. Wanasiasa wengi wanaotaka Chato iwe Mkoa wako kwenye payroll ya wafanyabiashara, wanalalamika waliingizwa mkenge.
Bado we waliojenga viwanda
Yale mataa ya barabarani yanayowaka usiku pale Chato yanasaidia kumulika umasikini mkali uliotamalaki na kuthibitisha hoja ya Nyerere kwamba maendeleo ni ya watu, sio ya vitu, wananchi wanatembea kwa miguu kurudi na kwenda makazini huku wakimulikwa na taa za barabarani, wanalala njaa majumbani huku wakichungulia dirishani wanaona barabarani Kuna taa zinawaka usiku.
Mawaziri na viongozi waliolazimishwa kununua viwanja Chato wanahaha kupata mteja wa kuwauzia kwa karibu mwaka sasa.
Ajenda ya chato kiwa Mkoa sio ya wananchi, ni ya wafanyabiashara na wanasiasa, wananchi wanataka Samia awatoe kiuchumi tu na kusomesha watoto wao ambao waliachwa wakihaha