Waliokuwa na bidii na elimu lakini wapo mtaani wanadharaulika kwakuwa jamii iliweka matarajio makubwa

Waliokuwa na bidii na elimu lakini wapo mtaani wanadharaulika kwakuwa jamii iliweka matarajio makubwa

Tunahitaji wakalimani, wanasheria, HR’s nk hawa wote hawasomi sayansi.
Wanasheria na HR’ mtoto yeyote aliyesoma masomo ya sayansi anaruhusiwa kusoma degree zake

Mfano PCB na PCM huruhusiwa Kusoma digriii ya kwanza ya sheria na HR bila shida
Walisoma sayansi Wana wigo mpana sana
 
Wanasheria na HR’ mtoto yeyote aliyesoma masomo ya sayansi anaruhusiwa kusoma degree zake

Mfano PCB na PCM huruhusiwa Kusoma digriii ya kwanza ya sheria na HR bila shida
Wewe unafahamu wwzazi wanavyopata shida kusomesha watoto mpaka wanahitimu degree ya kwanza, leo hii unasema taaluma nyingine zianzie kwenye shahada ya uzamili nani atagharamia?

Kwanini nchi za Ulaya imewezekana kwetu ishindikane? Tuangalie ubovu uko wapi katika utoaji wa elimu yetu.
 
Uongo inattegemea ulichosoma. masomo ya sayansi hakuna kukariri lazima uelewe ulichosoma
Degree za Arts zifutwe

Misomo ya Arts ni aibu kwa nchi ndio inazalisha watu wa kukariri huwezi soma digriii ya engineering au udaktari ukafaulu kwa kukariri

Na huwezi soma combination za sayansi kama PCB, PCM ukafaulu kwa kukariri
Masomo ya art yanataka uelewa na sio kukari kama sayansi.
Maana sayansi huwa haina majibu mawili na huwa hayabadiliki miaka.
Kufaulu sayansi ni uwezo wako tu wa kukariri.
Magazijuto, archimedes principle, algebra, quantum,nk majibu ni hayo hayo miaka.
2+2 haijawahi kubadili.
Art inataka reasoning,sayansi ni claiming capacity yako tu.
 
Atajighariimia mwenyewe digriii ya pili ya kwanza asome yenye soko mfano kasomea umeme atafanya kazi kukusanya pesa atajisomesha kuliko umpeleke kusomea digriii isiyo na demand au ambayo hataweza kuitumia mtaaani bora umpe hiyo hela afungue biashara
 
Nilikuwa na kadhia hiyo. Watu niliowaacha form 4 na darasa la Saba ndiyo walianza kunifundisha maisha mengine huku wakinisimanga sana kwamba kusoma sana hakujasaidia kitu, ingawa wale jamaa walinisaidia sana.
Nilikuwa na mawazo makaali sana. Ila nashkuru Mungu alinikumbuka nikaachana na zile stress.
 
Wanasheria na HR’ mtoto yeyote aliyesoma masomo ya sayansi anaruhusiwa kusoma degree zake

Mfano PCB na PCM huruhusiwa Kusoma digriii ya kwanza ya sheria na HR bila shida
Walisoma sayansi Wana wigo mpana sana
Sababu sheria ni thinking na sio claiming.
 
Atajighariimia mwenyewe digriii ya pili ya kwanza asome yenye soko mfano kasomea umeme atafanya kazi kukusanya pesa atajisomesha kuliko umpeleke kusomea digriii isiyo na demand au ambayo hataweza kuitumia mtaaani bora umpe hiyo hela afungue biashara
Huoni kama kuna hatari ya baadhi ya taaluma kukosa wataalamu, tutaishia kukodi wanasheria kutoka Kenya na Uganda.
 
Masomo ya art yanataka uelewa na sio kukari kama sayansi.
Maana sayansi huwa haina majibu mawili na huwa hayabadiliki miaka.
Kufaulu sayansi ni uwezo wako tu wa kukariri.
Magazijuto, archimedes principle, algebra, quantum,nk majibu ni hayo hayo miaka.
2+2 haijawahi kubadili.
Art inataka reasoning,sayansi ni claiming capacity yako tu.
Sayansi huijui inatumika zaidi kwenye application mfano uliotoa hayo mahesabu mwisho wa siku unayatumia mfano kujenga majengo, kuunda ndege na mitambo nk hayapo hapo kwa ajiri ya kukaririwa ndio maana lazima kuwa ili nitengeneze meli ielee na isizame mahesabu ya kila eneo yaweje nk ndege ili iruke mahesabu yake ya kila eneo yaweje
 
Ni lile kundi la watu ambao tulisoma nao shuleni na vyuoni, walikuwa serious sana na elimu na waliweza kuwa na matokeo mazuri sana, wengi walisifika kwa kuitwa majina maarufu kama vipanga.

katika fikra za wengi hawa walikuwa wanaonekana tayari wana future nzuri maana wakimaliza tu elimu zao basi wana maisha

kiukweli yalikuwa ni matarajio makubwa sana lakini kwa uhalisia mambo yapo tofauti kabisa na ndio maana wapo ambao wapo mitaani kwa kukosa ajira au kukosa mitaji.

changamoto kubwa wanayoipata ni kwamba tayari walijizolea umaarufu wa kuwa na uwezo mkubwa darasani hivyo kila anaekutana nae anajua ana bonge la kazi au cheo shirika flan na lazma aulize ili kuthibitisha. wengine masnich tu anajua kila kitu lakini anauliza makusud ili tu amtibue.

basi baada ya hapo kinachofuata anaweza kudharaulika sana ama kuonewa huruma sana kama mtu mgonjwa asiejiweza maana alitarajiwa afike mbali sana kwa juhudi zake ila hakuna alichoambulia, mbaya zaidi katika kundi la waliomdharau hilo kunaweza kuwa na wenye ajira au biashara zao basi wanasambaza sumu kwamba elimu si kitu kwa kumfanya mwenzao awe mfano.
Laiti ajira zingekuwepo,wale waliokuwa vipanga darasani,wangekuwa na maisha mazuri,Hilo halina ubishi.Mtu katoka chuo kikuu na GPA ya juu,ni Muhandisi,muhasibu,Dokta,unafikiri akipewa nafasi vitengo nyeti lazima atafanya masjabu.
Hawa maprofesa unaowaona leo,kama serikali isingewapa nafasi za kusoma nje na ajira za uhakika ,wangekuwa makapuku watupu,
Hakuna miujiza waliojariwa wanafanya kuwa na maisha mazuri,mtu yeyote ukimpa nafasi atafanya miujiza.
Hawa unaowaona wana maisha mazuri serikalini,sio kwamba Wana akili sana,wakipoteza hizo ajira wanakuwa choka mbaya tu
 
Sayansi huijui inatumika zaidi kwenye application mfano uliotoa hayo mahesabu mwisho wa siku unayatumia mfano kujenga majengo, kuunda ndege na mitambo nk hayapo hapo kwa ajiri ya kukaririwa ndio maana lazima kuwa ili nitengeneze meli ielee na isizame mahesabu ya kila eneo yaweje nk ndege ili iruke mahesabu yake ya kila eneo yaweje
Lkn wanatumia kanuni ambazo hazibadiliki
 
Lkn wanatumia kanuni ambazo hazibadiliki
Zinabadilika kutegemea mazingira na levels mfano mbili mara mbili ni nne kwa hesabu za chekechea lakini ukienda kwenye uzalishaji mfano una mbegu mahindi mbili mkono wa kushoto na mbegu mbili mkono wa kulia ukazipanda moja moja kwenye shimo moja zikaota Hali ikawa nzuri mahindi yatakayopatikana punje zake huwezi jibu zitakuwa ngapi

Kwenye sayansi principle yaweza badiilika ndio maana wanasayansi kila kuchapo wanagunduaa vitu vipya na teknolojia mpya

Sayansi unaruhusiwa kwenda nje ya principle mradi utoe result nzuri inayokubalikaa
 
Masomo ya art yanataka uelewa na sio kukari kama sayansi.
Maana sayansi huwa haina majibu mawili na huwa hayabadiliki miaka.
Kufaulu sayansi ni uwezo wako tu wa kukariri.
Magazijuto, archimedes principle, algebra, quantum,nk majibu ni hayo hayo miaka.
2+2 haijawahi kubadili.
Art inataka reasoning,sayansi ni claiming capacity yako tu.
Degree zenu ni za hovyo sana na ni lazima mpate shida sana ya ajira!
Yaani graduate unaandika "claiming capacity" ukimaanisha ndio kukariri?! Very stupid graduates!
 
Uongo inattegemea ulichosoma. masomo ya sayansi hakuna kukariri lazima uelewe ulichosoma
Degree za Arts zifutwe

Misomo ya Arts ni aibu kwa nchi ndio inazalisha watu wa kukariri huwezi soma digriii ya engineering au udaktari ukafaulu kwa kukariri

Na huwezi soma combination za sayansi kama PCB, PCM ukafaulu kwa kukariri
Kwa hiyo hao wa sayansi walioelewa ndio wameajiriwa wote?
 
Kuna Degree za science hazina issue, Degree zenye issue za science night Udaktari, pharmacy, nursing,lab tech,
 
Nilikuwa na kadhia hiyo. Watu niliowaacha form 4 na darasa la Saba ndiyo walianza kunifundisha maisha mengine huku wakinisimanga sana kwamba kusoma sana hakujasaidia kitu, ingawa wale jamaa walinisaidia sana.
Nilikuwa na mawazo makaali sana. Ila nashkuru Mungu alinikumbuka nikaachana na zile stress.
Mkuu ni Kama Mimi kwenye kampuni yetu kazi zilivyoisha si hatukupewa malipo yetu yoyote Yale Sasa unatoka huko mtupu huna pa kuanzia na Mimi nimesomea civil engineering nilichofanya nilikuwa na viela kidogo nikaanzisha mradi wa Kuku Kama 20 hivi na badaye nikakusanya vijana wanne nikaanzisha kikundi Cha watu 5 tukaomba mkopo halmashauri tukapewa milion 4 na tulivyopewa tukauendeleza huo mradi kwa kuongeza Banda kubwa na Kununua Kuku wakafika 300 tumeendelea nao hao Kuku Kama miezi sita hizi tukarudisha huo mkopo wa mil 4 ila watu huku mtaani bado wakawa wananikebehi kwamba na degree yangu nitafugaje Kuku Yani ilikuwa shida aisee na baada ya kurudisha mkopo tukapewa Tena saivi mkopo wa mil 10 na saivi tumenunua mashine za kutengenezea mkaa wa kisasa unaotokana na mabaki ya mimea Naona kwa Sasa wametulia sio Kama awali niliyokuwa nafuga Kuku aisee Yani wasomi huku mtaani tunadharaulika Sana kama tukifanya kazi ambazo wengine wa mitaani wanafanya.
 
Hao uliowataja demand yao soko la ajira ni ndogo mno
Kusoma ni Investment kama zilivyo investments zingine kuwekeza kwenye eneo lenye demand ndogo ni uwekezaji mbaya

Kusoma hiyo Misomo ni uwekezaji mbaya kwa sasa
Demand ya wanasheria ni kubwa sana, tatizo ni umaskini wa kipato wa hao wahitaji.
 
Kwa hiyo hao wa sayansi walioelewa ndio wameajiriwa wote?
Wana uwezo mkubwa kuingia mtaaani na kumaliza survive kuliko wa Arts

Mtu kasomea umeme au ujenzi mtaaani anaishi hao Wengine atazunguka na vyeti hadi aaanguke kwa kizunguzungu
 
mkuu yale ma arrhenious law yanaeleweka kweli?? Mfumo wa elimu ya kibongo n wa kukaririshwa mkuu, hakuna kuelewa jambo.

Hata huko udaktarini pia n ukaririshwaji wenye ahueni. Kama ulisoma huo udaktari bila shaka ulipitia ishu kama drancuculus medinences.... Hawa microorganisms ulikaririshwa na si kuwaelewa.
Watu wanajua sayansi hakuna kukariri hahahahah. Kuanzia Engineering hadi u daktari ni kukariri mwanzo mwisho.......sema tu ni kukariri wenye nafuu
 
Back
Top Bottom