Waliomchagua Muheshimiwa mteule John P. Magufuli ni 42% ya wapigakura wote waliojiandikisha

Pia kuna kitu walikuwa wanabishana kabla hajakamilisha kama ulifuatilia Na akasahau kuzima mic. Alisikika akisema "wanatutazama watahisi kuna......." kachukua fomu katangaza.
kama kuna MTU ana clip original ya ITV angalia ila clip za mtandaoni kwa sasa lazima wame edit wakatoe mana hakakukaa vizuri
 
Acha upumbavu wako.Hao ndio walipiga kura ? Mmebwekabweka sana humu JF wakati wa kampeni.Hamjakoma tu kwa matokeo haya ? Nyau nyie !!!!
 
Aloo tumewaza pamoja eti
 
Acha upumbavu wako.Hao ndio walipiga kura ? Mmebwekabweka sana humu JF wakati wa kampeni.Hamjakoma tu kwa matokeo haya ? Nyau nyie !!!!
Milioni 15 ndio walijitokeza kupiga kura. Ambayo ni sawa tu 50%.
Sawa mama!
Kwa haya matokeo au hata kama Lissu angeshinda kwa kweli kila mtanzania inamhusu. Km ni number wote tutaisoma.
Kama Tanzania kua km "Uraya" wote tutachekelea. Huu ndio utamu wa democracy. Una lolote la nyongeza mama?
 
Kumbuka na ktk hiyo 42% kuna kura fake kibao! Binafsi sikuhangaika kwenda uchaguzi kwa sababu wahusika walijulikana toka mwanzo kwamba hawaamini sanduku la kura.

Vitimbi vyote kuanzia kutupwa kwa maelfu ya wagombea kwa kisingizio cha makosa ya fomu na wagombea kupita bila upinzani ilikuwa dhiaka kubwa sana.

Viongozi wa Tume ya Uchaguzi kuonyeshwa asubuhi makaratasi ya kura yaliyo kamatwa yakiingizwa yanaingizwa vituoni bila hatua yeyote kuchukuliwa ulikuwa ni ushahidi wa wazi kwamba hapo hakuna uongozi wala uchaguzi bali vurugu tupu.

Isilaumiwe CCM kwa ujumla wake bali wanayo iongoza sasa ndiyo wamekula njama kufedhehesha taifa! Ni jukumu la CCM kujisafisha na uchafuzi huu walioshirikiana na Polisi na TISS kuchafua uchaguzi! Sifa binafsi za kijinga za boss wao haikua haki kutuharibia uchaguzi.
 
Idadi ya waliopiga kura ni wachache inabidi elimu ya uraia itolewe ili watu wapige kura
 
Mbwebwe zoote zile halafu unapata kura 1,933,271 si utopolo. Lissu hata milele hawezi kuwa Rais wa Watanzania.
 
Ila kashinda asilimia zote waachie internet bana
 
Pia mwaka huu waliopiga kura hawafiki milion maana watu walikuwa hamna vituoni, wazee ndio walikuwa wengi, hyo milion kumi na mbili siamini. In short watu waligomea uchaguzi
 
Pia mwaka huu waliopiga kura hawafiki milion maana watu walikuwa hamna vituoni, wazee ndio walikuwa wengi, hyo milion kumi na mbili siamini. In short watu waligomea uchaguzi
Ni kweli kabisa, wapiga kura hawakufika milioni 10 kabisa, case study za vituoni zinajionyesha dhahiri
 
Ni kweli kabisa, wapiga kura hawakufika milioni 10 kabisa, case study za vituoni zinajionyesha dhahiri
Hata milion tano ni nadra kufika hasa huku Dar ndio usiseme, watu hawapigi kura then baadae wanaanza kulalamika kuhusu uwakilishi, Wanaolia kura kuibwa hata kura hawajapiga
 
Milioni 15 ndio walijitokeza kupiga kura. Ambayo ni sawa tu 50%
Hilo la Chadema ngoja viongozi wao waje jibu bwashee japo ni hoja fikirishi
Mpaka asubuhi ya 28/10 viongozi wa mitaa walikuwa wanapita kwa wanachama wao kucheki wino kwenye vidole. Waliwatumia sms kuwahamasisha wakapige kura.

Kwanini chadema hawakumobilise watu wao? Inashangaza sana. Naimani kabisa, wengi wa hao waliojitokeza kupiga kura ni wanachama wa CCM, maana ni kama walishurutishwa.

Chadema wanatakiwa waende likizo, alafu vigogo wao watupwe nje, walete damu mpya. Maana hawa waliopo wanafanya siasa za kukariri. Haiwezekani miaka 5 ya Magu, wawe wameshindwa kupata njia ya kupambana naye, wanang´ang´ania mbinu zile zile za enzi zote.

Wapate uongozi mpya alafu wafanye zoezi la kusajili wanachama wao, wawajue. Jinsi Bashiru alivyofanya. CCM hata wakati wa korona, walikuwa wanatumia wanachama wao sms na ushauri jinsi ya kujikinga!

Waache kulalamika tu kila siku, haiwasaidii. Wabadilike. Wajipange. 2025 sio mbali.
 
Kachaguliwa na NEC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…