Waliokuwa wakiitukana awamu ya 5 waanza kujuta, watakiwa kuchutama

Waliokuwa wakiitukana awamu ya 5 waanza kujuta, watakiwa kuchutama

Kinuju

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2021
Posts
2,386
Reaction score
5,325
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.

Ni miaka sita sasa tangu Tundu Lisu aitabirie Tanzania mabaya ikiwemo kushitakiwa MIGA, ndege kukamatwa, uchumi kufilisika, kunyimwa misaada mbalimbali. Mpaka sasa hakuna hata kitu kimoja kilichotabiriwa na Lissu kilichotimia maaana yake aliwadanaganya watanzania, yani licha ya kusoma kwa kodi za watanzania yeye anakuja kufanya kazi ya kuwadanganya watanzania!

Kinyume na utabiri wa Lissu,Tanzania ya sasa imeingia uchumi wa kati, hatujashitakiwa MIGA na viwanda vya kuchenjua dhahabu vimejengwa Mwanza. Mapato ya madini yamepanda kutoka billioni 100 hadi billion 500, ndege hazikamatwi na watanzania ni wamoja zaidi kinyume na utabiri wake.

Baada ya kuona aibu Tundu Lissu na Lema badala ya kuwaomba msamaha Watanzania wao wamekimbilia Ulaya kwenda kulishwa bure na wazungu.

Lema na Lissu rudini nyumbani muwaombe msamaha Watanzania muanze kuishi kwa jasho lenu kwa kufanya kazi na siyo kulelewa.
 
Awamu ya Tano ilikuwa inauwa Biashara ifanye wote Masikini, ilitaka tugeuke mafukara wote ila watuendeshe vuzuri kabisa, hii ya sasa inagawanya mzigo kwa wote hata hao wanaojiita Wanyonge nao watalipa
Habari za porojo hizo za vibavicha. Unabiashara wewe?

Awamu ya 5 iliandaa mazingira mazuri hamna dalali wa kati anayejifanya yeye bandari.

Sema wewe unabiashara gani ili tuiangalie ilivyo athiriwa na awamu ya 5?
 
Hizi tozo zimewekwa na wanufaika wa utawala wa magu.

Walipoona magu amekua akisemwa vibaya wao wamekuja na hizi tozo onevu ili kuwaaminisha watu kua angekua magu asingeruhusu
 
Nakubaliana na wewe kabisa Kuna makusudi ili Rais aonekani hafai.
Bila kodi nchi haiendi, mnataka naye akakombe hela kwenye akaunti za akina Manji? Nashauri hata elimu bure iondolewe, ilikuwa ni kiki ya kisiasa isiyo na tija yeyote! Haiwezekani uzae watoto then serikali ikusomeshee!! Hizo hela ziende kwenye mambo mengine kama kilimo, miundombinu na maji.
 
Awamu ya Tano ilikuwa inauwa Biashara ifanye wote Masikini, ilitaka tugeuke mafukara wote ila watuendeshe vuzuri kabisa, hii ya sasa inagawanya mzigo kwa wote hata hao wanaojiita Wanyonge nao watalipa
Kalipe kodi ya uzalendo huko kenge wewe
 
Hizi tozo zimewekwa na wanufaika wa utawala wa magu.

Walipoona magu amekua akisemwa vibaya wao wamekuja na hizi tozo onevu ili kuwaaminisha watu kua angekua magu asingeruhusu
Hebu mpumuzisheni mzee wetu JPM mpambane na serikali iliyopo madarakani. Kwani nyie si ndo mlisema mama anaupiga mwingi, leo imekuwaje tena.
 
Bila kodi nchi haiendi, mnataka naye akakombe hela kwenye akaunti za akina Manji? Nashauri hata elimu bure iondolewe, ilikuwa ni kiki ya kisiasa isiyo na tija yeyote! Haiwezekani uzae watoto then serikali ikusomeshee!! Hizo hela ziende kwenye mambo mengine kama kilimo, miundombinu na maji.
Hvi kwenye simu tunakatwa VAT Bado na hyo Kodi ya serikali ambayo wamei double mara dufu Sasa hapo wanajemga uchumi gani kwa kunyonya watu wachini ka sikuongeza mzigo na watumiaji kupungua zaidi na mawakala kutupa line zao.

Uchumi inabidi umaimarishwe kwa kuangalia vitu vingi na sio kuongeza Kodi kwenye kila kitu nchini, mikodi kibao huku ajira hamna, wawekezaji nao hamna, Sasa kumkamua ng'ombe aliyekonda bila kumu feed ni kumuua mazima.

Hafu nchi hii Kodi huleta maendeleo kidogo kama tu matumizi ni 80% ya makusanyo na maendeleo ni 20% why wachoshe maskini.

Nchi yetu Ina rasilimali nyingi lazima tuzitumie hizo kuondoa umaskini na sio kukomoana. Binafsi hata transaction za simu kwa Sasa naacha kabisa Hela yangu haiendi bure kuwalipa wabunge hovyo wasio katwa Kodi.
 
Hvi kwenye simu tunakatwa VAT Bado na hyo Kodi ya serikali ambayo wamei double mara dufu Sasa hapo wanajemga uchumi gani kwa kunyonya watu wachini ka sikuongeza mzigo na watumiaji kupungua zaidi na mawakala kutupa line zao. Uchumi inabidi umaimarishwe kwa kuangalia vitu vingi na sio kuongeza Kodi kwenye kila kitu nchini.
Baada ya muda watu watazoea, jambo lolote jipya hasa linalohusu ongezeko la matumizi lazima liwe na kelele mwanzoni! Nilipo kwa sasa tunapigwa kodi za kufa mtu na watu wanalipa and maisha yanasonga.

Nadhani hata wao wakati zinaanza kelele zilikuwa hivihivi! Muhimu hiyo hela isimamiwe vizuri na itumike kwa malengo tajwa, siyo kuwajaza matumbo akina Wasira! Ikitumiwa vibaya hilo ni jambo lingine, na wananchi watakuwa na hasira haswa.
 
Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lisu ameshauriwa kama mtu mzima aombe msamaha kwa watanzania kwani mtu mzima akivuliwa nguo huchutama na siyo kukimbia uchi.
Hivi zile rasilimali alizokuwa analinda dhalimu ziko wapi ili tuziuze tuondokane na hizi double taxation? Au raslimali zetu ni hizi line zetu za simu?
 
Baada ya muda watu watazoea, jambo lolote jipya hasa linalohusu ongezeko la matumizi lazima liwe na kelele mwanzoni! Nilipo kwa sasa tunapigwa kodi za kufa mtu na watu wanalipa and maisha yanasonga, nadhani hata wao wakati zinaanza kelele zilikuwa hivihivi! Muhimu hiyo hela isimamiwe vizuri na itumike kwa malengo tajwa, siyo kuwajaza matumbo akina Wasira! Ikitumiwa vibaya hilo ni jambo lingine, na wananchi watakuwa na hasira haswa
Mimi kuzoea kwangu ni kuacha kutumia miamala kwa simu, Kodi ya wizi haizoeleki na hii itaua tu uchumi kabisa na jinsi biashara zilivokuwa mbovu haswa. Transcations za miamala kwa simu zifanywe na matajiri tu mie kajamba nani staki kuitumia Wala kuzoea.
 
Back
Top Bottom